BAWACHA: Spika Ndugai kuita barua rasmi kipeperushi ni kiburi cha madaraka. Amekuwa Mtetezi wa wanawake kuanzia lini?

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,167
Hotuba ya Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu

Tarehe 20 April 2021 Naibu Spika alitoa kauli Bungeni kwamba ofisi ya Spika haikuwa na taarifa rasmi ya CHADEMA kuhusiana na kuvuliwa uanachama kwa waliokuwa wanachama wake 19.

Ibara ya 67 (1)(b)ambayo imeweka masharti na sifa za mtu kuteuliwa kuwa Mbunge kuwa ni lazima awe amependekezwa na Chama cha siasa ‘ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.

Mei 3, 2021 Spika ameonyesha Barua aliyopokea kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Bungeni. Hii inaonyesha nia ovu kwenye ofisi ya Spika. BAWACHA tunamtaka Spika aueleze umma ni lini alipokea barua hiyo na pia kutoa ufafanuzi wa kwanini kunakuwa na kauli mbili kinzani ndani ya ofisi

Spika pia amezungumzia Suala la viambatanisho kwenye barua,hii ni hoja isiyokuwa na mashiko kwani si mamlaka ya Spika kudai viambatanisho hivyo. Ni dhahiri kwamba Spika anatengeneza hoja zisizo na msingi juu ya udhaifu wake katika kutekeleza matakwa ya kikatiba aliyoapa kuilinda.

BAWACHA tunajiuliza, je wakati CCM kinamuandikia barua ya kumvua uanachama Sofia Simba au wakati CUF wanamuandikia barua ya kuwavua uanachama wanawake 8 waliokuwa wabunge wa viti maalum alikuwa wapi kudai viambatanisho hivyo? Au huu utaratibu ni kwa CHADEMA tu?.

Hata hivyo badala ya kujibu barua ya Katibu mkuu, Spika ameibuka miezi mitano baadae na kuzungumza bungeni ambako si njia rasmi ya mawasiliano lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa CHADEMA ndani ya Bunge anayeweza kujibu hoja hizo.

Hii inaonyesha namna gani Spika anavyotumia vibaya madaraka yake na kuonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi.

Katika maelezo yake Spika ameiita barua aliyoandikiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA “Kipeperushi”. Hii ni dharau kubwa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini kilichosajiliwa kisheria.

Kuiita Barua rasmi kipeperushi inaendelea kuonyesha kiburi cha madaraka alichonacho Spika ambacho kinaendelea kumshushia hadhi mbele ya jamii.Sisi Baraza la Wanawake Chadema hatutakuwa tayari kuona viongozi wetu wakidhalilishwa na chama chetu kikidharauliwa na tena.

CHADEMA ina katiba yake na ndani ya katiba hiyo kuna miongozo, kanuni na taratibu kuhusu vikao na uendeshaji wa Chama. Kwa muktadha huo mkutano wa Baraza Kuu ambalo litapitia Rufani iliyokatwa na waliokuwa wanachama hao litakaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Hata hivyo kukata rufani hakutengui maamuzi ya awali mpaka hapo rufani hiyo inaposikilizwa na maamuzi kutoka tofauti na maamuzi ya awali.

Kitendo cha Spika kutochukua hatua kwa kuwa kuna rufani imekatwa kupinga maamuzi ya awali linaonyesha namna gani alivyo na nia ovu juu ya jambo hili kwani anaelewa namna taratibu zilivyo na kwa makusudi ameamua kupindisha. si mamlaka ya Spika kuingilia mambo ya ndani ya chama.

Sisi Baraza la Wanawake Chadema tunapenda kuwahakikishia umma wa watanzania kwamba Chama chetu hakina mfumo dume kwa sababu, mosi, ndio chama chenye wajumbe wengi wa kamati kuu wanawake (9) kuliko vyama vingine vyote vya siasa kikiwemo Chama anachotoka Spika.

Katika kikao kilichofanya maamuzi ya kuwavua uanachama kulikuwa na wajumbe Wanawake 4 kwasababu wengine 5 walikuwa kwenye kundi la watuhumiwa.

Pili, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Chama chetu ndio kilipitisha wanawake Zaidi ya 60 kugombea nafasi za ubunge wa majimbo kuliko vyama vingine vyote pengine kwenye ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati.

Leo hii Spika anajivika hadhi ya kuwa mtetezi wa wanawake huku akiwa amesahau kwamba ni yeye ambaye Bunge lililopita alikuwa mstari wa mbele kutweza haki za wanawake kiasi cha kuwafukuza bungeni wanawake ambao baadhi ni sehemu ya hao wanaoitwa wabunge 19 kushiriki vikao.

Spika Mtetezi wa wanawake, amekuwa akitumia askari wa kiume kuwaondoa Bungeni baadhi ya hao wanaoitwa wabunge 19 bila kujali jinsia zao

Wakati Halima na Esther walipopigwa na kuumizwa na askari Magereza Spika alionekana kufurahia tukio hilo. Hivyo ni unafiki mkubwa kujivika kilemba cha kujifanya ni mtetezi wa haki za wanawake.

Katika Bunge lililopita Chama cha Wananchi (CUF) kiliwavua uanachama wanachama wake 8 Wanawake waliokuwa Wabunge wa Viti Maalum na pale Spika alipoandikiwa barua aliwaondoa Bungeni mara moja.

Kwenye barua yake Spika alisema “Suala la kuwavua uanachama wanachama ni suala la utashi wa chama” sasa iweje leo Spika huyo huyo ajisahaulishe kuwa amewahi kuwavua ubunge wabunge 8 Wanawake kwa mara moja na leo hii kujifanya amegeuka ghafla kuwa mtetezi wa wanawake?

CADEMA imewahi kuwavua uanachama wabunge wake 4 wa kiume, je na huo pia ulikuwa mfumo jike kama anavyodai sasa hivi kwamba Chadema ina mfumo dume?.

Kikao kilichokaa na kuwavua uanachama wanaoitwa wabunge 19 ni kikao halali cha Kamati Kuu ya Chama ambacho kinaundwa na wajumbe wa jinsia zote na kina mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.

Wakati wa kusikilizwa kwa shauri la kuwavua uanachama, waliokuwa wanachama hao waliitwa kwa barua kuhudhuria kikao hicho ili waweze kusikilizwa lakini walikataa kuhudhuria hivyo shauri lao likasikilizwa bila wao kuwepo.

Kwa mujibu wa taratibu pale unapoitwa na ukakaidi kuhudhuria basi haki yako ya kusikilizwa inapotea hivyo shauri lako litasikilizwa upande mmoja (ex parte hearing).

Suala la maridhiano ni baina ya CHADEMA na Rais na kwa kutambua umuhimu wake CHADEMA ilimuandikia barua rais naye pia kwa kutambua umuhimu wake akakubakubali hivyo halina mahusiano yoyote na Spika.

Baraza la Wanawake CHADEMA tunaona kama Spika ana lengo la kuvuruga mazungumzo hayo huenda akawa na manufaa binafsi kuona nchi iliyogawanyika.

Pia tunapenda kumwambia Spika kwamba chama chetu hakina mgogoro wowote na hata pale kunapotokea mgogoro Katiba yetu inatuongoza namna ya kushughulika na utatuzi ndani ya chama.

Suala tunaloliongelea ni kuhusiana na waliokuwa wanachama wetu ambao tuliwavua uanachama kwa kosa la usaliti, uasi, ubinafsi na kugushi nyaraka za chama na ni jukumu la Spika kufanya kazi yake na sio kuwa mshauri wa namna ya kuendesha chama chetu.

Kwa maelezo yake,Spika amesema hapangiwi lini achukulie hatua suala la wanaoitwa wabunge 19. Spika anatakiwa atambue kwamba suala la utekelezaji wa Katiba si suala la utashi wa yeye kuamua ni lini achukue hatua. Hivyo tunamtaka Spika atekeleze matakwa ya kikatiba.

Taratibu za upatikanaji wa Wabunge wa Viti Maalum kwenye Chama huanzia ngazi ya chini kabisa kabla ya kufikia Kamati ya Utendaji na kisha Sekretarieti ya BAWACHA Baada ya hapo majina hupelekwa kwenye Kamati kuu ambayo hupitisha majina na kuyawasilisha Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Hivyo basi wanaoitwa wabunge 19 kujichagua na kujipeleka kwenda kuapa sio tu kwamba ni uvunjaji wa Katiba ya Chama Bali ni kiwango cha juu kabisa cha ubinafsi, uasi na usaliti.

Tunamtaka Spika atueleze wakati anawaapisha wanaoitwa wabunge 19, aliwaomba nakala ya Katiba, muhtasari nanyaraka nyingine anazozitaka Sasa hivi?.

Mwisho tunawaomba waandishi wa habari na umma tuendelee kumuuliza maswali ya msingi Spika kama tulivyoainisha hapo juu lakini kubwa likiwa ni kwanini anaendelea kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda? Je, anaweka mfano gani kwa wananchi.

Kwamba leo wanaweza kuvunja Katiba kama anavyofanya yeye kwa kiburi na wasichukuliwe hatua? Na je hizi hoja zake, zinailenga CHADEMA peke yake au ana maslahi binafsi na wanaoitwa wabunge 19?.

Tunazitaka Kamati za Utendaji za BAWACHA kila Jimbo kukutana hara kwa ajili ya kujadiliana hatua stahiki za kuchukua juu ya suala hili kwani sisi kama chama tutasimamia utekelezwaji wa Katiba ya JMT na hatutakuwa tayari kuona mtu yoyote, mwenye madaraka yoyote akiivunja katiba.

Baada ya kupokea mapendekezo kutoka Majimboni tutatoa maazimio ya hatua gani tutachukua kushinikiza utekelezaji wa jambo hili. Haijalishi kama wangekuwa wanaume au Wanawake kama ilivyo Sasa, pale Katiba itakapovunjwa tutasimama, kukemea na kuchukua hatua.

Tunamtaka Spika sio tu ajisifie ni miaka mingapi amekaa ndani ya bunge, bali aangalie kwenye kipindi cha uongozi wake ameacha alama gani chanya kwenye Taifa.

"Alama hizi lazima ziwe zile zinazotuunganisha kama nchi, kuleta Amani, haki na usawa kwa wote huku ikiweka misingi ya kuheshimu Katiba, Sheria na taratibu mbalimbali tulizojiwekea.
 
Hivi kwanini chama na wanasheria wasifungue kesi ya kikatiba haraka na waombe hati ya kesi hiyo kuendeshwa kwa haraka?
 
Bawacha na bavicha kwa ujumla wenu mlishindwa kutoa tamko mwaka 2015, wakati mwenyekiti alipopachika "mamluki" ndan ya chama kugombea uraisi na ubunge bila kufuata sheria wala kanuni za chama. Leo hii ndo mnajifanya kuonea dagaa huku papa akiendelea kutembea na akili zenu mfukoni.
 
Hivi mnachohangaikia na hao wanawake ni nini? Simmewafukuza bado mnataka nini?

Huwezi kumlazimisha spika afanye unavyotaka wewe ile ni ofisi yake anataka viambatanisho wewe unamletea mambo ya kina sophia sima mtakaa hapo mtapiga kelele mpaka 2025
 
Hivi mnachohangaikia na hao wanawake ni nini? Simmewafukuza bado mnataka nini?

Huwezi kumlazimisha spika afanye unavyotaka wewe ile ni ofisi yake anataka viambatanisho wewe unamletea mambo ya kina sophia sima mtakaa hapo mtapiga kelele mpaka 2025
Halafu Hata Mm Pia Nashangaa Mnaangaikaje na Watu Ambao Hata Hawahusu na Mlishawafukuza, Ndugai Kashasema Wako Bungeni Kwa Sababu yake na Sio Kwa Sababu ya Cdm.
 
Back
Top Bottom