Baba bora wa JF

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Kwanza nianze kwa kusema sina hatimiliki na mtandao huu,na hivyo sina mamlaka ya kuanzisha ushindani wa aina yoyote ndani ya jukwaa hili na majukwaa mengine.

Baadhi yetu ni vijana wadogo ndio tunaelekea kuitwa baba. Haina ubishi kuwa baba ni kiungo kikubwa katika familia,ni kichwa,wengine huenda mbali na kusema kuwa baba ni rais na mama pengine ndiye Makamu wa rais. Kwa sifa zote hizi bado ipo changamoto ya kumjua baba bora.

Katika uzi huu ningependa tujadili kwa hoja ni kwa jinsi gani unavyomfahamu baba bora.Baba huyu aweza kuwa wewe mwenyewe,baba yako anayeishi au ambaye ametangulia mbele ya haki.

Kuna mambo wewe kama baba,au babako mzazi umeyafanya,anayafanya au aliwahi kuyafanya,na mpaka sasa umekuwa msingi mkubwa na mweongozo wa maisha yako.

Mfano mimi baba yangu ni mtu mwenye kujiamini na kujigamba kupita kiasi,lakini mimi nimechukua tabia ya kujiamini na kuona ndo inanifaa. Babu yangu ambaye ni baba wa baba yangu alikuwa ni mtu mpole na msikivu tabia hii pia nimeinyaka.

Je wewe kama baba ukoje, babako yukoje au alikuwaje?

Karibuni.
 
Haya Mababa mtueleze vile tabia zenu ziko..kama wasununu,kama macho ya juu,kama mnakula kwa macho,kama mmepewa nyama mkanyimwa meno hayaaaaaa uwanja huooooooo!!!!!!!!!!
 
Kwanza nianze kwa kusema sina hatimiliki na mtandao huu,na hivyo sina mamlaka ya kuanzisha ushindani wa aina yoyote ndani ya jukwaa hili na majukwaa mengine.Baadhi yetu ni vijana wadogo ndio tunaelekea kuitwa baba.Haina ubishi kuwa baba ni kiungo kikubwa katika familia,ni kichwa,wengine huenda mbali na kusema kuwa baba ni rais na mama pengine ndiye Makamu wa rais.Kwa sifa zote hizi bado ipo changamoto ya kumjua baba bora.Katika uzi huu ningependa tujadili kwa hoja ni kwa jinsi gani unavyomfahamu baba bora.Baba huyu aweza kuwa wewe mwenyewe,baba yako anayeishi au ambaye ametangulia mbele ya haki.Kuna mambo wewe kama baba,au babako mzazi umeyafanya,anayafanya au aliwahi kuyafanya,na mpaka sasa umekuwa msingi mkubwa na mweongozo wa maisha yako.Mfano mimi baba yangu ni mtu mwenye kujiamini na kujigamba kupita kiasi,lakini mimi nimechukua tabia ya kujiamini na kuona ndo inanifaa.Babu yangu ambaye ni baba wa baba yangu alikuwa ni mtu mpole na msikivu tabia hii pia nimeinyaka.Je wewe kama baba ukoje,babako yukoje au alikuwaje?Karibuni.

Aiseee, mimi kama baba bora majukumu yangu ni kuhakikisha familia yangu inapata mahitaji yote muhimu (chakula, malazi, mavazi, elimu, na ulinzi) kwa juhudi zangu mwenyewe. Pia ni jukumu langu kuishauri familia katika mambo yote muhimu kuhakikisha hatuingii kwenye matatizo yasiyo ya lazima. Zaidi ya hapo, ni wajibu wangu kumpenda, kumlinda, kumtunza, kumhudumia,kuwa karibu na kumpa heshima zake mke wangu ili asijutie maamuzi ya kuwa mke wangu!

Napendelea pia kupata wasaa wa kufanya kazi za ziada, kubadilishana mawazo na kushiriki michezo ili kujenga mwili. Na la mwisho, hupenda kushirikiana na jamii iliyonizunguka, marafiki na ndugu zangu wote kwenye mambo yote muhimu ya kijamii na kiuchumi.
 
Haya Mababa mtueleze vile tabia zenu ziko..kama wasununu,kama macho ya juu,kama mnakula kwa macho,kama mmepewa nyama mkanyimwa meno hayaaaaaa uwanja huooooooo!!!!!!!!!!

Kweli kabisa uwanja ni wao.
 
Katika maisha yangu yote sijawahi kuona baba bora kama Baba Yangu. Na hii ni Tanzania nzima, kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Yote, Ulaya, Amerika, Asia, AUstralia na Dunia yote kwa ujumla.

Kinachonishangaza, hata vibinti vyangu vinanisifia kama mimi navyomsifia dingi angu. tena vinaongeza na kachumbari kabisa.

Sasa baba wa JF si ni asiyeonekana Invisible? Basi atakuwa ndo baba bora wa JF.

Konklushen: Kila mtu atamsifia baba yake

Topic Klozd!!
 
Kwa mwanaume yeyote ukimuuliza atakuambia yeye ndiyo baba bora, ungeweka vigezo. Kwa mfano mimi najichukulia kama ndiye baba bora kuliko woote na anayebisha nitampa vigezo vyangu nilivyotumia lazima akubaliane na mimi.
 
Sikiliza wimbo wa Nikki wa Pili--imma good boy

"Kama baba wa kweli akikisha nyumbani hawakosi mlo,mavazi na makazi mazuri",ungo dekoda mwendo dstv zinga la tv na deki ya dvd bonge la mziki linatwanga tu cd,bafuni sinki hakuna bali jakuzi screen kila chumba tunacheki tu movies!!
 
Katika maisha yangu yote sijawahi kuona baba bora kama Baba Yangu. Na hii ni Tanzania nzima, kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Yote, Ulaya, Amerika, Asia, AUstralia na Dunia yote kwa ujumla.

Kinachonishangaza, hata vibinti vyangu vinanisifia kama mimi navyomsifia dingi angu. tena vinaongeza na kachumbari kabisa.

Sasa baba wa JF si ni asiyeonekana Invisible? Basi atakuwa ndo baba bora wa JF.

Konklushen: Kila mtu atamsifia baba yake

Topic Klozd!!

Hahahaaaaa na kweli mwaya hata mie nitampa baba yangu misifa kibao!
 
Mimi nimeshasema mengi sana hapa na ninajua ukimuuliza mhusika atakuambia hakunaga baba kama mimi.
 
Hivi nimekusahauje?Hata wewe unaonekana ni baba mzuri, ila unaonekana utamdekeza sana matoto wa kike.

Hapana, huyu ambaye ninaye simdekezi bali ninampenda sana na ninamuonyesha kuwa ninampenda. Ninamfunza mbinu mbalimbali za kimaisha ili ikija kutokea sipo tena hapa duniani asije kushindwa ama kuhangaika sana na namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Na kama shuleni anafanya vizuri na ni mtoto mwenye tabia nzuri basi nami ni jukumu langu kuhakikisha anapata mahitaji na matakwa yake yote ambayo yako ndani ya uwezo wangu.
 
Mmmmh, unaonekana una-komitimenti kubwa, good for you.

Umeongea kama askari anatoa 'kiapo cha utii'

Back
Top Bottom