Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,895
NDOA NI LAZIMA KWA WATU WANAOTAKA KUWA NA FAMILIA NA KIZAZI BORA, ILA KIZAZI CHA MBWA AU NYOKA NDOA SIO LAZIMA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Kama hutaki kuzaa watoto na kuwafanya wawe watoto bora wenye malezi ya Baba na Mama. Basi kwako Ndoa sio lazima.
Ndoa sio ishu ya Sex pekee. Sex unaweza pata popote. Sex unaweza hata kulala na mnyama, au kununua midoli, kujichua au hata kununua Kahaba. Hizo zote ni Sex.
Lengo la Ndoa sio sex au ngono kama Watu wengi wenye upeo Mdogo wanavyofikiri. Ndio maana kwa wale ambao wapo ndoani watakubaliana na mimi kuwa tendo la ndoa linachukua asilimia 10% tuu ya maisha ya ndoa. Ingawaje ni moja ya nguzo muhimu katika ndoa.
Huwezi sema unakataa ndoa alafu muda huohuo unawatoto. Labda uwe mwehu. Mtoto anahitaji malezi ya Baba na Mama tena wanaoishi pamoja.
Baba pekee hana uwezo wa kumpa mtoto malezi Bora. Wala Mama pekee hana huo uwezo wa kumpa mtoto malezi Bora. Ila wote wawili nusu kwa nusu wanachangia malezi bora kwa watoto wao.
Mtoto kimwili anachukua vinasaba nusu kwa nusu kutoka kwa Baba na Mama.
Vivyohivyo kwenye ishu ya hisia, akili, na mambo ya kiroho.
Mtoto kukua pasipo malezi ya Wanandoa inampa nafasi kubwa ya kuwa kizazi cha mbwa au nyoka. Yaani anakuwa kama Mnyama fulani hivi.
Mtoto bila malezi ya Baba na Mama ni sawa na wananchi bila serikali. Yaani hapo muda wote ni fujo, uhalifu, vurugu, uasi, uovu, usalama unakuwa hafifu.
Ndoa, Baba na Mama ni serikali kwa ngazi ya familia. Sasa mtu anayekuambia Ndoa sio lazima alafu anataka watoto ujue kuna nati ya kichwa haijakaa vizuri.
Wewe kama Baba au Mama ambaye ni mtawala katika serikali yako ya familia ni wajibu wenu kuhangaika kujenga serikali yenu. Sio changamoto Kidogo unakimbia, unaacha familia bila utawala. Unategemea nini.
Hata Serikali inapopata changamoto inapambana nazo. Wakitokea waasi au vurugu unatafuta namna ya kuzima.
Sasa mwanamke au mwanaume umechagua mwenyewe, hakuna aliyekulazimisha kuoa au kuolewa. Hakuna aliyekulazimisha kuanzia familia na kuingia ndoani.
Umepata watoto badala upambane kujenga familia na kizazi bora unaleta mambo ya kitoto.
Kama mkeo au mumeo anakusumbua, itabidi upambane hivyohivyo kuweka mambo sawa mpaka watoto wakue, wawe Watu wazima ndio uvunje hiyo serikali yako.
Ni kweli umalaya, ubinafsi unaumiza sana ndani ya familia. Lakini ukishakuwa na watoto, elewa watoto ni muhimu kuliko hayo mambo yenu ya umalaya na ubinafsi.
Mnaweza kuendelea kuishi mkiwa mmetengana kwa maslahi ya watoto. Mkisubiri wakue angalau umri wa kujitambua yaani Watu wazima.
Miaka 20 sio mingi kihivyo.
Maelezo haya ni kwa wale waliokosa bahati na kujikuta wamekosea kuoa au kuolewa na Watu wasio sahihi.
Sio unazalisha au kuzalishwa kama Mbwa. Yaani kila mtu na Baba au Mama yake. Hiyo haijakaa sawa.
Ikiwa imetokea huna namna nyingine na mmetengana iwe kwa Kifo, au kutalakiana. Ni vizuri uoe au kuolewa ili watoto wawe ndani ya ndoa. Au kumpeleka mtoto kwenye familia ambayo iko na ndoa imara.
Iwe ni Bibi na Babu., Kakaako ambaye ameoa, yaani wanandoa.
Ínashauriwa, hata siku ukiona unataka kufa au unaona hauna uwezekano wa kutoboa kiafya, watoto wako ni muhimu kuwakabidhi kwa ndugu yako au rafiki yako ambaye unajua kabisa ndoa yake iko imara. Maadili na malezi kwa mtoto ni muhimu kuliko maisha mazuri.
Acha Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam