ZZK aililia nchi ya asali

ZZK aililia nchi ya asali

kisugujira

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
774
Reaction score
200
Hivi karibuni Mh.Zito Kabwe akiwa katika moja ya ziara zake mkoani Tabora amesema "Kosa lenu kubwa mnalolifanya wanaTabora ni kuendelea kuikumbatia CCM kwa kuipigia kura na kuichagua bila kupata mafanikio yoyote mazuri ya kimaendeleo kwa muda mrefu!"

Ameifananisha Tabora na nchi ya Malawi kwa kusema,"Kama Malawi ambayo ni nchi ndogo uchumi wake unategemea tumbaku na imeweza kupata mafanikio hayo yaliyopo sasa, kwa nini imeshindikana kwa Tabora hapa nchini ambayo inatoa asilimia 75 ya tumbaku yote inayolimwa hapa nchini?"

Mapato yanayotokana na tumbaku, mazao ya misitu (mbao na asali) na madini yanayochimbwa mkoani Tabora kwa Taifa hili ni makubwa sana ukilinganisha na huduma za kijamii (afya,maji,umeme,barabara,nk) zinazotolewa na serikali ya CCM kwa wanaTabora!
 
hicho ni kitu kinachosikitisha sana kwa wana Tabora,wakati Nyerere anang`atuka usafiri wa treni ulikuwa kila iitwayo leo,lakini Leo ni mara mbili kwa siku na wanazungumzia kuifufua reli ya kati,najiuliza aliiua nani?Na ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya walioua,kwa masikitiko wanawapa nafasi ya kuwaongoza nahisi wana Taborea wenzangu kuna aliyewaroga.

Miaka 50 ya uhuru ukizingatia mchango ambao Tabora ilitoa katika harakati za ukombozi wa Tanzania hadi leo makao makuu ya mkoa hayajaunganishwa kwa barabara ya kiwango cha lami,usafiri wa uhakika hakuna kama ilivyokuwa enzi za Nyerere lakini kwa sababu wakazi wameshikiwa akili na CCM bado wako kwenye kudumisha fikira za mwenyekiti ambaye kwa sasa ni Kikwete.Na mwenye akili na uchungu wa Tanzania anaona chini ya uongozi wake ilipofikia,udini,ukabila mauaji ya wanahakati na hali ya maisha kuwa ya juu,WANATABORA INABIDI KUOMBEWA ILI TUBADILIKE hata mnyama ukimuonea atakurarua labda awe kondoo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
WALAANI VIONGOZI WAKE
 
[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]

Mkuu CENCER nifanikiwa kufika tbr nikakaa wk 3, wale watu wanahitaji maombi maalumu sio bure, sikutaka kurudi tena huko, ukitoka nzega kwenda tbr utafikiri unaenda AHERA nililala siku 3 kuuguza maumivu ya kichwa kuna mashimo utadhani mahandaki, nilirushwa nkajigonga kwenye roof ya basi ni balaaaaaaaa, rudini mkawakomboe wenzenu mzee
 
Back
Top Bottom