Zuma aponyoka kura ya kutokuwa na imani naye

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,527
865
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amepenyoka kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Zuma alipata kura kutoka kwa wabunge 233 wanaomuunga mkono dhidi ya 143 za wabunge ambao hawakuwa na imani naye.

Awali naibu spika alikuwa amewataka wabunge wapaze sauti hadharani kuhusu iwapo alikuwa anaunga mkono kura ya kutokuwa na imani au la.
 
Ameponyoka lakini heshima yake imetelemka sana na kifikia kiwango cha chini sana kuliko watu wote nchini humo
 
Zuma ana mambo huyo. Ila heri yao wamemuumbua na kakubali. Ila fisadi aliekuwa pm sasahv anapeta tu.
 
Wabunge wa ANC wamempigia kura sio Kama wanaimani naye ila wamepiga kura ya kulinda chama, wameogopa Kama kilicho tokea kwa Thabo mbeki kisije tokea tens.
 
Hata ingekuwa Tanzania.hakuna jipya zaidi ya hayo yaliyotokea South Africa.viongozi hawafuati katiba na maslahi mapana ya nchi wanalinda maslahi binafsi na vyama vyao.'AFRICA THE SLEEPING GIANTS'
 
bado siuoni mgawanyo wa madaraka ikiwa mahakama imeona ana hatia hata kura asingstahili zaidi ya kuukabili mkondo wa sheria
 
Hata ingekuwa Tanzania.hakuna jipya zaidi ya hayo yaliyotokea South Africa.viongozi hawafuati katiba na maslahi mapana ya nchi wanalinda maslahi binafsi na vyama vyao.'AFRICA THE SLEEPING GIANTS'
walau Katiba yao inaruhisu Raisi kushitakiwa akingali madarakani ingawa haina meno sana kitikadi
 
waasisi wa ANC wanaandaa maandamano makubwa ya slogani yao ya pay and go hii nadhani itamsumbua kidogo kuriko kura..
 
Je sheria inasemaje? Je raia au taasisi ina uwezo wa kumshitaki rais zaidi ya bunge? Linaloweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais, kama bunge likipiga kura ya kuwa na imani na rais, je sheria inasemaje, watalaam wa sheria nadhani watatufafanulia.
 
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amepenyoka kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

Zuma alipata kura kutoka kwa wabunge 233 wanaomuunga mkono dhidi ya 143 za wabunge ambao hawakuwa na imani naye.

Awali naibu spika alikuwa amewataka wabunge wapaze sauti hadharani kuhusu iwapo alikuwa anaunga mkono kura ya kutokuwa na imani au la.

Bila shaka ameponyeka ni kwa maslahi ya chama sio taifa weusi bana.
 
Kwa mujibu wa katiba inamaanisha wana imani naye. Lakini kitendo tu cha kupigiwa kura halafu tena zaidi ya wajumbe 100 kukukataa hiyo inatosha kabisa kudhihirisha kuwa watu hawana imani nawe.
 
Zuma ndo profesa wa siasa za South Africa,hakuna wa kumtoa mpaka ifike muda wa kutoka mwenyewe
 
Back
Top Bottom