Zuio la Magufuli kusafiri laathiri soko la masanduku yenye magurudumu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Jana nilipita madukani kununua trunker la mtoto anayeenda shule.Wauzaji kibao walinikimbilia wakiniambia kama nataka sanduku lenye magurudumu wataniuzia bei poa hata ya kutupa kwani hawajauza siku nyingi hamna wanununzi.

Wauzaji wanasema mwanzoni mwa mwaka huwa wanapata wateja wengi hasa wale wanaosafiri sana na ndege kwenda nje ya nchi ambao hununua hayo masanduku yenye magurudumu kubadili ya zamani ambayo husema magurudumu yake yanakuwa yamechakaa kwa kuburuzwa sana kwa safari nyingi walizosafiri mwaka mzima.

Agizo la Raisi la kuzuia wafanyakazi kutosafiri nje ya nchi limeathiri soko la masanduku yenye magurumu ambayo wasafirio na ndege kwenda nje ya nchi huyaburuza kwa mbwembwe airports mbali mbali huku wakiimba nyimbo za kizungu za akina Jim REEVES wanapoyaburuza
 
Kwakuwa ni durable goods wavumilie/ama kufanya biashara zingine mpaka atakapoziruhusu hizo safari tena.
 
Back
Top Bottom