Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi yagaragazwa Bungeni

Amemtaja Juma Kapuya kama mwanahisa wa Kampuni ya Simons group iliyouziwa UDA, na anasema kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza sakata lote Kapuya nae alikuwepo, kwa hiyo ni kama kesi ya nyani kumpelekea ngedere, amemtaka Kapuya kudeclare interest na kuomba radhi kwa kuidanganya kamati.
Amesema serikali haitaki kutoa tamko kazi yake ni kuomba miongozo tu na kuchukua hiyo hela na kujenga mahekalu Ulaya.
 
AHSANTE SANA ENDELEA KUTUJUZA MKUU NAAMINI UNA JENERETA WEWE,HUKU TANESCO TOKEA ASUBUHI WAMETUGAWIA GIZA SIJUI JIONI WATATUGAWIA nini
Mkuu Ngeleja hajafika kwetu situmii jenereta
 
Hivi huyu Nundu si nasikiaalikuwa anaishi nje ya nchi mda mrefu tu hakuwa nchini sasa anatambuaje matatizo ya wananchi? Bila aibu jk amemwita kuja kugombea jimbo la tanga mjini na akampa uwaziri..naona hatofautiani na Masha labda wanatofautiana wizara tu,.
 
Pamoja na hilo usishangae tangazo kusikia kuwa wabunge wa ccm kukutana mchana, then baada ya muda budget inapita.
Si waamini kabisa wabinge wa ccm.

Kama wanaweza kutengewa rushwa ya shilingi bilioni moja na Madini na Nishati ili wapitishe bajeti ya Wizara ile basi wanaweza kufanya chochote kile ikiwemo ahadi za kuneemeshwa ali mradi tu hiyo bajeti ya Uchukuzi ipitishwe. Umesikia yeyote kati ya Kikwete, Pinda au Makinda kufuatilia Wabunge waliochukua rushwa toka nishati!? Wote wako kimya kabisa ili kulinda maslahi yao wenyewe na ya chama chao cha magamba
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Amemtaja Juma Kapuya kama mwanahisa wa Kampuni ya Simons group iliyouziwa UDA, na anasema kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza sakata lote Kapuya nae alikuwepo, kwa hiyo ni kama kesi ya nyani kumpelekea ngedere, amemtaka Kapuya kudeclare interest na kuomba radhi kwa kuidanganya kamati.
Amesema serikali haitaki kutoa tamko kazi yake ni kuomba miongozo tu na kuchukua hiyo hela na kujenga mahekalu Ulaya.

Huyu kapuya waliopo kwenye teaching staff ya UDSM, tuelezeni alipatataje Uprof wake? maana hana maadili ya mtu mwenye taalum (proffessional ethics), shame on him........watu kama hawa huwa nawahurumia watotot wao ambao they have to live with all this na hawana jinsi maana hawakuchagua wazaliwe na nani!
 
Zitto anasema ana barua ya waziri wa Miundo mbinu ambayo alimwandikia waziri Mkuu barua ya kuomba kuongezewa fedha kwa ajili ya wizara yake lakini waziri Mkuu hakuifanyia kazi barua hiyo.

Ameomba wafanye retreat, serikali/wizara irudi ikakae itafute fedha ije na bajeti ambayo itakidhi miradi ya wizara yake.
 
Zitto amemshanga mwenyekiti wa kamati kwa nini amekubali bajeti yenye matatizo mengi hivi ipite.
Anaendelea kusisitiza serikali irudi ikakae upya
 
Jamani ilibidi niache kazi nisikilize hiyo bajeti. Mbowe amemzodoa Waziri mkuu na kumshangaa kwamba inakuwaje madudu hayo wayajadili kwenye baraza la mawaziri. Amezungumzia ulaji wa KIA na mabo kadhaa
Mama Maria hewa ( CCM) amesema ni aibu sana kwa serikali kutokujua umuhimu wa reli ya kati. Ameomba wabunge wasiipitishe bajeti hii. Amehoji ulaji wa pesa za ujenzi uwanja wa ndege Mwanza, na umakini wa waziri kufufu ATCL
Naye mbunge wa Mafia (CCM), ameipinga na kumwomba waziri mkuu awakamate Meya wa DAR and wale wawili walioamua kujiuzia UDA. Ametaka TAKUKURU iingilie kati swala la UDA na isiangalie uso wa mtu mpaka kieleweke . Amepinga Bajeti
Naye Kariuki (CCM) ameonge kwa uchungu na kuipondelea mbali bajeti kwa kutojali mipango ya Reli.
Kwa ujumla Omar Nundu ameonekana mtupu kabisa na Baraza zima la mawaziri limumbuka.
Kama hawatazimwa mchana, bajeti hii haipiti!
we

Hiyo bajeti itapita tu!
Kukwama kwa hii bajeti itakuwa ni picha mbaya ya utendaji wa serikali nzima iliyoko madarakani! Kwa sababu yote anayotwishwa Omari Nundu,yeye kayakuta hivyo hivyo si yeye...mambo ya TRL ,UDA yenyewe ilijifia zamaniiiiiiiiii,walikula kidogokidogo mwishowe wameamua kuchukua jumla! ATCL ndo usiseme wakubwa walijiulia ili ngalau tundege twao tupate abiria wa kutosha....sasa nundu ana mwaka mmoja pale...
si wanamnyonga bure kabisa!
 
Zitto ameomba wabunge wote waacha ushabiki wa kisiasa waikatae bajeti hii ili wawafute machozi watu wa Kigoma
 
we

Hiyo bajeti itapita tu!
Kukwama kwa hii bajeti itakuwa ni picha mbaya ya utendaji wa serikali nzima iliyoko madarakani! Kwa sababu yote anayotwishwa Omari Nundu,yeye kayakuta hivyo hivyo si yeye...mambo ya TRL ,UDA yenyewe ilijifia zamaniiiiiiiiii,walikula kidogokidogo mwishowe wameamua kuchukua jumla! ATCL ndo usiseme wakubwa walijiulia ili ngalau tundege twao tupate abiria wa kutosha....sasa nundu ana mwaka mmoja pale...
si wanamnyonga bure kabisa!

LABDA ILA TUTAONa
 
Kuhusu UDA anasema kama kuna mtu amenunua hisa za UDA ameingia choo cha Kike. Anasema kama mwenyekti wa kamati ya mashirika ya umma UDA haijauzwa.
 
Zitto amemshanga mwenyekiti wa kamati kwa nini amekubali bajeti yenye matatizo mengi hivi ipite.
Anaendelea kusisitiza serikali irudi ikakae upya

mwenyekiti kashapewa chake akakaa kimya! by the way who's Mwenyekiti
 
Zitto amemshanga mwenyekiti wa kamati kwa nini amekubali bajeti yenye matatizo mengi hivi ipite.
Anaendelea kusisitiza serikali irudi ikakae upya

Hivi Mwenyekiti wa kamati ya wizara hii ni nani?na wenzie ni akina nani? ..lazima watakuwa wamekula ka....billioni hao, Unajua namkumbuka marehemu Faresi Kabuye aliyewahi kusema kuwa "wabunge wengine ni kama kuku kwani wakiingia kulala hapohapo wanakunya mavi asubuhi wanatoka kwenda machungani usiku wanaingia mlemle walimokunya usiku"
 
Amemaliza Zitto na ameanza Deo Sanga, ameanza kuishukuru serikali ya CCM kwamba inafanya kazi nzuri, anazungumzia bajeti ya miundombinu ya jana, huyu jamaa vipi?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom