Mkuu wa chuo
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 7,608
- 5,269
jamaa gamba lake inaonekana ni gumu sana kuvulika.
Jee kuna sababu yoyote ya maana kwa kutumia huduma ya mtu halafu usimlipe?
Kwa maelezo yako ni kama unataka kutuambia kwamba Chenge anajua sheria sana siyo?Inawezekana anaijua sheria lakini kujua kwake sheria hakujaisaidia hii nchi.Serikali iliingia kwenye mikataba mibovu ya madini Chenge akiwa mwanasheria mkuu je wwakati huo alikua haijui hiyo sheria?au aliijua ila alikua ana masilahi binafsi?na kama niko sahihi basi hata sasa inawezekana ana masilahi binafsi kwenye hili suala la Dowans.Hoja si kujua sheria tu,na hiyo sheria unaiyumia vipi kwa masilahi ya Taifa!Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?
Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?
Hawa jamaa hawana huruma kwakweli.
Kiongozi umeongea point sana, haina maana kuwasamehe hawa jamaa wa migodi kodi kwenye mafuta, yaani Madini wanachimba kwa manufaa ya nchi zao na familia zao na vizazi vyao halafu sisi tunawasamehe Kodi ambayo ingechangia kuboresha maisha ya wananchi wetu,
Hivi yupi bora! Mwananchi au mwekezaji? sasa kwa nini unaweka kodi kwenye mafuta anayotumia mwananchi halafu unamsamehe mwizi wa raslimali za nchi yetu? jamani mtanzania wa leo analipa kodi kibao na nzito na hii ni kwa ubinafsi wa viongozi wa ccm.
ifikie wakati watanzania tuache unafiki tuuone ukweli huu usani wa kuchezeana na huku maisha yanakwenda, fanya mabadiliko sasa na usingoje kesho maana wewe leo una lets say 30 or 50 or 60 years miaka 5 ijayo utakuwa umesogelea kaburi na huu usani utaendelea ni lini utaishi katika nchi nzuri uliyopewa na Mungu wako! hawa jamaa wachache wanaishi maisha na wanataengeneza maisha ya jamii zao, watoto wao wajukuu na hata vitukuu, je sisi wabongo wa kawaida hatuhitaji kuwacha watoto wetu wakiwa na maisha ya uhakika? angali watoto wote wa Vigogo wanasomea hapa kwetu? unafikiri ni kwa nini wapo USA, UK na kwingineko ni kwa sababu ya wizi na dhuluma ya baba zao, sisemi kwamba ni wote! wapo waliotafuta wao wenyewe lakini wengi wao ni ufisadi wa wazazi wao ndio umewafikisha hapo na ndio huwa wanawacheka wananchi wasumbukao kitaa.
Ndugu zangu tufumbuke macho, kuna Mchungaji mmoja aliwahi kusema saa ya ukombozi ni sasa na walio wengi walimponda lakini kadri siku zinavyozidi ushuhuda wake unazidi kujizihirisha.
Acha unafiki mtanzania na sasa uchukue hatua. Asilimia 60 ya wabunge wa ccm hawapaswi kurudi bungeni 2015 hamasisha watu wawabwage na ndipo tutapata ukombozi, jamani kwa kila mtu anayependa mabadiliko ya kweli hamasisha katika wilaya yako unakotoka, ili next Bunge Chadema iwe na wabunge walau kuanzia 55% na ndipo utaona nchi itakavyobadilika.
Mbunge wa Bariadi pamoja na tuhuma nzito zinazo onyesha negative atitude kwa WATZ kama vile tuhuma dhidi ya rada, kumiliki mabilion ya fedha nje ya nchi, kutia mkono wa kumuondoa spika SITTA aliye pendwa na WATZ wengi kuwa spika wa Bunge Leo napata habari mbaya kwetu kuwa CHENGE amepeleka ushauri mzito wa kisheria ili DOWANS walipwe sh. 94 bil. (source GAZETI LA NIPASHE) CHENGE kama kuna kosa WATZ wamekufanyia basi wasamehe bure !!!! Mbona wao awnakupenda wamekupa ubunge (kama hukuchakachua) kuonyesha wanakupenda tusamehe tu hata kama una mgawo DOWANS
U wapi uzalendo wa viongozi kwa Taifa lao.,bila hata aibu unaisaidia kampuni 'inayoidai' serikali unayoitumikia ili iweje?.Nilitegemea angesaidia serikali na nchi yake isiingie au jinsi ya kujitoa katika katika migogoro ya kisheria...
Wewe una laana kali sana!Jee kuna sababu yoyote ya maana kwa kutumia huduma ya mtu halafu usimlipe?
Bongolala, wakati nasubiri kulisoma hilo Nipashe, ningependa kusisitiza mahitaji ya kisheria na mahitaji halisi ni vitu viwili tofauti. Mahitaji ya kisheria ni laz`ima yatekelezwe no matter what, hata kama sio mahitaji halisi.
Tozo la Dowans lililotolewa na ICC ni hitaji la kisheria, kwa mujibu wa mkataba husika, uamuzi wa ICC ni uamuzi wa mwisho, haupingiwi na mahakama yoyote labda kufanyiwa mapitio na ICC yenyewe, hivyo kitendo cha kuusajili mahakama za nchini, ni kwa lengo la kuusajili uamuzi ule kwa utekelezaji tuu.
Siungi mkono tozo hiyo ya ICC kwasababu sio tozo halali, ila kisheria, maadamu wanasheria vichwa maji wetu waliukubali ule mkataba, na hivyo ndivyo mkataba unavyosema, then tozo hiyo imehalalishwa na mkataba mbovu ule, hivyo toso ile ni halali kisheria.
Nawaombeni wana jf na wananchi wote wa Tanzania, lazima tuukubali ukweli mchungu kwa kumeza kidonge kichungu cha tozo hii, tutatake tusitake, lazima tutalipa tuu, hatuna popote pa kutokea unless Tanzania kama nchi, tujitoe ICC na kuwafukuzia mbali hawa wanyonyaji wote wanaojiita wawekezaji wa kwendo makao n a mitaji yao, wakatumie fedha zao kutengeneza madini yao na sisi watuachie almasi zetu, Wasukuma tuzichezee bao, na dhahabu zetu tuziache humo humo ardhini, tubaki na umasikini wetu huku tumekalia malia zetu, kuliko kuwaruhusu wazipore kubadilishana na pipi huku wakituacha na umasini wetu palepale.
Mbunge wa Bariadi pamoja na tuhuma nzito zinazo onyesha negative atitude kwa WATZ kama vile tuhuma dhidi ya rada, kumiliki mabilion ya fedha nje ya nchi, kutia mkono wa kumuondoa spika SITTA aliye pendwa na WATZ wengi kuwa spika wa Bunge Leo napata habari mbaya kwetu kuwa CHENGE amepeleka ushauri mzito wa kisheria ili DOWANS walipwe sh. 94 bil. (source GAZETI LA NIPASHE) CHENGE kama kuna kosa WATZ wamekufanyia basi wasamehe bure !!!! Mbona wao awnakupenda wamekupa ubunge (kama hukuchakachua) kuonyesha wanakupenda tusamehe tu hata kama una mgawo DOWANS
Mkuu kumbe ulikuwa haulijui hilo? wenzio tulishamshitukia kitaaaamboAwali nilidhani upo humu kutetea CCM na mafisadi kumbe I was wrong. Wewe upo si kwa ajili ya CCM ila kwa ajili ya JK na udini.
Hilo nimelinusa. Hata hivyo wenye fikra pevu wanakudharau.
Uamuzi aliouchukua Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Mzee wa vijisenti/'Mr. Clean) wa kuongeza nguvu Dowans kwa kutoa ushauri wa kisheria ili ilipwe bilioni 94 na Tanesco=Tanzania, unadhihirisha jinsi alivyoumizwa na uamuzi wa chama chake CCM wa kuvuliwa gamba na sasa ameamua kuwasaidia Dowans ili Tanzania ilipe mabilioni ya fedha. Ikumbukwe huyu jamaa alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na amesaini mikataba mingi na huenda alishirikishwa kwa kuomba ushauri katika suala la Dowans lakini leo ameamua kuvuaa miwani ya mbao na kuitetea.
Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?
Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?
Mbunge wa Bariadi pamoja na tuhuma nzito zinazo onyesha negative atitude kwa WATZ kama vile tuhuma dhidi ya rada, kumiliki mabilion ya fedha nje ya nchi, kutia mkono wa kumuondoa spika SITTA aliye pendwa na WATZ wengi kuwa spika wa Bunge Leo napata habari mbaya kwetu kuwa CHENGE amepeleka ushauri mzito wa kisheria ili DOWANS walipwe sh. 94 bil. (source GAZETI LA NIPASHE) CHENGE kama kuna kosa WATZ wamekufanyia basi wasamehe bure !!!! Mbona wao awnakupenda wamekupa ubunge (kama hukuchakachua) kuonyesha wanakupenda tusamehe tu hata kama una mgawo DOWANS
ENYI WANA WA TAMAA! Wekeni mbali vazi la majivuno na mjivue vazi la ufedhuli.ewe asili halisi ya shauku! Weka mbali tama na tafuteni kuridhika kwa maana mwenye tamaa daima amenyimwa, na mwenye kuridhika daima amependwa na kusifiwa na mngu