Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,643
- 1,786
mimi kuna mjinga mjinga moja wa temeke bakery iliyopo karibu na libya street? nilikwenda chukua keki ya birthday ya mtoto, basi naye akaja moto moto nitoe gari, basi zilipanda zile hasira za kimasai nilimbonda mbele ya staff wake halafu nikamwambia akalete hao mabwana zake anaofikiria wata mtetea, washenzi saana hawa watu, na ni sisi wenyewe tunawaachia wanatutia vodole machoni, kutokana na kuwa na viongozi wabovu wabofu
Mimi kuna mzungu mmoja alimleta mbwa wake aje kunya kwenye ka kampaundi kangu. Halafu mi mtu mwenyewe safari kitambo, nishabaguliwa sana na wazungu kwao siwafagilii hata kidogo, na najua kwao mtu hatembezi mbwa bila kuwa na kifuko mkononi ili akichafua mazingira unaokota njee la mbwa wako. Basi hasira zilinipanda kuzidi sniper, nikamfata yule mzungu nikamwambia yani unamtoa mbwa wako ndani kwako unamleta aje kuachia njee kwenye eneo langu? Okota mavi yenu sasa hivi kabla sijashuti hicho kijibwa manyoya, e bwana mzungu akajua kweli nimebeba kubwa, alitoka nduki huku anatukana nilimwonea huruma...na njia akabadili
Foreigners wana dharau sana, na ni sisi ndio tunawaendekeza.