Zoezi vitambulisho vya taifa kuanza Jumatatu

Zoezi vitambulisho vya taifa kuanza Jumatatu

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Vitambulisho.jpg


Vitambulisho vya Taifa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imetangaza kuanza kwa zoezi la uchukuaji alama za vidole na upigaji picha kwa watu wote waliojaza fomu za kuomba vitambulisho vya taifa, litakaloazaJumatatu ijayo.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati kutoka NIDA, ThomasWilliam, ilisema kuwa zoezi hilo litaanza kwa kanda na litaanzia Wilaya ya Temeke.
Alisema zoezi hilo litakalodumu kwa wiki moja katika wilaya ya Temeke, litaanzia katika maeneo ya Kimbiji, Simbamnazi, Kigamboni, Vijibweni, Mjimwema, Somangila, Kisarawe II na Tungi.
Alisema mitaa itakayoanza na zoezi hilo ni ya Mgeni Nani, Mtoni Kijichi na Misheni iliyopo katika Kata ya Kijichi.
William alisema baada ya kumaliza kwa Wilaya ya Temeke, zoezi hilo litaendelea katika Wilaya ya Ilala na kumalizia Wilaya ya Kinondoni.
CHANZO: NIPASHE
 
duh ! Vigezo gani vimetumika kuanzia Temeke ? Nimestuka !
 
mbn wengine mpk vimeshapotea au kuharibika
 
zoezi la vitambulisho halina maana, ni njia ya kula pesa za walipa kodi,
nasema hivi kwa sababu tuna mavitambulisho kibao yanayotutambulisha ndani na nje ya nchi kwa mfano pasport za kusafiria zinatutambulisha kimataifa, ukija humu ndani kuna utitiri wa mavitambulisho kama nssf/lapf/ppf/pspf, nhif, vitambulisho vya kazini, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu (leaving na academic), nk nk.

kama tunafuta matumizi ya vitambulisho vingine sawa nitaunga mkono zoezi hili vinginevyo ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.
 
Tungewaomba serikali kushirikisha jeshi la ulinzi,idara ya uhamiaji na serikali za mitaa kwa utambuzi hasa katika maeneo ya pembezo na baadhi ya maeneo mijini ili kuthibiti wahamiaji haramu kupata haki isiyokuwa yao.
 
Nadhani wangesitisha mpaka hii issue ya katiba/Muungano ipatiwe majibu kuepuka gharama mara mbili!
 
tanzania ni nchi moja nzuri tu tatizo watu wake ndio wabaya kwani wamejaa tamaa na kuwaza makubwa huku madogo hawayawezi by the way tutoe ushirikiano tuvipate sijui kule remote areas zitafika lini.
 
Back
Top Bottom