Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi,

Mjinga na Mpumba..
Leo naomba kuianza makala ya leo kwa angalizo kuhusu neno mjinga na mpumba. Mtu kuitwa mjinga ni mtu asiyejua, mjinga akiishafundishwa akajua, anaerevuka ujinga unamtoka anakuwa sio mjinga tena bali mwerevu! Mjinga aliyefundishwa na bado akabaki na ujinga wake, huyo sasa sio mjinga tena bali ni mpumba. Hivyo mpumba.. ni mjinga asiyefundishika!. Mwalimu wangu wa somo la wajinga na wapumba.. ni Mwalimu Nyerere
View: https://youtu.be/BeCC28fFQb4
Tulipota uhuru ujinga ni moja wa maadui wakubwa watatu wa taifa letu. Leo miaka 60 ya uhuru, adui ujinga bado anatutesa ila sasa ame graduate na kuwa adui Upumba..!.

Hiki ndicho kinachotokea kwenye baadhi ya issues za taifa letu, na mimi kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa, kujitahidi kuwaondolea ujinga Watanzania wenzetu.

Makala ya leo ni a Cry for my beloved country!, kwa jinsi ujinga wetu au sijui niuite ni upumba.. wetu unavyozidi kutu cost, leo tumelipa tena tuzo nyingine ya US $ 30 milioni!, ambazo ni sawa na tumepigwa tena Billioni 75 kwa ujinga tuu au kwa upumba.. wetu! tuu. Nimesema tumepigwa tena kwasababu hii ni mara ya tatu tunalipishwa publically mabilioni kama haya!. Hayo yanayolipwa kwa siri we can't tell mpaka ripoti ya CAG ya mwakani. Mabilioni ya kwanza ni Bilioni 300 za tuzo ya Simbion!, zikaja Bilioni 260 za tuzo ya Indiana, Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini? na sasa ndio hizi za leo!.

Swali ni tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?!. Hivi sisi Watanzania wote ni wajinga hivi au ni wapumba.. hivi? Au kuna baadhi yetu ndio wajinga na wapumbavu, wanafanya mambo ya kijinga na kipumba, kwa vile ni Tanzania inatajwa kama Tanzania nchi, under the principal of a collective responsibility hivyo wote tunaonekana ni wajinga na wapumba..!.

Kwanza unisamehe kutumia neno kwa "ujinga wetu" kumaanisha sisi Watanzania ni ama ni wajinga, ama sio wajinga tuu bali pia ni wapumba.. under a collective responsibility, kama serikali yetu imefanya jambo la kijinga, ikaambiwa huo ni ujinga, ikaendelea, Bunge letu likaitunga sheria ya kijinga likaambiwa hiyo ni sheria ya kijinga, Bunge letu likaendelea, na wakajitokeza Wazalendo wakaiomba Mahakama yetu isimamishe ujinga huu, Mahakama ikasikiliza, ikakubali kweli ni ujinga, ila kwavile ujinga huu umefanywa na serikali yetu na Bunge letu, then mhimili wa Mahakama unaiheshimu sana serikali, na unaliheshimu sana Bunge, hivyo ikabariki ujinga huo, huku wananchi kwa umoja wetu tunashangilia!, huu sasa bado ni ujinga au ni upumba.., tukijiita wote ni wajinga na wapumba ni kujionea?

Ukimkuta mtu anakata mti, huku amekalia tawi analolikata, ukamwambia simamisha kwanza kukata maana hapo ulipokaa, mti ukikatika na wewe utaanguka!, kukata tawi la mti ulililokalia ni ujinga, mtu huyo anaendelea tuu kukata huku akikubeza, hayakuhusu!

Baada ya muda mfupi unasikia kishindo cha kuanguka huku unasikia mayowe ya yalaa! yalaa! nakufa!, naomba mnisaidie!. Unageuka na kumuona ni yule jamaa ameanguka anagugumia maumivu!.

Japo utamsaidia kibinaadamu kwa kumpatia huduma ya kwanza, ila pia ni lazima utamsimanga kuwa yeye sio tuu ni mjinga bali pia ni mpumba...kwasababu alielezwa ujinga anaoufanya hakusikia!, "asiyesikia la Mkuu, .... "

Jana nimeianza siku kwa taarifa hii

20231017_133627.jpg


Tanzania tumelipa Dola Milioni 30 za Marekani kumaliza hili shauri nje ya Mahakama ya usuluhishi lililotokana na ujinga tuu wa wanasheria wetu, kutoishauri vizuri serikali yetu, na rais wetu, kulikopelekea Bunge letu Tukufu kutunga sheria batili nyingine inayokwenda kinyume cha sheria za haki za Jumuiya ya Madola, kwa serikali yetu kutunga sheria ya rasilimali za taifa yenye vipengele batili vinavyokwenda kutumika kwa retrospective ambapo ni kinyume cha haki!.

Kabla sheria hiyo haijapitishwa na Bunge letu, niliandika kuuliza Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? no one paid any attention!.

Bunge letu Tukufu, likaipitisha na rais akaisaini ikawa sheria na kuanza kutumika. Tukafuta kibabe baadhi ya leseni za sheria ya zamani na kulazimisha matumizi ya sheria mpya, hivyo kuivunja kibabe mikataba baadhi ya mikataba iliyopo.

Sheria mpya ilikataza mashauri yoyote ya uwekezaji kusikilizwa nje ya nchi, na kusema kesi zote zitaendeshwa nchini kwa sheria za Tanzania!. Tukaieleza serikali yetu kuwa hili jambo la kutunga retroactive law ni repressive, na kinyume cha sheria, na tukaeza kilichotokea kwenye uhujumu uchumi enzi za Sokoine, lakini waheshimiwa wabunge wetu, ni pamba masikioni!. Sasa kama watu tuliwashauri kuwa sheria hii ina vipengele batili vya ujinga, na wakaendelea, sasa tunapokuja kulipishwa mihela kwa ujinga wao, tuwaite ni wajinga au ni wapumba.. kabisa?.

Wale wawekezaji wasiokubaliana nasi wakiwemo hawa jamaa, wakatushitaki huko nje wakidai dola US $ million 100. Yule shujaa wetu aligoma kuwa hatulipi!.

Kesi kama hizi ambazo tuligoma kulipa ziko nyingi ila nyingine kama tuzo ya Dowans, tuliipa kimya kimya kwa siri, ila baada ya Mama kuingia, tukaanza kulipa kimya kimya kisiri siri! huku mambo hadharani!.

Kwanza tukalipa kwa siri tozo ya Simbion na kununua kwa siri mitambo ya Richmond/Dowans/Simbion sasa ni mali yetu!.

Kila dege zetu zinaposhikiliwa kwa kukazia hukumu fulani, huwa tunalipa kisiri siri, ndege zinaruhusiwa maisha yaendelee.

Hata malipo haya, wasinge yatangaza wenyewe, wala tusingejua na mpaka sasa bado hakuna taarifa yoyote rasmi kuhusu hili kutoka serikali yetu!.

Namuomba Mkurugenzi Mpya wa Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi aonyeshe utofauti kwa serikali yetu kuwa proactive kwenye utoaji wa habari badala ya kuwa reactive. Serikali yetu ingekuwa proactive kwenye ile IGA ya DPW, wala tusingefika kote kule tulikofika.

Kwa kuanzia, serikali iweke wazi, tangu kupitishwa kwa sheria mpya ya madini na rasilimali za taifa, ni wawekezaji wangapi walikubali ku subscriber kwa sheria mpya, taarifa iliyopo zaidi ya Barrick na Twiga wake, sikumbuki kusikia mgodi mwingine wowote kuzungumzia mgawanyo wa 50/50.

Jee kuna mashauri mangapi Mahakama zipi ili yote yafanyiwe out of court settlement, Tanzania tuwe clean.

Kwa vile sheria zetu zinazuia mashauri kusikilizwa nje ya nchi, kwanini haya mashauri bado yanapelekwa nje ya nchi?.

Mkiisha pitisha sheria, haijalishi sheria hizo ni mbovu kiasi gani, lazima ziheshimiwe na zitekelezwe, mfano sheria ya uchaguzi ni moja ya sheria mbovu, inayokwenda kinyume cha katiba, ila ubatili huo umechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, hivyo kuuhalalisha ubatili huo, lakini tunaitekeza mpaka kesho kwa vile ipo.

Kwavile sheria ya rasilimali za taifa ipo, na inakataza kuingia mikataba kwa sheria nyingine yoyote isipokuwa sheria za Tanzania, serikali yetu iliwezaje kuisaini IGA ya DPW na Bandari yenye vipengele batili kinyume cha sheria zetu na Bunge letu Tukufu kuridhia IGA hiyo hivyo hivyo ilivyo pamoja na ubatili wake?.

A Way Forward
  1. Japo serikali ina wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, kwenye issues zote za katiba, sheria na haki, especially on rasilimali za taifa, isiwategemee sana hawa jamaa pekee, always seek a second opinion from TLS members, kuna vichwa vya ukweli mule!.
  2. Sababu za kutowategemea hawa pekee, ni kwasababu ni wanasheria hawa ndio waliopitisha madudu yote haya yaayotugharimu sasa!. Niliwahi kuuliza Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  3. Pia ni manguli hawa wabobezi na wabobevu wa serikali na Bunge ndio walioruhusu Ajabu Hii ya Haki Iliyotolewa na Ibara Moja ya Katiba, Kuporwa na Ibara Nyingine, Ilifanyika Vipi Huku Tuna Washeria Manguli, Wabobezi na Wabobevu?
  4. Wanasheria hawa wa serikali, sio tuu hawajui sheria, bali hata katiba, hawaijui kikamilifu! Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?
  5. From now kuwe na maximum transparency kwenye issues zote za rasilimali za taifa, hakuna haja ya the confidentially clause kwenye mikataba ya kimataifa na ya rasilimali za taifa.
  6. Serikali imetukosea sana kutunga miswada ya sheria za ajabu zinazokuja kutugharimu, tusiishie kulipa tuu mabilioni ya fedha, waliotufikisha hapa nao pia washughulikiwe!.
  7. Bunge letu liache kujipendekeza kwa serikali, likiletewa miswada ya ajabu ajabu, liwe na uwezo wa kuigomea serikali na kuwarudishia madudu yao kuepuka wote kuonekana wajinga!.
  8. Itafutwe namna ya kuliwajibisha Bunge letu Tukufu lililotunga sheria batili na za ajabu, na kutufanya Watanzania wote tuonekane wajinga na wapumba...
  9. Bunge la 2025, turuhusu wagombea huru, ili watu independent wa maana wa kulisaidia taifa, wajitokeze
  10. Mhimili wa Mahakama, uachane na nidhamu ya kikondoo kuiheshimu serikali na Bunge, Checks and balance zifanywe kikamilifu.
Conclusion,
This is my cry for my beloved country Tanzania!, baada ya leo kulipa tena US $ 30 milioni!, ambazo ni sawa na Billioni 75 kwa ujinga tuu au kwa upumba.. wetu! tuu, tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?!.

Hivi sisi Watanzania wote ni wajinga na wapumba.. hivi?, au kuna baadhi yetu ndio wajinga na wapumba.. , wanafanya mambo ya kijinga na kipumba.., na kupelekea wote tunaonekana ni wajinga na wapumba.., tutaendelea kufanywa hivi mpaka lini?.

Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
 
Nashukuru leo umeandika kama Paschal Mayalla, kimsingi hizi ni dili za Mkwere, hii kesi haikuwepo imefufuliwa mwezi wa 7 2023 September 2023 malipo yakafanyika sijui kwa budget ipi? Ukisikia wateule wanamsifia sn maza kupita MUNGU wao sababu ni dili kama hizi, mara awe Mama wa Taifa sijui Dkt huku nchi ipo gizani, hakuna maji petrol shida, majibu ni haya. Tuacheni uchawa tusimame na nchi yetu
 
Nani alaumiwe mkuu kama sio ccm. Mmoja apokee wawekezaji mwingine aje wafukuza. Unategemea nini?
Hii kesi imefufuliwa na wanaume wapige pesa then maza wa mwambie anaupiga mwingi na majina mazuri mazuri huku wanapiga pesa za umma, umewahi kuona wapi kesi kubwa kama hii inaendeshwa kwa miezi 2? kuna kesi ya ubunge ambayo haina maslahi kwao leo ina miaka 2 haijulikani hata mwisho wake.
 
Wanabodi,
Leo naomba kuianza makala ya leo kwa angalizo kuhusu neno mjinga na mpumba... Mtu kuitwa mjinga ni mtu asiyejua, mjinga akiishafundishwa akajua, anaerevuka ujinga unamtoka anakuwa sio mjinga tena bali mwerevu!. Mjinga
Mnajaza bungeni makada wa chama, wanasheria wa Tz wote wameja wale wenye strong connection na vigogo wa CCM, kweli utegemee ufanisi katika sekita yoyote.

Hizo $30m bado nyingi zitalipwa kosa kubwa ni kuruhusu mtu kama JPM kua Raisi wa nchi hi bado wataendelea kulipia hayo makosa.
 
Wanabodi,
Leo naomba kuianza makala ya leo kwa angalizo kuhusu neno mjinga na mpumba... Mtu kuitwa mjinga ni mtu asiyejua, mjinga akiishafundishwa akajua, anaerevuka ujinga unamtoka anakuwa sio mjinga tena bali mwerevu!. Mjinga aliyefundishwa na bado akabaki na ujinga wake, huyo sasa sio mjinga tena bali ni mpumba..!. Hivyo mpumba.. ni mjinga asiyefundishika!.

Hik
Tafakari upya msimamo wako wa kupigia chapuo CCM

Serikali ya CCM imetufikisha hapo na hatuna la kuifanya. Tukiwa na serikali inayowabikika kwa wananchi inakuwa na guts za kutofanya makosa ya kuigharimu nchi.

Hatukuanza leo kulipishwa hayo mabilion. So long as tunaendelea na CCM haitakuwa mwisho wa kulipishwa hayo mahela.

Leo tunamlaumu JPM kwa kudhani ndo tumeshaliadress tatizo. JPM ni zao la CCM na hata huyu wa sasa anayetuingiza mkenge maradufu naye ni zao la chama chetu kilichopoteza dira.

Inauma, lakini tuanze kuuishi ukweli
 
Nashukuru leo umeandika kama Paschal Mayalla, kimsingi hizi ni dili za Mkwere, hii kesi haikuwepo imefufuliwa mwezi wa 7 2023 September 2023 malipo yakafanyika sijui kwa budget ipi? Ukisikia wateule wanamsifia sn maza kupita MUNGU wao sababu ni dili kama hizi, mara awe Mama wa Taifa sijui Dkt huku nchi ipo gizani, hakuna maji petrol shida, majibu ni haya. Tuacheni uchawa tusimame na nchi yetu
Tuwaulize wanazi Lucas mwashambwa ChoiceVariable haya mahela yanatolewa kwenye vote ipi ya bajeti.

Maana wao wanaijua seeikali kuliko hata waliomo ndani ya serikali
 
Back
Top Bottom