Baba na Watoto 3 wateketea kwa Moto Mkoani Morogoro

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Baba aitwaye Amani Malekela Madumba na watoto wake watatu wa kiume wamefariki dunia kwa kuteketea na moto baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuwaka moto katika Kijiji cha Malolo B, Kata ya Malolo, Tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

IMG_7054.jpeg

Mwenyekiti wa Kijiji cha Malolo B, Sufiani Ramadhani Ndagama, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia Mei 5, 2023.

UPDATE;
Imeelezwa Mzee Amani Madumba aliyekuwa akiishi Kata ya Ruaha Mbuyuni wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro aliyefariki dunia yeye pamoja na watoto wake watatu usiku wa kuamkia leo Mei 5, kwa kuteketea kwa moto, kwamba yeye ndiye aliyeichoma nyumba hiyo kisa ugumu wa maisha.

Ndugu wa marehemu aitwaye Rajab Madumba, amesema ndugu yao huyo wakati wa uhai wake alikuwa akilalamika kwamba endapo yeye akifariki basi watoto wake watabaki wakiteseka na pengine ndiyo sababu ya kuamua kuiteketeza familia yake hiyo.

Chanzo: EATV
 
Baba aitwaye Amani Malekela Madumba na watoto wake watatu wa kiume wamefariki dunia kwa kuteketea na moto baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuwaka moto katika Kijiji cha Malolo B, Kata ya Malolo, Tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

View attachment 2610674

Mwenyekiti wa Kijiji cha Malolo B, Sufiani Ramadhani Ndagama, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia Mei 5, 2023.

Chanzo: EATV
Hao watoto hawakuwa na mama!!?

WAPUMZIKE KWA AMANI.
 
Hii inaumiza sana wakati serkali ikilifanya sikio zito kuhusu ugumu wa maisha hasa kupanda kwa bei ya vyakula leo mkazi wa kilosa amejichoma moto yeye na familia yake hadi kufa akidaiwa ugumu wa maisha ndio tatizo

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha usiku wa kuamkia leo

USSR
Screenshot_20230505-135357.jpg
FB_IMG_1683284048870.jpg
FB_IMG_1683284059340.jpg
 
Nasikia wanasema 'Ugumu wa Maisha ni kipimo cha Akili', hii ndo akili yenyewe ama!

Aheri angejiua yeye na kuwaacha hao watoto jamani.
Haya ni mambo ya kitaam kama huna taaluma ya saikolojia huwezi kuelewa kwann suicide case haziishi wala kupungua.
 
Sio kila kitu kubebesha serikali, yaani njaa ndo uue wanao? babu yake yeye alikuwa kama bakhresa? dunia yetu hii hata tuwe na serikali ya namna gani maisha lazima yapande na kushuka hakuna namna nyingine.

Amedhulumu uhai wa watoto wadogo wakati yeye ameshaishi zaidi ya nusu karne ubinafsi wa hali ya juu, kama maisha magumu na dawa ndo hii mbona wewe USSR haujiui?.
 
Kwa Nini wamesema kajichoma?Nani aliona wakati anajichoma?Kuna mtu alimuaga kwamba naenda kujichoma Sasa?mbona hakumsaidia...na je kwani haiwezi kuwa ajali Kama zilivyo ajali zingine?na what if kachomwa na mtu mwingine?
Mambo yasirahisishwe hivi jamani,vyombo vya dola vifanye uchunguzi kabla ya kutoa taarifa za mwisho
 
Hii inaumiza sana wakati serkali ikilifanya sikio zito kuhusu ugumu wa maisha hasa kupanda kwa bei ya vyakula leo mkazi wa kilosa amejichoma moto yeye na familia yake hadi kufa akidaiwa ugumu wa maisha ndio tatizo

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha usiku wa kuamkia leo

USSR
View attachment 2610862View attachment 2610863View attachment 2610864
Kwa mtu anayeshiba na kusaza chakula kila siku, kamwe hawezi kuelewa hali halisi iliyoko mtaani.
 
Back
Top Bottom