Zoezi la ukaguzi magari na changamoto mpya

Zoezi la ukaguzi magari na changamoto mpya

Dr Guitar tz

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2018
Posts
312
Reaction score
247
Nimefuatilia kipindi cha Meza Huru Leo kupitia ITV mada ikiwa zoezi la ukaguzi magari linaloendelea nchini, bahati mbaya nilikosa muda wa kuchangia pale studio kwa njia ya simu.

Nimestuka kuona ile gari pale Oysterbay iliokosa stika mpaka ibadilishwe tairi ikitajwa kua life span ya tairi ni miaka minne tu, na zile tairi kwa macho zilionekana poa tu.

Ni kweli kiusalama, lakini nimejaribu angalia hali ya uchumi wa nchi yetu kwa wananchi walio wengi uwezo wa kubadili tairi zote ambazo ki machoni ziko salama naona litakua shida, shida ikizingatiwa mazoea watu tumetumia tairi kuu kuu kwa miaka mingi tu bila shida.

Changamoto- Nikienda dukani ntazipata tairi zilizotengenezwa tarehe ya juzi au za mwezi uliopita? Pengine hata maduka ya tairi mjini wanauza tairi kwa speed ndogo hivyo kuna uwezekano zikawepo tairi zenye tarehe za nyuma au hata zilizopitisha umri wake wa kutumia.

Ushauri kwa Jeshi la Polisi wajaribu pia kupitia stock za wauzaji wa jumla na reja reja kuangalia tarehe za muda wa matumizi ya tairi zikiwa madukani kwao kabla ya mtumiaji wa mwisho kununua, sababu waweza ends nunua tairi kisha kwa life span yake ikawa bado miezi 6 hiyo itakua hasara.

Mamlaka ifuatilie hilo.
 
Dr Guitar tz
Lakini mkuu jamaa kuambiwa abadili tairi je ni kwa usalama wa askari au kwa usalama wa mwenye chombo? Huoni unaweza ukawa kasi lakini tairi likabust wakati ni jipya? Basi jibu ndo hilo wakuta life span yake imefika na material yaliyotengenezea yashaexpire. So vitu vingine tusiwe tunabisha bali tuwe tunaelewa na kuchukua kama fundisho.

Tukienda madukani ni wajibu wetu kuhakikisha matairi tunayochukua ni sahii na bado life span yake haijakwisha...

HILI NI KWAAJILI YA USALAMA WAKO PAMOJA NA WANAOTUMIA BARABARA WENGINE
 
Upo sahihi lakini kibongo bongo mhm shughuli itakuwepo kwenye hili...
Halafu athari ya used tyre tena kwa safari za mijini risk yake nadhani Ipo 0.03%...Ki uzoefu ktk miaka 10 hapa mjini Dar sikuwahi sikia Gari imepata ajali mbaya kwa burst ya tyre..ingawa huenda zimetokea
 
Mkuu tujuze wanakagua ninihasa
Wanafungua Bonet wanaangalia kama kuna leakage yeyote,Plastic insulator ya battery terminal upande wa (+)kile Ki plastic chekundu,pia wana angalia mifumo ya breki,spring mneso,tyres,uonekano nzima wa body Na pengine vingine vya kawaida,taa,vioo,indicators,wipers nk
 
There is always a shortcut to all that mess.
 
Pamoja na uzuri wa hili zoezi mimi kwangu nililitilia shaka, uzuri wa gari ni kwa maono ya askari wa usalama barabarani ambaye sina uhakika kama ana taaluma husika ni ka zoezi kenye harufu ya rushwa tu haka
 
Expy date ya tairi huonyeshwa kwa namba 4. Namba mbili za mwanzo ni week iliotengenezwa na namba mbili za mwisho ni mwaka iliotengenezwa. Na kimfano ukikuta imeandikwa 2209 ina somwa hivi... Kwamba imetengenezwa week ya 22 ya mwaka 2009. Sasa ili kujua inaexpy lini inabidi ujumlishe miaka mi4 ijayo. Kwa mfano huohuo hii tairi itexpy 2213.
Angalia zaidi hapa
images%20(2).jpeg
images%20(1).jpeg
 
KUNA MAADISHICKATIKACTAIRI YANAYOHESHA MWISHO WA KUTUMIKA.WANAOELEWA HUMU NAOMBA WATUELE!EZE. TBS KAMA HII NI KWELI MBONA WASIINGIE KWA WAZAJII ?
Matairi karibu yote USED yame expire lakini yanauzwa Magomeni na Kariakoo peupe. Serikali inaliona hili lkn wanasubiri wanyonge barabarani. TRA wamejaa kariakoo wanadai risiti tu. Traffik nao wamenona mattakko utafikiri mapipa ya mavvi wanaota rushwa tu
 
Hiyo ya juu imetengenezwa week ya 9 ya mwaka 2007. Maisha yake ni miaka 4 itaexpy 0911.

Ya chini imetengenezwa week ya 29 ya mwaka 2010.
Kwenye tair panakuwa na maelezo yote, speed inayotakiwa, upepo unaotakiwa, uelekeo, uzito wa kubeba ukubwa na kila kinachoihusu hiyo tairi. Na kama sikosei size ya tairi inayotakiwa kufungwa kwenye gari huonyeshwa ktk mkanda wa dereva. Tuwe makini jamani uswahilini watu hubadlisha size za tairi ktk gari labda kwa kutaka yapendeze lakini hawajali gari liliundwa litumie size gani! Matokeo yake gari inakuwa unstable hupelekea ajali zisizoeleweka!
 
Back
Top Bottom