Serikali imepandisha nauli kisha Daladala za Kawe - Buza zinakatisha ruti, hii inaumiza sana

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Kuna tabia ambayo imekuwepo kwa muda, awali ilianza kama kitu kidogo kwa kufanywa na watu wachache lakini sasa hivi inazidi kuwa kama ndivyo uhalisia.

Daladala za kutoka Kawe kwenda Buza (Dar es Salaam) hasa nyakati za jioni zimekuwa na kawaida ya kutokamilisha ‘ruti’, zinaishia Buguruni kisha baada ya hapo zinageuza kurejea Kawe au zinasogea hadi cha Chama kilichopo maeneo hayo na kuanza kubeba abiria upya kuelekea Buza au maeneo mengine.

Hiki wanachokifanya si sawa kwa kuwa kinatuumiza sisi Wananchi hasa wa hali ya chini ambao maisha yetu yanategemea usafiri wa Daladala.

Maumivu zaidi ni kuwa hivi karibuni Serikali ilitangaza kuongeza bei ya nauli, so nauli zimeongezwa kisha daladala zinaamua kutoza mara mbili nauli, hapo maumivu yake ni makali zaidi ya noma.

Mamlaka za usafiri wa ardhini ziangalie hili suala, tunaumia kwa sana.
20240214_183523.jpg

Hili ni moja ya Daladala ambayo ilikatisha ruti nami nikiwa ndani ya basi hilo nikalazimika kuanza kutafuta usafiri mwingine.
 
Kama Latra wameshindwa au manpower yao haitoshi 'site' wa-delegate hii kazi kwa traffic maana hata wakipigiwa simu hawana watu barabarani.. Inatakiwa mtu akitoa taarifa unamsubiri daladala linapoishia, hata faini inaonekana ni haki kwa mhusika. Sio taarifa huku haijulikani kama hatua zinachukuliwa
 
Uwe unawahi kurud nyumbn ..sincerely km mchn wanakkatisha alafu si human wanatangaza kabisa kabla hujapanda
Wanafanya hivyo kutokana na foleni kua kubwa jion iende irud mda unakua ushaisha vigogo nao wapo bize kutafuna nchi
 
Poleni sana watu wa hali ya chini, pambaneni mtoke kwenye hiyo hali, bila hivyo tabu haitoachana na nyie
 
Kuna tabia ambayo imekuwepo kwa muda, awali ilianza kama kitu kidogo kwa kufanywa na watu wachache lakini sasa hivi inazidi kuwa kama ndivyo uhalisia.

Daladala za kutoka Kawe kwenda Buza (Dar es Salaam) hasa nyakati za jioni zimekuwa na kawaida ya kutokamilisha ‘ruti’, zinaishia Buguruni kisha baada ya hapo zinageuza kurejea Kawe au zinasogea hadi cha Chama kilichopo maeneo hayo na kuanza kubeba abiria upya kuelekea Buza au maeneo mengine.

Hiki wanachokifanya si sawa kwa kuwa kinatuumiza sisi Wananchi hasa wa hali ya chini ambao maisha yetu yanategemea usafiri wa Daladala.

Maumivu zaidi ni kuwa hivi karibuni Serikali ilitangaza kuongeza bei ya nauli, so nauli zimeongezwa kisha daladala zinaamua kutoza mara mbili nauli, hapo maumivu yake ni makali zaidi ya noma.

Mamlaka za usafiri wa ardhini ziangalie hili suala, tunaumia kwa sana.
View attachment 2908995
Hili ni moja ya Daladala ambayo ilikatisha ruti nami nikiwa ndani ya basi hilo nikalazimika kuanza kutafuta usafiri mwingine.
Kwann na nyinyi mkakubali kushushwa katikati ya safari ? Ina maana wanaume wazima mkishindwa kumkomalia dereva apeleke gari mpaka mwisho wa safar? Watanzania tumezidi uzuzu na ndio maana CCM inatufanya vibaya Kila kukicha.
 
Back
Top Bottom