Anataka awe nyumba ndogo yangu; nifanyeje?

Wapendwa habari za majukumu ya kulijenga taifa;
Nikiwa katika pitapita zangu miezi mitatu iliyopita; nikikutana na mwanadada mrembo; nikawa nimekaa naye meza moja. Katika kuongea ongea akanipa historia ya maisha yake. Kikubwa ni kwamba aliolewa lakini tabia ya mume wake kumpa kichapo mara kwa mara aliamua kuomba uamisho kazini na kuhama toka kwenye mji anapoishi mume wake.
Kwa kuwa tuliendelea kuwa na mawasiliano; siku moja akanikaribisha nyumbani kwake; nikakuta amejiandaa kisawasawa; mambo ya kikubwa yakaendelea, jioni nikatoka naye out; haikuishia hapo tukaendelea kama wapenzi. Majuzi ananambia eti anataka anizalie mtoto na anitambulishe hadi kwa ndugu zake.
Nashindwa kumpa ok kwa kuwa mi tayari nina mke; na mume wake bado anambembeleza warudiane. Yeye anadai awezi kurudiana na huyo mwanaume kwa sababu ni mkorofi na anamdunda mara kwa mara; mtoto wa watu ana makovu hadi namuonea huruma. Naomba ushauri wako we unayesoma hii habari.

Haya ndio mambo yanayotufanya wabongo tuzidi kuwa masikini.
 
Nnavyojua mimi, mtu haombi ushauri ukiwa na nyumba ndogo. Unatakiwa tu ujue ukiwa nayo kuna siku atakuomba mtoto kama hana na roho ya huruma ikikuingia utapata shida sana hata umkwepe vipi. We unafikiri sie hatutaki tule nje? Tunayaogopa haya mambo eti.
 
na unavyojifanyaga kumsifia mkeo! leo totoz kawa bora kuliko mkeo, we muoe tu huyo dada, tena umpangishie hukohuko nyakato ikibidi awe shost wa mkeo
Eh! we dada; mke wangu
namjali sana na anavutia kinomi; nikitaka kwenda kwenye mitoko rasmi
kama vile harusi ndo naenda na wife; nikitaka kwenda club kama vile
villa ndo naenda na huyo toto.
 
ungekuwa unampenda na kumheshimu wala usingewaza hbr ya nyumba ndogo, muoe kbs tena umhamishie hukohuko nyakato ikibidi awe shost wa mkeo
nampenda, namuheshimu ndo
maana mambo mengine nafanya tena kwa siri kubwa. ikitokea niko kwa
bi-mdogo; wife akapiga sm kwamba ananihitaji - naondoka haraka sana
nisijemkwaza mama watoto wangu.
 
Siyo wazo baya. Hivyo ndivyo alivyokuwa anafanya Kawawa. Alikuwa ana mke wake Sophia,halafu alikuwa na nyumba ndogo.
 
Wapendwa habari za majukumu ya kulijenga taifa;
Nikiwa katika pitapita zangu miezi mitatu iliyopita; nikikutana na mwanadada mrembo; nikawa nimekaa naye meza moja. Katika kuongea ongea akanipa historia ya maisha yake. Kikubwa ni kwamba aliolewa lakini tabia ya mume wake kumpa kichapo mara kwa mara aliamua kuomba uamisho kazini na kuhama toka kwenye mji anapoishi mume wake.
Kwa kuwa tuliendelea kuwa na mawasiliano; siku moja akanikaribisha nyumbani kwake; nikakuta amejiandaa kisawasawa; mambo ya kikubwa yakaendelea, jioni nikatoka naye out; haikuishia hapo tukaendelea kama wapenzi. Majuzi ananambia eti anataka anizalie mtoto na anitambulishe hadi kwa ndugu zake.
Nashindwa kumpa ok kwa kuwa mi tayari nina mke; na mume wake bado anambembeleza warudiane. Yeye anadai awezi kurudiana na huyo mwanaume kwa sababu ni mkorofi na anamdunda mara kwa mara; mtoto wa watu ana makovu hadi namuonea huruma. Naomba ushauri wako we unayesoma hii habari.

Bila shaka uliuza mechi....chonde chonde usipeleke ukimwi nyumbani!!!PAMBAF....
 
Siyo wazo baya. Hivyo ndivyo alivyokuwa anafanya Kawawa. Alikuwa ana mke wake Sophia,halafu alikuwa na nyumba ndogo.

Yaan Mzee A.Nyerere hizo ndo busara zako,yaan kwa sabab Kawawa aliwah fanya hivyo nae afanye? Watu weng sana hivo vit tunapenda lkn tunaogopa kuangamiza na kuharib mustakbari wa watoto na familia zetu. Yeye kama din yake inaruhusu amwambie mke wake akimkubalia amuoe kabisa awe na familia mbili.
 
mangi kama we unajijua pendapenda kwa nin ulikimbilia kuoa,hyo ni holy commitment na ukiisaliti utakufa
 
Kuna post humu inaitwa "Ukitaka kuwa na nyumba ndogo- the guide " nadhani itakusaidia . Ila moja ya ushauri ulikuwa kuwa ,nyumba ndogo ikipata mtoto haiwi ndogo tena ,kwa hiyo utakuwa na nyumba kubwa mbili ,na usipokuwa makini unaweza jikuta ukitafuta nyumba ndogo tena.

Hapo kwenye bold kuna ukweli .... ebu nitafakali kwanza.
 
Anza ukorofi, na kumdunda ili akukimbie au kubali kuzaa naye ili awe nyumba ndogo au msihi arudi kwa mumewe.

Mhaya na mangumi wapi na wapi? Mi mwili wangu ni wa kazi na mapenzi, bas
 
Nakufaham vilivyo Tutor B bora uachane tuu na hiyo nyumba ndogo yako tarajiwa maana nilivo na speed gavana 0 mdomoni, hapa nlipo nawashwa kwenda kumwambia mkeo, na amenipigia kesho twende wote kwenye kiche party. Sasa sijui ntaweza kukaa muda wote huo bila kumwambia???

Wallah! My wife huwa haendi kwenye sherehe za kiswahili kama hizo za kitchen party.
Hunifahamu;
Sikufahamu,
Inakuweje hunipakazie?????
 
uwezi kumuoa kwasababu yule alikua na m2 wake na wewe unaye mke!licha ya ivyo yule mpnz wake anataka kurudiana nae uoni kua utajutia baadaye baada ya ugomvi utakao tokea?Coz ndoa siyo siri ila mnaweza kujifcha mkiwa mnafanya mapenzi! SIKUSHAURI HATA KIDOGO!kumwoa

Sio kumuoa, ni kuzaa naye tu basi!
 
Kwa Usalama wako:- "ONYO la mwisho"
Taifa limechoka kuleya watoto wa zinaa, Idadi ya watanzania imefikia millioni 45. ikiwa kila mtanzania anafuata tamaa zake na kulala na wanawake na wazae watoto bila mpango... Basi hapatoshi hapa.

Hayo yote uliyo shauriwa na Wapendwa weka maanani, Kundi la Wanaume fulani linajulikana kwa kurukaruka na kwa kuzini kila wapatapo 'VICTIMS" ukweli kuwa madamu upo hai utaendelea kupendwa hiyo sii "big deal"... kifupi, yaani utaharibu maisha yako na maisha ya familiya yako kama walivyo kuonya wanaJF. Tabia na Uhusiano wako utaleta matokeo kadha za kijamii, Watoto haramu wengi,Vunja ndoa za wenzio, Maisha bila muelekeo,kukumbwa na madhara ya ngono, NK.
ushauri kuwa na MSIMAMO na ujirudi uishi na mama watoto wako mujenge TAIFA imara !!
Good luck na UBARIKIWE na familya yako halali.
 
ungekuwa unampenda na kumheshimu wala usingewaza hbr ya nyumba ndogo, muoe kbs tena umhamishie hukohuko nyakato ikibidi awe shost wa mkeo

Hapo kwenye red pamenishtua sana.... ningeweza ningefunga hii mada.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom