Shepherd
JF-Expert Member
- Dec 14, 2012
- 2,425
- 1,653
Nafikiri RC angetumia Taasisi ya Taifa ya Takwimu kupata tarifa azitakazo au angeomba ushauri jinsi ya kufanya hilo zoezi kutoka Taasisi ya Takwimu ya Taifa au wana sheria watutafsirie sheria ya takwimu ya mwaka 2015 inasemaje kama unataka kupata idadi au tarifa ya utafiti.Mwaka Jana 2015 mwezi wa kumi na moja Ilianza kutumika sheria mpya ya takwimu ya mwaka 2015 inayotoa mwongozo jinsi ya kufanya zoezi la takwimu.Nadhani ingekuwa vyema kama angetumia tafiti na tarifa za hii Taasisi ya Takwimu ya Taifa kujua idadi ya wakazi wa Dar wasio na kazi kuliko hili zoezi jipya analotaka lifanyike.Kabla ujachangia usome huu uzi uelewe pia majukumu ya Taasisi ya Taifa ya Takwimu kwenye website yao alafu uchangie. Lengo langu ni kufikirisha jinsi ya kupata taarifa kirahisi kwa kutumia Taasisi zilizopo kisheria bila ya kutumia resources kufanya jambo lenye majibu tayari na sina lengo la kupingana na zoezi la RC yeye kaona linafaa akifanya kama anavyotaka kulifanya mimi kwa mtazamo wangu kujua idadi ya wasio na kazi angetumia tarifa za NBS.