LATRA kujadili Shinikizo la Wamiliki wa Mabasi linalotaka nauli mpya za Daladala, Mabasi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhi (LATRA) imekusudia kuitisha mkutano wa wadau wa sekta ya usafiri nchini kupokea maoni kuhusu marejeo ya nauli za mabasi ya mikoani na daladala.

Aprili 2022, LATRA ilitangaza kupanda kwa viwango vya nauli kwa daladala ilikuwa kuanzia kilomita 0 hadi 10 ilipanda kwa Sh100 wakati kwenye mabasi ya mikoani daraja la kawaida kwa kilomita moja iliongezeka kwa asimilia 11 kutoka Sh36 hadi 41.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 18, mwaka huu Dar es Salaam na shinikizo la kufanya hivyo linatokana na kampuni za Super Feo, Enterprises, ABC Upper Class na Happy Nation kuwasilisha maombi ya kupitiwa upya nauli kutokana na ongezeko la gharama za uendeshaji unaosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa kwa umma na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano LATRA imeonesha kampuni hizo zimetoa mapendekezo tofauti ya kuongeza nauli kutoka ya sasa ya Sh56.88 kwa kilometa 1 kwa kila abiria.

“Super Feo Enterprises kwa daraja la Kati imependekeza Tsh. 101.88 ongezeko kwa kilomita moja Tsh. 45.00 sawa na asilimia 79.11, Kampuni ya ABC daraja la Kati Tsh. 92.84 ongezeko la kilomita moja Tsh. 36.96 ikiwa sawa na asilimia 63.22 na Happy Nation kwa daraja la kati Tsh. 84.06 ongezeko la Tsh. 27.18 sawa na asilimia 47.78,” imesema.

Kupitia barua hiyo imesema sheria ya Mamlaka ya LATRA, sura ya 413 na kanuni ya 9(3) ya kanuni za Latra (tozo) za mwaka 2020 (tangazo la Serikali Namba. 82 la Julai 2,2020, Mamlaka inapaswa kutoa fursa kwa kampuni hizo kuwasilisha mapendekezo yao kwa wadau wa usafiri wa abiria kisha kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi.

“Nauli zinazotumika kwa sasa zilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 18 la Mei 6, 2022 na mamlaka imeandaa mkutano wa wadau kupokea maoni juu ya mapendekezo ya watoa huduma ya kufanya marejeo ya nauli za mabasi ya masafa marefu,” imesema taarifa hiyo.

Katika mkutano huo, LATRA itawasilisha mapendekezo ya vigezo vya mchakato wa kuridhia mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma mijini (daladala). Wasilisho litafanywa kwa mujibu wa kanuni ya 13 ya kanuni za tozo za Mwaka 2020.

“Kutokana na umuhimu wa suala hilo wadau wote wa usafiri wa umma na wananchi kwa ujumla tunawaalika kuhudhuria mkutano huu muhimu ili kutoa maoni baada ya kusikiliza mapendekezo yatakayowasiliishwa na kampuni zilizoleta maombi ya kufanya marejeo ya nauli,” imesema.

Angalizo
LATRA imetahadharisha wakati mchakato huu ukiendelea, inawashauri wamiliki wa mabasi na watoa huduma wote wa usafiri wa umma kuendelea kuzingatia masharti ya leseni zao kwa kutojipangia nauli kinyume na Sheria.

“Adhabu ya kutoza nauli isiyo halali ni Sh250,000 kwa mujibu wa kanuni ya 30 ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji (Mabasi ya Abiria) za Mwaka 2020, mamlaka haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mmiliki au mtoa huduma yeyote atakayekiuka Sheria na Masharti ya Leseni yake,” imesema.

MWANANCHI
 
Athari za kupanda kwa gharama za mafuta.

Kwenye hili sakata anayeumia mwisho ni mlaji wa mwisho ambaye ni Mwanachi wa kawaida.

Maana viongozi wengi husafiri kwa ndege pamoja na kutumia magari ya Serikali 🙌
 
Paza wewe sauti
Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Paza wewe sauti
Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Paza wewe sauti
Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Paza wewe sauti
Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mbona makampuni ya Mabasi Mengine wamepandisha tayari?
====
Yaani aliyetaka kuleta usafiri wa treini inayotumia Umeme wetu w Maji walimuita mshamba na baadhi wakachekelea. Angesikilizwa na aliyoanzisha yakamaliziwa haya madhila yanayotusibu yasingetupata!!!

Bwawa la Maji ya umeme liishe na treini ikamilike uone ka changamoto hii itajirudia.

Utakumbukwa. Ulikuwa na maono.
 
Huu ndio ujinga SAS serkali ingekuwa Ina bus zake za mikoani na uda za kila mkoaa hata wasingetishika na hao walanguz

Naona Mia kwa kila ruti ikirejeww wakt nauli ya Mia tano kwa hata haijamaliza mwaka tayari inapindukaaa wakt tulikaa kwa nauli ya Mia 400 all most miaka 8


Samia naomba ujitadhimi kwa kweli mama angu Hadi mwakni nauli itakuwa laki mbili kwenda mwaza dar
 
nawambieni ukweli na mnisikie hivi vita vya israel na warabu kama vitaendelea tutapata shida sana africa sababu mafuta ndio yanatokea huko nakama mnabisha subirini mwezi wa 11 katikati au mwishoni mtajua shida iliyopo
 
Back
Top Bottom