Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,434
- 8,581
Tarehe 15.03.2021
Dar,Tanzania.
Nimefuatilia mijadala kwa muda mrefu hapa kwa siku ya jana na leo kwa zuio la CAF kwa mechi ya kesho ya Simba dhidi ya El Merreikh.
Zuio la CAF ni la washabiki kutoingia uwanjani kwa kama ilivyozoeleka huko nyuma. Ama kwa hakika hili ni pigo kubwa katika ustawi wa ushindani kwani kwa kawaida mshabiki ni sehemu ya mchezaji namba 12 uwanjani. Simba inategemea sana mashabiki wake viwanjani ambao hawakati tamaa katika kuishangilia na hujazana kwa wingi viwanjani kuishangilia.
Leo kuwaambia wasiingie viwanjani kuishuhudia timu yao ni pigo japo pigo hilo limetolewa na mamlaka za soka za Afrika ambazo ndio baba ama mama wa soka Afrika.
Lakini je zuio la CAF limekujaje?
Hapo awali kama inavyofahamika katika taifa letu hatupo kwenye lockdown na ni moja ya mataifa machache sana duniani ambayo hayana sheria kali za udhibiti wa janga la corona. Watu wapo free wakimtumainia Mungu wao. Huku wakiwa na furaha ya Rais wao ambaye kutwa haishi kuhamasisha watu kuabudu Mungu na kusisitiza kuhusu tahadhari.
CAF wanaandaa michuano na inaanza na Simba inashiriki kwa maombi yao Simba kuingiza walau idadi ya watu wachache uwanjani.CAF wanairuhusu Simba na kuwa ndio timu pekee kati ya timu zote zinazoshiriki michuano iliyo chini yake.Simba inaingiza watu nusu ya uwanja kwa mechi zake zote inazocheza Dar Es Salaam na CAF ndio watoa ruhusa hiyo.Mechi zaidi ya 3 zinachezwa huku Simba SC ikiingiza watu zaidi ya 30,000. CAF wanaangalia repoti ya makamishna wa mechi zote za Dar Tanzania ambazo Simba inacheza.
Wakati inatoa chagizo la kuruhusu watu kuingia walau nusu ya uwezo wa uwanja kondisheni moja inayotoa ni watu kuvaa barakoa na kukaa kwa walau kiti kimoja mtu kiti kimoja kitupu.Nia ni ile idadi ya nusu uwanja kutimia.
Simba inacheza mechi zake uwanjani na washabiki wengi wa Simba wanajazana viwanjani hawavai barakoa, washabiki hawakai nafasi kwa nafasi kama utaratibu wao CAF unavyotaka.Wanajazana na kuegemeana na bila barakoa na kusababisha wazi kukiukwa kwa taratibu walizoziweka CAF.
CAF kwa kuwa michuano yao inaoneshwa wazi na televisheni mbalimbali duniani wanaona jambo hilo na madhara yake na kwa hofu ya maagizo ya New World Order na mataifa baba yenye nguvu ya kiuchumi juu ya maoambano ya Corona wanaanza kustukia hali hii.
CAF sasa kwa kutoa hukumu,walikuwa na haki kabisa ya kufuta matokeo yote ya uwanjani ya Simba kwa Dar (wengi hatulijui hili ama hatutaki kuliongelea kwa kuwa labda chungu) wao wanatumia njia ya adhabu laini.Wanatualert, wanazuia watu wasiingie kabisa uwanjani na sio kama zuio hilo ni la milele bali ni morning call.
Wanataka tuamke ili next time tutambue kuwa tunapaswa kufuata utaratibu uliowekwa ambao kwa hapa Tanzania watu wamekuwa wavivu na wagumu kuufuata na matokeo yake tunakuja hapa kujipa maneno ya moyo kuwa tumeonewa na kwa sababu ya matokeo yetu chanya.
Kwa kubreach taratibu za CAF halali zilizowekwa ambazo mama yetu TFF amezikubali na ameiambia Simba basi sisi wazi tungeweza kuadhibiwa na CAF kwa kufutiwa mechi zote tu.
Nini hoja yangu?
Hoja ni kuwa tujaribu sana kutii maagizi halali na kuachana na mambo ya hisia hisia.
Tujaribu sana kusikiliza wenye mpira wao wanataka nini tufuate.
Ninayo imani kabisa iwapo muda ungeruhusu na uongozi wa klabu ya Simba ungeweza kukutana na TFF pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya,Wizara ya Habari na Mamlaka ya ulinzi na usalama Tanzania yangejadiliwa ya kujadiliwa kisha TFF wangeomba kwa CAF walau mashabiki waruhusiwe kuingia uwanjani kwa mechi hizo za Dar.Lakini hii ya Merreikh wazi muda hauruhusu na hautoshi.Badala ya kulalama muda wote basi ni muda mwafaka wa kuangalia wapi tulipokosea na kisha kuketi na kuyafanyia kazi makosefu hayo na hatimaye kurejea tena ktk utaratibu halali unaotakiwa na sio kuvunjwa kwa utaratibu.
Nawasilisha.