Anapenda kujichanganya na wanaume.... Ushauri plz!

Habari zenu jamani?
Mimi nina mpenzi wangu ambaye nampenda sana na yeye ananipenda sana (kwa mujibu wa mdomo wake)
Sasa tatizo ni kwamba anapenda sana kukaa na kupiga story na wanaume.
Niliwahi kumwambia kuwa sipendi tabia hiyo na akaniahidi ataiacha.
Sasa juzi nilimkuta kwa macho yangu akiwa amekaa na wanaume watano huku mtoto wa kike akiwa peke yake wakipiga story. Hivi jamani mi nimuelewaje mtu huyu? Kweli ni sawa kwa mtoto wa kike kupenda kujichanganya na wanaume kiasi hiko. Hebu nishaurini maana hapa nilipo nafikiria kumuacha japo ameniahidi hatorudia tena.


Sasa wewe siyo mwanaume? unamtakaje asijichanganye na wanaume wakati anajichanganya na wewe ukiwa mwanaume. au unamaanisha nini unaposema kujichanganya na wanaume?. kuna kitu umekificha, hebu kuweke wazi nikusaidie
 
Kama hilo ni kosa na sababu ya kuachwa kwenye mahusiano naona na mimi nilitanikumba!!!! Tangia ninasoma nimekuwa na kampani ya wavulana/wanaume wengi kuliko wanawake/mabinti. Nimefanyakazi katika mzingira ya wanaume zaidiiiiiiiiiiiiiiiiii

Na mpaka sasa nafanya kazi ofisi ambayo wanaume ni wengi kuliko wanawake na kwa bahati nzuri mi mwanamke peke angu......Life langu lipo happy manake hakuna shosti wakushindana naye mambo....navaa nikipendacho kwa mapenzi yangu....Niko nilivyo kwa matakwa yangu mimi, sishindani na mtu wala nini.

Rafiki yangu wa kike ni ndugu yangu mmoja hivi yani huyo ndo wakupiga naye stori za kike kike.....hakuna Umbeya wala nini......maisha yanakwenda safi sana ukiwa na marafiki wa kiume. Wanaongea ukweli kuhusu wao wenyewe....wanakupa mbinu za kujua life linavyokwenda. Ahiiiii we ukitaka uwe na maisha safi bahatika kuwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wa kike.

Safi sana LD, upo shosti wangu? lol
 
  • Thanks
Reactions: LD
Sioni sababu ndio akae nao, mimi kwetu tumezaliwa 10 na 9 wote ni wanaume wakike peke yangu na kwetu kulikua hakwishi wanaume rafiki wa kaka zangu lakini haikua sababu ya mie kukaanao na ukikaa baribu yao utaipata habari yako.

Hapo ni sawa kabisa,kwa hali ya kawaida mtotoo wa kike muda wote upo na wanaume umekaa kijiweni unapiga stori!!!! yaani hapana,kunaki2 hakipo sawa.Ni tabia mbaya
 
Mhhhhhhhh!!!! mimi mwenyewe rafiki zangu wakubwa wanaume. Sidhani kama ni tatizo. Ila watu wanaokuzunguka mara nyingi huwa wanakuchukulia kama mhuni. Ila kwa wakati mwingine inaweza isiwe hivyo binafsi nimesoma shule, chuo na rafiki zangu wakubwa walikuwaga wanaume lakini hakuna hata mmoja aliwahi kunimega.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Inategemea kakangu, kujichanganya na wanaume si kwamba basi yeye ni mhuni, watu wengine wameumbwa hivyo tu, mimi mwenyewe asilimia kubwa ya marafiki zanguni wanaume na si kwamba natoka nao kimapenzi ni kamapani tu,so relax
 
Back
Top Bottom