Huu sii uchochezi? Wadai msimamo wa Rais Magufuli kupinga uzazi wa mpango utalitia umasikini bara lote zima la Afrika! Je, kuna ukweli wowote?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali

"Huu sii Uchochezi? Gazeti Ladai Msimamo wa Rais Magufuli Kupinga Uzazi wa Mpango Utalitia Umasikini Bara Lote Zima la Afrika!. Jee Kuna Ukweli Wowote?.

Hebu soma hii ni headline ya makala kwenye jarida la the Economic la wiki hii:

"Africa’s high birth rate is keeping the continent poor "
Hii inamaanisha wanasema wanadai kiwango kikubwa cha kuzaliana barani Afrika, ndiko kunakosababisha bara ka Africa tubaki Masikini.

Baada tu ya kichwa hicho cha habari, sasa soma habari yenyewe, ni tangu sentensi ya kwanza ni Magufuli mwanzo mwisho!

DemographyAfrica’s high birth rate is keeping the continent poor

Why the birth rate has been slow to fall
Print edition | Middle East and Africa
Sep 22nd 2018
JOHN MAGUFULI, the president of Tanzania, has strong views about birth control. He does not see the point. In 2016 he announced that state schools would be free, and, as a result, women could throw away their contraceptives. On September 9th this year he told a rally that birth control was a sign of parental laziness. Tanzania must not follow Europe, he went on, where one “side effect” of widespread contraception is a shrinking labour force.
There seems little danger of that. Tanzania’s fertility rate is estimated to be 4.9, implying that the average woman will have that many children. Europe’s rate is 1.6. Tanzania is helping drive a continental baby boom. In 1950 sub-Saharan Africa had just 180m people—a third of Europe’s population. By 2050 it will have 2.2bn—three times as many as Europe. If UN forecasts are right, sub-Saharan Africa will have 4bn people in 2100 (see chart 1).

That is worrying, although not for the old reasons. In “An Essay on the Principle of Population”, published in 1798, Thomas Malthus claimed that the human population was bound to increase faster than the supply of food, leading to catastrophe. Although Malthus is still admired by some, the green revolution rubbished his hypothesis. The fear now is not that countries will run out of food but that a surfeit of babies will retard their development.
Mr Magufuli is right to suggest that Europe has many old people and could do with more workers to support them. But Tanzania’s many children weigh on its economy, too. Sub-Saharan Africa’s dependency ratio (the population younger than 20 and older than 64 versus the population between those ages) is 129:100, compared with 65:100 in Europe. Sub-Saharan Africa is expected to have a worse dependency ratio than Europe even in 2050.
20180922_MAC359_2.png

High fertility can also be seen as a global problem, says Bill Gates, whose foundation (jointly run with his wife, Melinda) will hold a conference next week about the state of the world. Overall, humanity is becoming wealthier. But because birth rates are so high in the poorest parts of the world’s poorest countries, poverty and sickness are that much harder to eradicate. “Kids are being born exactly in the places” where it is hardest to get schooling, health and other services to them, he explains.
There is nothing inherently African about large families. Botswana’s fertility rate is 2.6, down from 6.6 in 1960. South Africa’s rate is 2.4. And although the UN has a good record of predicting global population growth, it has got fertility projections badly wrong in individual countries. Sudden baby busts in countries like Brazil, Iran and Thailand caught almost everyone out. Could Africa also spring a surprise?
The UN’s demographers project that fertility will fall in every single mainland African country over the next few decades. They just expect a much slower pace of change than Asia or Latin America managed when their families were the same size. It took Asia 20 years, from 1972 to 1992, to go from a fertility rate above five to below three. Sub-Saharan Africa is expected to complete the same journey in 41 years, ending in 2054. Its fertility rate is not expected to fall below two this century. Because many Africans marry young (see next article) the generations turn over quickly, leading to fast growth.
The reason the UN expects change to be slow in future is that it has been slow until now. After stagnating economically in the 1990s, countries like Nigeria and Tanzania grew wealthier in the 2000s. But their fertility rates hardly fell (see chart 2). Nor has urbanisation transformed family life as much as you might expect. West Africa is much more urban than east Africa, but has a higher fertility rate.
20180922_MAC343_2.png

Three things could drastically change the picture, however. First, more African governments could promote family planning. Ethiopia, Malawi and Rwanda have done so, and their birth rates are dropping faster than average. Perhaps the starkest change is in Kenya. Alex Ezeh of the Centre for Global Development, a think-tank in Washington, remembers showing Kenyan politicians evidence that wealthy people both desired and had small families, whereas the poor wanted large families and ended up with even larger ones. The government invested in clinics and propaganda, to some effect. Household surveys show that 53% of married Kenyan women used effective contraception in 2014, up from 32% in 2003. Kenya’s neighbour, Tanzania, is at least a decade behind.
The second cause for optimism is education. Broadly, the more girls go to school in a country, the lower that country’s birth rate. This seems to be more than just a correlation: several studies, in Africa and elsewhere, have found that schooling actually depresses fertility. To attend school—even a lousy school where you barely learn to read—is to gain a little independence and learn about opportunities that your parents had not envisaged for you.
Researchers at the International Institute for Applied Systems Analysis in Austria suggest that Africa’s schools are about to drive a large change. They point out that education spending weakened in some African countries in the 1980s as governments scrambled to cut budget deficits. Girls’ schooling, which had been increasing, flattened. It is probably not a coincidence that African fertility rates fell little in the 2000s, when that thinly educated cohort reached womanhood. But school enrolments have risen since then. If education really makes for smaller families, that will soon be apparent.
The third profound change would be stability in the Sahel. The semi-arid belt that stretches through Burkina Faso, Chad, Mali, Niger, northern Nigeria and Sudan is lawless in parts and universally poor. Child death rates are still shockingly high in places. Partly as a result, and also because women’s power in the Sahel is undermined by widespread polygamy, people still desire many children. The most recent household survey of Niger, in 2012, found that the average woman thought nine the ideal number.
Progress on all three counts depends mostly on African politicians. It falls to them to create more and better schools, provide security for their people and invest in family planning. They, not foreign observers, need to conclude that their countries would be wealthier if they had rather fewer children. Like so much in Africa, almost everything depends on the quality of government. And that, sadly, is hard to decree.
This article appeared in the Middle East and Africa section of the print edition under the headline"Babies are lovely, but..."
Lengo la habari yoyote ni ama kuhabarisha, ama kuelimisha, au kuburudisha. Headline kama hii, lengo lake ni uchonganisha, kuiambia dunia kuwa msimamo wa rais Magufuli kupinga uzazi wa mpango, sio tuu utaongeza umasikini Tanzania, bali wana suggest msimamo huu wa rais Magufuli ukiachwa, sio tuu Watanzania ndio watakaozaliana na kuongezeka, bali kuongezeka kwa Watanzania, kutaongeza umasikini kwa bara zima la Afrika!, kitu ambacho sii kweli!.

Japo utafiti umethibitisha kwa kadri watu wanavyokuwa matajiri, ndivyo wanavyotaka familia ndogo, na kwa kadri watu wanavyokuwa masikini ndio wanazaa watoto wengi, hivyo hawa Economists wanataka kuiaminisha dunia kuwa kitendo cha rais wa Tanzania kupinga uzazi wa mpango, kutawafanya Watanzabia ambao tayari ni masikini wa kutupa, wengi wakiishi kwenye lindi la umasikini wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, wamehamasishwa waachane na uzazi wa mpango, hivyo wazaane waongezeke, kutaongeza number ya masikini Tanzania, hivyo kuongeza the overall rate ya umasiki wa Bara la Africa!.

Wakati hawa the economists wanayasema haya, hawazungumzii kabisa jinsi Tanzania tulivyo matajiri!, juzi Tanzania tumekuwa nchi ya tatu barani Afrika tumenunua ndege kubwa, jipya na la kisasa the dreamliner kwa pesa cash, kuonyesha jeuri ya pesa, wakati hata hao matajiri wenyewe wakiwemo Marekani, huwa hawanunui kwa cash money, bali hununua kwa mkopo, hire purchase!. Hawa the economic hawaoni tulivyo matajiri, japo tuna reli mbili ambazo tumeshindwa kuzitumia, lakini kwa jeuri ya pesa, tunajenga reli mpya ya kisasa ya SGR itakayotumia umeme, kwa fedha zetu za ndani!, juzi tumezindua barabara ya juu kwa juu, yote haya hawa the economists hawayaoni, wao wanaona umasikini tuu!.

Wazungu walipokuja, walikututa tunazaliana sana, ndipo wakatuletea maujinga yao ya uzazi wa mpango, na madawa yenye masumu kibao yanayoharibu wanawake wetu!. Vikwazo vya familia kubwa vilikuwa vitatu tuu, kulisha, kuvisha na kusomesha, sasa rais Magufuli anasomesha bure, hivyo alianza kupinga uzazi wa mpango, kwa kutusisitiza tufyatue tuu watoto, atasomesha bure. Juzi kati alipopinga tena uzazi wa mpango, alisisitiza kama una uwezo wa kulisha na kutunza, uzazi wa mpango wa nini?.

Lengo la hawa the economist ni kujenga hoja, kuwa umasikini wa bara la Afrika unatokana na wingi wa idadi ya watu, hivyo lengo la makala hii ni kulichagiza bara la Africa na dunia kwa ujumla, imshukie rais Magufuli na kuiadabisha Tanzania kwa kitendo chake cha kupingana na uzazi wa mpango kwa hofu ya kuongeza umasikini bara zima la Afrika. Mimi nasisitiza Watanzania tuungane na rais wetu kusema no to family planning za kizungu, kama ni umasikini, then ni umasikini wao sio wetu, sisi Tanzania ni nchi tajiri, and soon tutakuwa a donor counrty mipango yote ya rais Magufuli ikikamilika. Tuna madini ya kila aina, tuna gesi asili ambayo soon tutai export kuiuza nje, tuna vyanzo vya maji na mradi wa Stigler ukikamilika, tutauza umeme nje kwa majirani zetu, tunaelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati, uchumi wa gesi na viwanda, hivyo hata tukizaana tukizaana kama panya, bado nchi yetu ni tajiri, na utajiri wetu sio utaleta utajiri Tanzania, bali utainua viwango vya utajiri kwa bara lote la Africa, sasa idadi ya Watanzania utalitiaje umasikini bara la Afrika badala ya kuliongezea utajiri?.

Wanaume wa kizungu wana low sper.s count hivyo hawawezi kutunga sana, na wanawake wa kizungu na low fertility, hivyo hawawezi kupachikwa sana hivyo wanateletea haya mambo ya family planing ili tufanane nao!. Sisi wanaume wetu ni madume ya mbegu na wanawake wetu ni viwanda vya kutotolea, hivyo rais Magufuli yuko right, Watanzania kazi yetu iwe moja tuu, tufyatue!.

Ila katika ufyatuaji huu, lazima pia tujiulize swali moja la msing. Jee hii population growth inakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi wetu na uwezo wetu wa kuprovide socials services kama hudima za afya, elimu na sanitations?. Kama Watanzania wa sasa ambao tuko milioni 50 tuu ndio tuna umasikini huu tulionao, na kwa birth rate ya asilimia 5% kwa mwaka, kama tutaufuata ushauri wa rais wetu Magufuli na kuachana na family planing, hivyo kila mtu angalau azae watoto 4, baada ya miaka 32 tuu, yaani 2050, Watanzania tutakuwa milioni 200!. Jee tutakuwa na uchumi wa kubeba ongezeko hilo la watu, tutakuwa na chakula cha kuwalisha?, tutakuwa na miundombinu ya kusupport idadi hiyo ya watu?, tutakuwa na social services za kuwahudumia?.

Paskali.
Tujikumbushe




Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!. - JamiiForums

Rais Magufuli ni Mkweli Daima!. Jee Tumuunge Mkono Rais Wetu Katika Kila Ukweli Wake, Hata Kama Uko Kinyume cha Katiba, Sera na Ilani?. - JamiiForums

"Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?" - JamiiForums
Update 1
Huu ni mchango very objective
Watu ni nguvu kazi kama utawatumia inapasavyo,Umasikini wa Afrika haupo kwa sababu ya wingi wa watu,Umasikini wa Afrika unaletwa na mipango mibaya ya viongozi wa Kiafrika kwa watu wao..

Wingi wa wa watu sio neema kwa nchi,Nchi ya Japani ina watu wengi sana ukifananisha na ukubwa wa nchi lakini Japani ni moja ya nchi zilizoendelea sana Duniani,kuna Nchi za Ulaya Magharibi haziwezi hata siku moja kuukaribia uchumi wa nchi ya Japan...

Kutozaliana ni kukosa nguvu kazi,Nchi nyingi za Ulaya Magharibi zina ukosefu wa nguvu kazi kwasababu watu hawazaliani,Nchi kama Spain wengi wa watu wake ni wazee wasioweza kufanya kazi,kwasababu hiyo,nchi ya Spain inahitaji nguvu kazi kutoka nje ya nchi..

Utajiri ni watu,Wajapani hawahitaji soko la nje kunufaisha biashara zao,soko la ndani linatosha,Nchi ya Nigeria ni nchi yenye watu wengi katikabara la Afrika,Nigeria ni nchi ya Afrika yenye mamilionea wengi kuliko nchi yoyote ile,soko la ndani la Nigeria linanufaisha linatosha kutokana na wingi wa watu ..

Wazungu na hoja za kuwa wafrika kuzaliana sana ni kuleta umasikini kama bara Afrika sio kweli,Wazungu wanawachukia ana Wafrika wanatamani sana watu weusi wamalizike duniani,inasemakana hata maradhi kama Ebola,Ukimwi ni maradhi ya kutengenezwa kwenye library ili kuwamaliza au kupunguza wingi wa watu weusi katika bara la Afrika..

Kwa wale anaosoma historia ya watu weusi Marekani,wanaweza kuungana na mimi kwani kuna matukio mengi ya maradhi ya kutengenezwa waliopewa watu weusi ili kupumguzwa wingi wao,

Mfano miaka ya nyuma watu weusi wa Marekani waliambukizwa ugonjwa wa ndui kwa makusudi,kwa wakati huo ndui zilikuwa hazina dawa,

Watu weusi wametolea kizazi bila ya wao wenyewe kuja,ugonjwa wa ukimwi mwazo walikuwa ni ugonjwa wa watu weusi kuliko weupe.wanasema chimbuko la ukimwi ni Uganda

Hizi sasa inasemekana kuna baadhi ya miji ambayo wanakaa watu weusi wengi inasemekana maji yametiwa chemikali fulani ili kupunguza nguvu za uzazi kwa watu weusi waishio sehemu hizo

Ukweli nakuwa nampinga sana siasa za Magufuli lakini kwa hili niko pamoja nae..Kama tutakuwa na mipango mizuri kwa watu wetu basi watanufaisha taifa,Umasikini unaletwa na mipango mibovu, umasikini hauletwi kwasababu nchi ina watu wengi
Asante.
P
 
China Birth rate: 12.3 births/1,000 population (2017 est.) na bado kila kona flyover za kumwaga,bombadia kama bodaboda, dreamliner kama daladala.university kama vibanda vya vocha tz na hospital kama magenge ya nyanya dar.

Wazungu wazushi sana, kuna watu wanafaidika na program za population control kama ilivyo kwenye madini.
 
Kivuko kimezama tumeshindwa kuokoa ndugu zetu kwa muda muafaka. Wlimu bure vijana wanafika kidato cha nne lakini hawawezi hata kuandika barua ya maombi ya kazi.

Huko mashuleni watoto wanapangana kama viazi darasani, haijulikani yupi ni yupi.

Shule nyingi hazina majengo wala madarasa ya uhakika, walimu hakuna na waliopo wanafanya kazi bora maisha yaende maslahi duni.

Halafu mtu anasema tufyatue tu.

Tatizo la Tanzania ni.
Elimu
Elimu
Elimu
 
China Birth rate: 12.3 births/1,000 population (2017 est.) na bado kila kona flyover za kumwaga,bombadia kama bodaboda, dreamliner kama daladala.university kama vibanda vya vocha tz na hospital kama magenge ya nyanya dar.
Wazungu wazushi sana, kuna watu wanafaidika na program za population control kama ilivyo kwenye madini.
Watoto wa shule tu wanakaa kwenye mawe madarasani kwenye shule za tope huku kwenye wodi za wazazi kina mama wajawazito wanalala mzungu wa nne.

Mikopo vyuo vikuu mnaiota kwa ubaguzi kisa hamna uwezo wa kutoa mikopo kwa wote wenye sifa za kusoma elimu ya juu.

Ajira zimewashinda kutengeneza; huduma za maji shida, watu wana-share maji na mifugo;pembejeo kwa wakulima mnashindwa kutoa mpaka mnanyang'anua wakulima fedha za korosho alafu leo mnataka tuzaliane kama kuku!

Hata milioni hamsini kwa kila kijiji imewashinda.

Bajeti ya nchi bado inategemea wahisani alafu bado tunaona sawa tu kuzaliana bila mpango.

Sisi ni masikini wa mali na akili!!
 
Aliyozungumza Raisi si mageni na najua Paskali unapenda kusoma hebu mtafute mtu aitwae Malthus na theory ya population checks.Alitabiri ya kuwa uzalishaji wa chakula hauendani na ongezeko LA watu na ktk aliyoshauri ni pamoja celibacy huku tukitegemea vitu kama majanga kuthibiti
 
Ifike mahala kama nchi tujisimamie,haya matakwimu ya kupika ya wazungu tuyaweke kando,hawa jamaa furaha yao ni kutu drive.
Hivi paskali nikuulize swali hiyo namba ya watu 200kufikia 2050 una hakika?.kuna majanga ya asili, magonjwa ya mlipuko,yote haya huua watu, lazima namba iwe kubwa kureplace idadi itakayopotea.

Nasema hivi acha wachonge,kama hali yangu ni nzuri kiuchumi ni kuijaza dunia tu
 
China Birth rate: 12.3 births/1,000 population (2017 est.) na bado kila kona flyover za kumwaga, bombadia kama bodaboda, dreamliner kama daladala.university kama vibanda vya vocha tz na hospital kama magenge ya nyanya Dar.
Wazungu wazushi sana, kuna watu wanafaidika na program za population control kama ilivyo kwenye madini.
Exactly!
 
China Birth rate: 12.3 births/1,000 population (2017 est.) na bado kila kona flyover za kumwaga,bombadia kama bodaboda, dreamliner kama daladala.university kama vibanda vya vocha tz na hospital kama magenge ya nyanya dar.
Wazungu wazushi sana, kuna watu wanafaidika na program za population control kama ilivyo kwenye madini.

Huu ni ujinga huwezi kuruhusu raia wako wazaliane kama popo unless you're crazy
 
Paskali hivi unafahamu kama tz hatutaki uzazi wa mpango basi hela za wahisani za M.C.H nazo wasilete. Unajua mtoto anapokuwa na siku 1000 tangia anatungwa mpaka anakuwa M.C.H huwezi kuiacha ndo wahisani wanatoa hela yao hapo ambapo serikali haina uwezo wa kuwahudumia.

Juzi nadhani ulimsikua katibu mkuu wa TAMISEMI anayeshughulikia lishe bora anasema watoto wengi karibia 50% wana udumavu, hawapati huduma bora, balance diet n.k ambazo zinatolewa na hawa wahisani. Kama wahisani wakiondoka na hela zao basi tujiandae kulia kilio cha kusaga meno maana hakutakuwa na clinic ya mama na mtoto. Chanjo za surua, pentavalent, polio, ROTA ndo zinakwenda hivyo. Maana yake sasa ni vifo vya mama na mtoto kuwa vingi na yule atakaye survive basi tutakuwa vilema wa Nigeria na Afganistan

Embu fikirieni kabla ya kutenda
 
Watoto chini ya miaka mitano wanasumbuliwa sana na magonjwa. Katika kipindi hiki kinga yao ya mwili inajiimarisha.

Mama anahitaji matunzo na lishe bora baada ya kujifungua ili kurudisha nguvu pia kupata nguvu ya kulea kichanga.

Wengi tunafahamu michango ya wanawake katika kujenga uchumi. Mfano tu biashara ya chakula kwanini inaitwa mama ntilie au mama lishe?

Kuwa na mpango mzuri kwanza wa afya na chanjo kwa mtoto.

Mama afundishwe uzazi wa mpango kuupa mwili muda wa kurudisha nguvu.

Kuwe na mpango wa elimu ya awali ili watoto wapate malezi na elimu wakati wazazi wao wanazalisha.
 
China Birth rate: 12.3 births/1,000 population (2017 est.) na bado kila kona flyover za kumwaga,bombadia kama bodaboda, dreamliner kama daladala.university kama vibanda vya vocha tz na hospital kama magenge ya nyanya dar.
Wazungu wazushi sana, kuna watu wanafaidika na program za population control kama ilivyo kwenye madini.
Point yako ni nini hapo? Ina maana birth rate ya China ni 1.23% wakati Tanzania ni 5%.
 
Watoto chini ya miaka mitano wanasumbuliwa sana na magonjwa

Naogopa zaidi wahisani wakitoa hela zao hapo sasa mambo ndo yatakuwa mabaya zaidi maana sasa wale manesi wanaotoaga elimu na huduma basi wanarudi kwenye kazi zao halisi za wodini. Mambo za clinic za mama n mtoto ndo zinakufa alafu sikilizia sasa kama mortality rate ya watoto wanaozaliwa ni almost 655 per 100,000 sasa ilitakiwa iwe 15/100,000 naona itapanda mpaka 80,000/100,000 kwa kila kizazi hai.

Maana yake watakao kufa kwa kukosa huduma bora za afya ni zaidi ya nusu na huduma zitakuwa kama huna bima ya afya basi jiandae wewe mama kufa au mtoto kufa au wote.

Tatizo tuna kichaa anayeongoza wenye akili
 
Naogopa zaidi wahisani wakitoa hela zao hapo sasa mambo ndo yatakuwa mabaya zaidi maana sasa wale manesi wanaotoaga elimu na huduma basi wanarudi kwenye kazi zao halisi za wodini. Mambo za clinic za mama n mtoto ndo zinakufa alafu sikilizia sasa kama mortality rate ya watoto wanaozaliwa ni almost 655 per 100,000 sasa ilitakiwa iwe 15/100,000 naona itapanda mpaka 80,000/100,000 kwa kila kizazi hai. Maana yake watakao kufa kwa kukosa huduma bora za afya ni zaidi ya nusu na huduma zitakuwa kama huna bima ya afya basi jiandae wewe mama kufa au mtoto kufa au wote.

Tatizo tuna kichaa anayeongoza wenye akili
Sheria ni moja fyatuaneni msifuate uzazi wa mpango
 
Dunia ina limited resources, tukiendelea kuzaliana kama mapanya miaka michache ijayo tutalazimika kuvamia hifadhi za misitu na mbuga za wanyama ili kujipatia ardhi ya kutosha kuzalisha chakula kwa ajili ya wote, na hali ikiendelea hivyo basi miaka 100 ijayo hatutakua hata na sehemu ya kuwazika marehemu!
 
Ifike mahala kama nchi tujisimamie,haya matakwimu ya kupika ya wazungu tuyaweke kando,hawa jamaa furaha yao ni kutu drive.
Hivi paskali nikuulize swali hiyo namba ya watu 200kufikia 2050 una hakika?.kuna majanga ya asili,magonjwa ya mlipuko,yote haya huua watu,lazima namba iwe kubwa kureplace idadi itakayopotea.
Nasema hivi acha wachonge,kama hali yangu ni nzuri kiuchumi ni kuijaza dunia tu
Anachozungumza mheshimiwa ni sawa ikiwa tutaishi kama Serengeti na kusuburi nature to take its own course. Madam tumekubali ustaarabu hatuwezi kutegemea majanga kuthibiti idadi,tunahitaji mifumo yenye kuhakikisha kuwa maisha yanakuwa enjoyable.
 
Sheria ni moja fyatuaneni msifuate uzazi wa mpango
Sky Eclat najua unatania na hiyo sheria. Hebu tujiulize. Mtoto wa leo si ndiyo mzee wa kesho? Sasa leo tukiwa na watoto wengi haimaanishi kuwa kesho tutakuwa na wazee wengi? Na hilo halitakuwa tatizo tunalojaribu kulikwepa la kuzaa sana ili kuongeza nguvu kazi? ie.tutakuwa na wategemezi wengi (wazee) kuliko nguvu kazi?
 
Je, nchi haina sera ya uzazi wa mpango au ipo, kama ipo, kwanini ipo na kwanini ilitungwa. Je, watunga sera huwa wanapima na kujidhirisha mipango na mikakati ya sera hiyo,Je Nchi kama nchi inaendeshwa kwa kufuata sera zake au, nini maana ya dira, wasomi nisaidieni
 
Back
Top Bottom