Zuio la safari za nje kuokoa billion 900 ni uongo!! Kwanini tunadanganywa??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Imekua ni kawaida watanzania kudanganywa tena na taasisi nyeti sana. Sijui lengo lao ni nini!!
Na cha ajabu hawakosi watu wa kuunga mkono uongo huo!!

Tulidanganywa na ofc ya waziri mkuu kwamba zimetolewa trilion moja kwa ajili ya dawa tulipinga uongo huo hakuna aliyekuja kutolea ufafanuz taarifa hiyo mpaka leo japo ilitolewa na pm mwenyewe!!

Kuna taarifa ya hivi majuzi toka BOT inasema tangu rais Magufuli azuie safari za nje zimeokolewa sh billion 900. Ambazo hizo zimetokana na kuzuia kwa safari kwa 36% pekee. Unajiuliza asingezuia zingetumika sh ngapi?? Kama kazuia kwa 36% zimeokolewa b900? Hii pia ina maana 64% wamesafiri na kutumia takribani sh trillion 1.5 ! Je ni ya kweli haya??

Hebu tujikumbushe kidogo huko nyuma.

Wakati rais magufuli anaapishwa alilaan sana safari za njee! Na alitamka pesa iliyotumika kwa takribani miaka mitatu kuwa ni sh billion 356.3.
Na pesa hiyo ni miaka mitatu. Kwa wastani zilitumika bilion 118 kwa kila mwaka mmoja . Na hizo billion 118 ndizo alikemea na kuziona nyingi. Iweje hizi figa za kuokoa billion 900?? Mbona sielewi elewi?? Ina maana zilikua zinatumia sh ngapi kwa mwaka mmoja enz za jk, wanataka kutuambia zilitumika trion 2.6 kwa mwaka mmoja?

Nategemea katika utawala huu iwe chini ya b 118, iweje waokoe b 900 ?? Wakati safari zimepungua kwa 36% pekee??
Kwann viongozi wanapenda kutudanganya??
Kuna nini nyuma ya huu uongo??

Hata kama watanzania ni wajinga sio kwa kiasi hiki. Tafadhari viongoz wetu tupeni heshima yetu hata kama kuna baadhi wanasifia kila kitu kumbukeni kuna watu wana diriki kusema IMEKUWAJE!

Hebu jisomee mwenyewe baadhi ya matukio ya huko nyuma.

MICHUZI BLOG: WIZARA YATOA UFAFANUZI WA Safari za Rais Kikwete Nje ya Nchi

Magufuli: Safari za nje zingejenga kilomita 400
c5f0e5755248ca26e7c5be8ea3911564.jpg
01428d8c96ce91c30b09bcba6b333312.jpg
 
Ofisi za umma umezi include?

Naam boss, ofice ya rais pekee ilikua kiwango pekee kutumika cha juu ni b50 ambayo ilikua ni mwaka wa fedha 2014 /15. Huko nyuma ilikua nusu yake. Soma vizuri kwenye picha nilizo ambatanisha hapo juu , baada ya tuhuma kuwa nyingi za matumiz ya fedha.
 
Hata kama zimeokolewa, zimefanya jambo gani linalomgusa mtanzania moja kwa moja? maana tumezoea kudanganywa kila siku ohoooo, watumishi hewa, mara ohoooooo, safari za nje, mbona leo hawatangazi makusanyo kama walivyokuwa wanafanya kipindi cha nyuma? viongozi semeni ukweli wenu kuhusu hali halisi ya uchumi wa taifa hili na siyo kujificha nyuma ya pazia
 
Nakupinga kwa asilimia 100. Mimi mwenyewe nlienda nje ki masomo na sikulipwa hata coin na nlikuwa entilted kulipwa milioni 15 kwa miezi 3. Sikulipwa sababu safari, malazi, chakula vyote viligharimiwa na nchi nilokwenda. Na kwa utaratibu zamani ilikuwa ukienda tz wanakulipa na nchi unayoenda wanakulipa. Nakubaliana kabisa kwamba safari za nje zimesaidia kupunguza matumizi kwa asilimia kubwa sana
 
Watu kama nyie ndio mnasabisha Jf itake kufungiwa kwa kuhoji kwa fact na positive argument..........

Kichekesho eti wanakwambia tunalipa madeni ya billion 900 kila mwezi yaani ni aibu tupu.......

Tuna safari ndefu sana na Siri-kali.......
 
kwa kweli umesema wakiwa wanatupiga changa wajue basi kuna wengine tupo na fahamu zetu kamili billion 900 sio ya mchezo mchezo hata kidogo
 
Nakupinga kwa asilimia 100. Mimi mwenyewe nlienda nje ki masomo na sikulipwa hata coin na nlikuwa entilted kulipwa milioni 15 kwa miezi 3. Sikulipwa sababu safari, malazi, chakula vyote viligharimiwa na nchi nilokwenda. Na kwa utaratibu zamani ilikuwa ukienda tz wanakulipa na nchi unayoenda wanakulipa. Nakubaliana kabisa kwamba safari za nje zimesaidia kupunguza matumizi kwa asilimia kubwa sana

Mpendwa hatukatai kuokolewa kiasi cha pesa, tunahoji hizo b900 zimeokolewa vip wakati huko nyuma hazkuwahi kutumika?? Tumekupa vielelezo pesa zilizotumikaka miaka ya nyuma ni wastan wa b118 kwa mwaka . Kama kuokoa tunategemea tuambiwe zimeokolewa bililion kama 30 hiv iweje iwe billion 900? Tumia ubongo wako kidogo. Wasifikilie wengine kwa niaba yako
 
Back
Top Bottom