DOKEZO PreGE2025 Responded Zoezi la Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Dar) halizingatii utambuzi wa wanaojiandikisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
122
Reaction score
111
Leo Machi 17, 2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeanza rasmi zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Nikiwa Mdau wa demokrasia nimefanya ufuatiliaji mdogo kwa siku hii ya kwanza kwa kutembelea vituo takribani 10 ambavyo vinapatikana katika Kata ya Kawe pamoja na Kata ya Mbezi Juu, pamoja Kinzudi.

Licha ya mambo mbalimbali ambayo nimebaini huku mengine nikiwa nimejipa muda wa kuendelea kuyafuatilia, nimebaini changamoto moja ambayo inaweza kuibua migogoro siku za mbeleni hasa kipindi cha uchaguzi.
photo_2025-03-17_15-02-19.jpg

photo_2025-03-17_15-02-40.jpg
Kwa kuzingatia miongozo maalumu ambayo imebandikwa kwenye vituo, inaeleza moja ya kipengele kinaeleza kwamba "Mawakala wa Vyama vya Siasa watashirikiana na Mwandishi Msaidizi kuwatambua Wananchi wanaokuja kujiandikisha au kuboresha taarifa zao."

Katika udadisi wangu katika vituo takribani 10 ambavyo nimefanikiwa kuvifikia na kuweka kambi kwa muda, nimebaini changamoto ya kutozingatiwa kwa umuhimu wa kutambua wananchi wanaofika kujiandikisha au kuboresha taarifa zao.

Katika vituo vingi nilivyofanikiwa kufika kuna Wakala wa Chama kimoja (CCM), hata hivyo mchakato wa utambuzi haufanyiki badala yake Mwananchi anafika anaingia kwenye foleni na kuendelea na michakato mingine ya kujiandikisha au kuboresha taarifa.

Hata hivyo suala hili limeniachia maswali, ambapo najiuliza Je, suala la utambuzi halina msingi au umuhimu inapotokea vyama vya siasa vimeacha au vimeshindwa kuweka mawakala.
photo_2025-03-17_15-02-43.jpg

photo_2025-03-17_15-03-05.jpg
Ili kuepuka malalamiko kwa Tume juu ya kuwepo kwa wapiga kura feki au wasio na sifa kama ambavyo imekuwa ikitajwa, je, Tume imeshindwa kusisitiza uzingatiaji wa zoezi la utambuzi kabla ya wananchi kuendelea na hatua nyingine?

Kwa aina ya mazingira yaliyopo ni rahisi kujipenyeza au kupenyezwa kwa kundi la watu wasio na sifa jambo ambalo linaweza kuleta utata na kasoro wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo itakumbukwa Mwenyekiti wa INEC, alitangaza kwamba Watu watakaojiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura watachukuliwa hatua za kisheria, hoja hii pia inaibua wasiwasi juu ya ubora wa mfumo hasa baada ya kuona zoezi la utambuzi halizingatiwi ipasavyo.

Wito wangu kwa INEC ni vyema suala la utambuzi likasisitizwa na likapewa umuhimu. Lakini wito wangu mwingine nauelekeza kwa wadau ikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kufuatilia kwa ukaribu namna zoezi la utambuzi linaweza kufanyika kwa haki licha ya kukosekana kwa mawakala wa Vyama mbalimbali vya siasa.

Pia soma ~ INEC: Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi au ambaye atafikisha umri huo siku ya uchaguzi ndiye anatakiwa kujiandikisha
 
Leo Machi 17, 2025 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeanza rasmi zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Nikiwa Mdau wa demokrasia nimefanya ufuatiliaji mdogo kwa siku hii ya kwanza kwa kutembelea vituo takribani 10 ambavyo vinapatikana katika Kata ya Kawe pamoja na Kata ya Mbezi Juu, pamoja Kinzudi

Licha ya mambo mbalimbali ambayo nimebaini huku mengine nikiwa nimejipa muda wa kuendelea kuyafuatilia, nimebaini changamoto moja ambayo inaweza kuibua migogoro siku za mbeleni hasa kipindi cha uchaguzi.

Kwa kuzingatia miongozo maalumu ambayo imebandikwa kwenye vituo, inaeleza moja ya kipengele kinaeleza kwamba "Mawakala wa Vyama vya Siasa watashirikiana na Mwandishi Msaidizi kuwatambua Wananchi wanaokuja kujiandikisha au kuboresha taarifa zao."

Katika udadisi wangu katika vituo takribani 10 ambavyo nimefanikiwa kuvifikia na kuweka kambi kwa muda, nimebaini changamoto ya kutozingatiwa kwa umuhimu wa kutambua wananchi wanaofika kujiandikisha au kuboresha taarifa zao.

Katika vituo vingi nilivyofanikiwa kufika kuna Wakala wa Chama kimoja (CCM), hata hivyo mchakato wa utambuzi haufanyiki badala yake Mwananchi anafika anaingia kwenye foleni na kuendelea na michakato mingine ya kujiandikisha au kuboresha taarifa.

Hata hivyo suala hili limeniachia maswali, ambapo najiuliza Je, suala la utambuzi halina msingi au umuhimu inapotokea vyama vya siasa vimeacha au vimeshindwa kuweka mawakala.

Ili kuepuka malalamiko kwa Tume juu ya kuwepo kwa wapiga kura feki au wasio na sifa kama ambavyo imekuwa ikitajwa, je, Tume imeshindwa kusisitiza uzingatiaji wa zoezi la utambuzi kabla ya wananchi kuendelea na hatua nyingine?

Kwa aina ya mazingira yaliyopo ni rahisi kujipenyeza au kupenyezwa kwa kundi la watu wasio na sifa jambo ambalo linaweza kuleta utata na kasoro wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo itakumbukwa Mwenyekiti wa INEC, alitangaza kwamba Watu watakaojiandikisha zaidi ya mara moja watachukuliwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura watachukuliwa hatua za kisheria, hoja hii pia inaibua wasiwasi juu ya ubora wa mfumo hasa baada ya kuona zoezi la utambuzi halizingatiwi ipasavyo.

Wito wangu kwa INEC ni vyema suala la utambuzi likasisitizwa na likapewa umuhimu. Lakini wito wangu mwingine nauelekeza kwa wadau ikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kufuatilia kwa ukaribu namna zoezi la utambuzi linaweza kufanyika kwa haki licha ya kukosekana kwa mawakala wa Vyama mbalimbali vya siasa.
Mawakala wa vyama wanagharamiwa posho na vyakula na vyama vyao, Nec haiusiki nao.

Kama hujaona mawakala wa vyama vya upinzani hilo ni tatizo lao siyo tatizo la Nec wala Ccm.

Na kuhusu wizi wa kura wala haufanyiki kwa kupenyeza kujiandikisha zaidi ya mara moja, haiko hivyo.

Chama chochote makini kikiwa makini kwenye upigaji kura na wakala akatimiza majukumu yake huwezi kufanya udanganyifu wa kura, kura zinazoibiwa ni za Urais kwenye majumuisho ya nchi nzima na hapo ndipo vinazaliwa vituo hewa.

Ndio maana unapaswa kujiuliza mbona Ukawa mwaka 2015 walichukuwa majiji yote? Kura zikipigwa ni lazima zihesabiwe na hakuna wa kupenyeza kura.
 
Back
Top Bottom