Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,272
- 2,033
Kwa jinsi walivyopatikana na kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Wabunge Viti Maalum ni wazi kuwa ni chawa wa CCM. Kuthibitisha hilo ni jinsi Mihimili yote 3 inavyotumia nguvu kubwa kuwalinda licha ya ukweli kuwa CHADEMA haikuhusika katika Mchakato wao wa Kuteuliwa kuwa Wabunge Viti Maalum.
Mfano mdogo tu je, CHADEMA ingeweza kumtoa Gerezani mmoja wa hao Wabunge aende akaapishwe na SPIKA? Jibu ni HAPANA.
Mfano mwingine Angalia jinsi Spika anavyowakumbatia licha ya Mahakama kutamka katika Hukumu kuwa Wabunge hao sio wanachama wa CHADEMA kwani walifukuzwa kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi inatamka wazi kuwa Huwezi kuwa Mbunge kama sio Mwanachama wa Chama cha Siasa.
Mfano mwingine ni Serikali kuendelea kuwalipa Posho na Mishahara ilihali ikijua SIO wanachama na sio Wabunge kwa mujibu wa Katiba.
Kutokana na yote hayo Wabunge 19 wasio na Chama ni CHAWA wa CCM.