Zuma atajwa tena kashfa ya rushwa

Zuma atajwa tena kashfa ya rushwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Rais wa zamani wa Afrika Kusini amenukuliwa kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki hii na tume ya uchunguzi inayohusika na kutoa mwanga kuhusu mashtaka ya rushwa alipokuwa madarakani.

Shahidi mmoja amemshtumu Jacob Zuma kwamba alikuwa akipokea rushwa kila mwezi kutoka kampuni ya usalama.

Kulingana na Angelo Agrizzi, afisa wa ngazi ya juu katika kampuni ya usalama ya Bosasa, rais wa zamani wa Afrika Kusini alikuwa akipokea euro 20,000 kila mwezi.

Angelo Agrizzi, ambaye katika siku nane za ushuhuda mbele ya tume ya uchunguzi tayari amewahusisha Wakurugenzi wakuu wa makampuni ya umma, waziri mmoja na waandishi wa habari.

Jacob Zuma alilipwa kwa fedha taslimu, ambazo ziliwekwa kwenye mkoba na kupelekwa na mtu maalumu, Dudu Myeni, ambaye wakati huo alikuwa kwenye nafasi kiongozi wa Wakfu wa Zuma Foundation na rais wa shirika la kitaifa la ndege.

Sw.rfi
 
katiba yetu inazingua sana,kuna viumbe walitakiwa wapotee uraiani. mgodi wananunua kwa m.70 ila kimyaa kama hakuna lililo tokea.
 
Back
Top Bottom