Una bahati sana, mwanamke anayekaa sana na wanaume huwa anawafahamu zaidi wanaume. Atajua mahitaji yako, furaha yako na hata kero zako kiurahisi. Binafsi na enjoy sana mtu wa namna hii.
Sioni sababu ndio akae nao, mimi kwetu tumezaliwa 10 na 9 wote ni wanaume wakike peke yangu na kwetu kulikua hakwishi wanaume rafiki wa kaka zangu lakini haikua sababu ya mie kukaanao na ukikaa baribu yao utaipata habari yako.
Nakubaliana na wewe jamaa ana bahati sana!
Hujiamini tu, kwani wanamme sio watu?
Kuna saa unajikuta uko mwanamke mmoja kati ya wanamme 30, so ashindwe ishi?
Kumegwa hata kama anakaa na masista atamegwa tu.
Si tatizo sana! Lakini kama hakuna jambo baya! Wanawake wa namna hiyo siku hizi ni wengi na ukijaribu kuwa uliza wana sababu za msingi za kufanya hivyo!
Ila kwa sababu ali kuahidi kuacha ni vizuri ukajaribu kuongea nae tena kuhusu ahadi yake.
Pia jaribu kupunguza wivu!
Wivu tu unakusumbua,
Una bahati sana, mwanamke anayekaa sana na wanaume huwa anawafahamu zaidi wanaume. Atajua mahitaji yako, furaha yako na hata kero zako kiurahisi. Binafsi na enjoy sana mtu wa namna hii.
mfanyie 'background check'; it is possible katika makuzi yake ametokea ku-interact zaidi na wavulana kuliko wasichana wenzake, which might not necessarily be a bad thing
ndugu yangu mtoa mada ngoja nikwambie kitu fulan, huyo binti atakuwa wala hajaathiriwa na makuzi ama malezi bali mazingira. yawezekana kabisa akawa ameshashuhudia kadhia za marafiki wa kike ambazo ni uchoyo, umbea, kijicho na wivu wa kishenzi pia kutetana. Binafsi mimi hapa mara kwa mara nimekuwa sipend kampani ya wadada kama ya wakaka na sababu kubwa nilizo ziona ni hizi hapa
- wakaka wakikupenda wanakupenda kiukweli, watakuonya watakusaidia na watashirikiana na wewe as their sister pasi hata kutaka maishu ya ngono. ni kampan ambayo utaipata at any time incase of anyproblem. hasa wakati wa matatizo makubwa kama misiba. hawa ni watu ambao watakufunga turubai,watafanya usafi,watachimba kaburi bilakinyongona tena watafanya kwa moyo sana ikiwa ni mshakaji wao.
- wakaka watakuthamini sana, na thamani yao huenda mbali kama vile atakapo kuwa anataka kuoa ama kwenda shule akushirikisha pasi kinyongo.
sasa kwa huyu binti just make sure kwamba wewe hakuibii muda wako ila kama that is during her time siyo mbaya. MCHUNGUZE KATIKA HAYA je ana haiba ya kike? yaani siyo mropokaji hasa wa matusi, siyo mpayukaji, akaapo hukaa kike yaani siyo swala la duka la mzungu li wazi. pia muangalie kama kwa kampani hiyo anashinddwa kumeet her female obligations.
Sasa gfsonwin unataka wakaka wa kukupenda wa kazi gani wakati kama ni mpenzi tayari unaye. Huoni kuwa hapo unampa wakati mgumu baba nanii???
Mfano mimi mume wangu siwezi ku mention mara mbili mbili jina la mwanaume mwingine bila kupigwa maswali...na wala sioni shida...wivu lazima jamani. Hata mimi kwa kweli sivumilii kusikia jina la dada fulani halikauki mdomoni kwa mume wangu. Kwa ufupi hatuna urafiki na jinsia nyingine for the sake of our love.
hawa ma dear huwa mara nyngi sana nawaita wadogo zangu ambao kimsingi mr huwajua siko nao kwa stail ile ya kwenda kukaa nao vijiwen hapana but they do visit home na huwa nawatuma na huwa wako free hata kuja kula hapa home kwangu. siwe kuwa na marafiki close sana wa kiume hapa atachukia manake kuna siku niliwah kumsifia rafiki yake alikasirika sana so i learnt to be on his side.
wajua wanaume wana wivu sana kuliko hata sisi akina mama na pia wako sefish sana kuliko sisi manake ni rahisi sana kwa mwanaume kuona kama mtu baki anakaufurahia na kukaufaidi kuliko yeye jambo ambalo si kweli.
The Boss, binti anayetokea BK analelewa kutambua kuwa ni mwiko kukaa na wanaume hata kama ni kaka zake. Lol. Mwanamke analelewa kuwa na tabia za kike...siyo kuweka mguu juu ya meza. Sitanii mama yetu alikuwa mkali sana kwa hilo...ingawa baada ya kukua ndio nikajua ni mfumo dume...ila imenifanya niwe na tabia za kike ambazo sioni kama ni mbaya kwani sijawahi kumkwaza nimpendaye.
Unaweza kucheka lakini mimi mfano siwezi kupiga mluzi kwani toka nikiwa mdogo niliambiwa ni mwiko...ingawa nimezaliwa na kukulia Dar.
Sina watoto wa kike ila ningekuwa nao nadhani ningewalea kama nilivyolelewa mimi, hakuna kumanua manua mtoto wa kike unajikusanya wakati wa kukaa...na mengi mengineyo.
Nadhani hapa inategemea..
Kwa sisi wanaume inaletaga maswali pale mkeo au gf anapokuwa anatolea mifano ya kusifia kitu kwa kutumia cases za wanaume wengine hata kama ni marafikizako..