Nilisababisha mama mkwe kupewa taraka, kosa Moja tu

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,187
1,834
MY STORY; NATAMANI NINGEKUA NA NGUVU YA KUMUACHA MKE WANGU KAMA ALIVYOFANYA BABA MKWE!

Kila tulipogombana na mke wangu, alikuwa mtu wa kukimbilia kwao. Akifika huko, mama yake ananipigia simu ananitukana wee, mimi nitaomba msamaha hata kama ni kitu cha kijinga namna gani. Lakini kama mwanaume, sina namna, naomba msamaha.

Anaweza kukaa kwao wiki mbili, halafu bila ya mimi kumuomba msamaha, anarudi eti bila hata kujali kama nimeumia au la, anarudi ndani. Kwa kuwa mama yake alikuwa ananipigia mara kwa mara, mimi niliamini kweli yuko kwao.

Hali hiyo ilikuwa inanitesa sana kwani ni mambo ya kawaida, kwa mfano kuzidisha chumvi kwenye mboga, nikiiongelea atalalamika kuwa namnyanyasa kisha kiguu na njia, anaenda kwao. Nikawa makini sana kuto muudhi, lakini kuna kipindi kingine unakuta hata ukimfanyia nini, haongelei mambo ya kwao, nikaanza kushangaa kuna nini mbona kuna kipindi naksoa haondoki ila kipindi kingine ni yeye analazimishia makosa!

Kwani ilifikia hatua, akitaka kwenda kwao, basi hata kama sijamkosea, atatafuta kosa la lazima anakasirika na kuondoka.

Kuna kipindi nilisema huu ujinga, alipoondoka kwenda kwao, sikupiga simu kuomba msamaha, lakini jioni yake nilikusanya vitu vyake mpaka kwao. Nikafika nikamkuta mama yake ananiuliza mbona umekuja na vitu, namuambia "si binti yako yuko kwenu, nimechoka habari zake za kila siku kuondoka, nimekuja kumpa talaka na sitaki kusikia kuhusu yeye."

Baba yake alikuwepo, na kushangaa, mama yake anataka kunitoa nje ili tuongee, nikamuambia "hapana, tutaongea hapa hapa mbele ya baba." Niliongea kila kitu mbele yake huku mama akijaribu kunizuia ila sikutaka kunyamazishwa.

Baba alikua kama anashanga akaniambia mbona haapa hajaja na niemtoak kuongea anye muda si mrefu! "Binti yangu nimeongea naye sasa hivi kwenye simu, ananiambia yuko kwako na hakuna shida yoyote, na hayo mambo unayosema kuwa kila mkigombana anaondoka mbona hajawahi kuja hapa nyumbani kuniambia kagombana na mume wake."

Mama akataka kuzuga, lakini baba mkwe akakaza, akamuambia anataka kujua nini kimetokea hapa, "nataka kujua binti yangu yuko wapi na haya mambo anayoongea mume wake, kama ni ya kweli au la." Mama akaanza kujing'ata ning'ata, baba mkwe akacharuka na kumuambia "chukua simu, mpigie binti yako na weka sauti kila mmoja asikie."

Mama aligoma, lakini baba mkwe alichukua ile simu ya mke wake na kumpigia mke wangu, hakusema kitu ila ile "haloo" tu, mke wangu akamuambia "Mama, nitakupigia, niko na mkwe wako hapa, anakusalimia..." Aliongea huku akijichekesha, baba mkwe akawa anamuangalia mke wake ili aongee, mama akagoma kabisa kuongea.

"Mkwe gani unamzungumzia wewe!" baba alimuuliza, lakini kusikia sauti ya baba yake, mke wangu alikata simu.

Nilimuona yule mzee akiwa anabadilika uso kuwa mwekundu, yaani kama kuna moto unamuwaka kwa ndani. Aliingia ndani akiwa amevaa kanzu, kisha akarudi akiwa kawaida amevaa suruali yake ya jeans. Alimshika mkono mke wake bila kusema chochote, mke wake alianza kupiga kelele za maumivu huku akisema kila kitu. Yule mama nusu kujikojolea mpaka nilimuonea huruma, alisema kipindi chote mke wangu alipokuwa anaondoka, hakuwa akirudi nyumbani bali alikuwa akienda kwa mwanaume wake mwingine.

Mke wangu kuna mwanaume alikuwa naye tangu kipindi yuko chuo, hivyo siku mwanaume akimhitaji anajifanya kugombana na mimi ili kurudi nyumbani, na alikuwa anamtumia mama yake kama kisingizio cha kutoroka kwangu. Aliongea kila kitu, jinsi alivyokuwa anamhudumia mtoto wake, jinsi anavyohudumiwa na huyo mwanaume, na hata pale nyumbani huyo mwanaume alishakuja.

Baba alimuachia, nilimuona akitoka nnje akaja na majirani wawili, akaingia tena ndani akarudi na kalamu na karatasi, akamwandikia talaka akamuambia, "Nimekuacha, wewe si mke wangu, sitaki kuwa na mke kama wewe." Alinigeukia na kuniambia, "Mimi nishamalizana na mke wangu, huyu ndiyo halali yangu, sijui kuhusu wewe, siwezi kukupangia cha kumfanya mke wako."

Baba alitoka na kunicha mimi na mama mkwe anaalia, wale majirani waliondoka, mama akaanza kulia kuomba nimuombee msamaha. Kwakweli nilimuonea huruma, ingawa alikuwa na makosa, lakini uamuzi wa Baba ulikuwa wa ghafla, si kitu nilichokitegemea, hata mimi kupeleka vitu vya mke wangu ilikuwa kama namtishia, sikua tayari kumuacha.

Mama aliniomba sana msamaha huku akilia, akampigia simu binti yake huku akilia. Binti aliposikia, alinipigia simu, akaanza kunilaumu kwa kuharibu ndoa ya mama yake, alinitukana sana na kuniambia hanitaki.

Sijui kwa nini, lakini nilijikuta mimi ndiye naomba msamaha. Nilimuomba sana msamaha mke wangu, kuwa sikutarajia, lakini hata hivyo hakunisikiliza. "Kama ushaleta vitu vyangu nyumbani kwetu, ondoka, sitaki kukuona hapo. Na kama ni talaka, mpe mama yangu nitaikuta!" aliniambia. Lakini niligoma kumpa mke wangu talaka. Niliondoka pale na kumuacha mama mke wangu, lakini jioni nilipigiwa simu na mama mdogo wa mke wangu, akinitukana pia.

Hakuna aliyeona kosa la mama mkwe wangu, bali kila mtu aliniona kama mimi ndiye mkosaji. Kabla sijajua, nilimuona mama mkwe akija usiku na mdogo wake. "Hana pa kukaa mume wangu hamtaki, na mume wake hawezi kukaa mle ndani. Hivyo, kama ni eda, atakuja kumalizia hapa!" aliniambia, wakati huo mke wangu bado hajarejea. Kesho yake mke wangu alirudi, hata hivyo hakuniomba msamaha, alinitukana sana na kunambia kuwa anatafuta chumba kuondoka.

Ni mwaka wa saba sasa, naishi hapa na mama mkwe wangu na mke wangu. Baba mkwe hakumsamehe mke wake na kasha oa mwanamke mwingine. Mimi, hata sikuombwa msamaha, lakini sikua na namna. Kila nikitaka kumuacha mke wangu nashindwa, sasa hivi anaishi naye na mama yake, wananisumbua sana.

Mke wangu anaweza kuondoka bila kuniaga hata wiki, na nikimuulizia kwa mama yake, ananitukana. Yaani ni shida tupu, natamani ningekuwa na nguvu kama za Baba mkwe kutoka katika hii ndoa, lakini siwezi kumuacha mke wangu. Nampenda sana, natamani angeuona upendo wangu.
FB_IMG_1708105357758.jpg
 
Hawa ndio wale wanaume wanaitwa Simp, pig man. Ukipata vimali kidogo tu, watakuua maisha yako si marefu.

Mwanaume mwenzio kakuona boya, baba mkwe anakushngaaa aina gan ya mwanaume ww, mkeo yeye mwenyewe anajua jinsi ulivyo zuzu.
 
Wakati baba mkwe anaandika talaka na wewe ulitakiwa uandike yako, we ni pimbi
 
Back
Top Bottom