Kuna mdada siku moja tulikua nae kwenye dala dala anachati na Ki iphone chake halafu kadumbukiza kidole kwenye vile vi Pete kwenye haya ma cover ya siku hizi..Bahati mbaya alikua kakaa Dirishani Mimi maskini ya Mungu nimeingia kwenye daldala nimekosa siti Nimesimama.
Dada anaperuzi na kudadisi Alitokea msela mmoja Anauza maji nnje akapita Trip ya kwanza nikamuona Trip ya Pili akapita hana Maji alipita na ile simu ya yule dada Bado kidogo amtoe kidole dada wa watu..Sista badala ya kulia "simu yangu simu yangu" akawa anaita "kidole changu kidole changu" badae ndo BEAT likwa na chemistry nzury akaanza kulia vizuri "Simu yangu kidole changu,simu yangu kidole changu"
wabongo tulivyo waoga hadi tulosimama walokua wanachat kuskia mtu kaporwa simu eti wakaacha kuchat wakaingiza simu mifukoni...Gari likaanza na story mpk tunafika.