• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Ziwa Nyasa Mali Yetu Upande Wetu Tanzania

W

wamwala

Senior Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
138
Points
170
W

wamwala

Senior Member
Joined Jan 31, 2012
138 170
Ziwa Nyasa Mali Yetu Upande Wetu Tanzania
Kusuwasuwa Swali la Mipaka ya Ziwa Nyasa tumeletewa na Mkoloni Mwingereza kwa makusudi kabisa; lakini ni kosa kubwa la kutokuona mbele la League of Nations,sasa UN, iliyokubalia mipaka ya Mwingereza bila kufikiria Sheria za Kimataifa(International Laws) hata za wakati huo kuhusu maji ya asili yanayopakana na nchi za serikali mbalimbali. Wakubwa hao wote wa League of Nations walitoka katika nchi ambazo mipaka ya maji ya maziwa na mito yao ni katikati,isipokuwa bahari.

Hapo awali, makabila ya Malawi (Nyasaland,baada ya wazungu kuzungukia huko) yalijua na kutumia sehemu yao ya maji ya Ziwa Nyasa,na makabila ya Tanganyika ( German East Africa pia baada ya wazungu kuzungukazunguka bara letu) walitumia maji ya upande wao bila kuingiliana na wale wala kugombana,kila mmoja akijua tuko nusu kwa nusu,yaani mpaka ni huko katikati, kwa Sheria zamiliki zamila zetu. Aliyemegamega nchi zetu ni mzungu Mkoloni na kututenganisha pengine hata watu wa kabila moja. Mwingereza hakuipenda Tanganyika, maana alishikwa sana na Australia, New Zealand, India,na penginepo huko. Lakini Uingereza ilikubali kusimamia kampuni za Waingereza zilizofanya biashara Tanganyika, kuhusu meno ya tembo, madini,n.k.

Hivi kabla ya Vita Kuu ya Kwanza,mipaka ya Ziwa Nyasa ilikuwa katikati huku ikilindwa na Wajerumani upande wetu,na ng'ambo Nyasaland ikilindwa na Waingereza, wote wakilinda mipaka yao kwa zana za vita.
Wakati huohuo Wamisionari Waanglikani walikuwa na meli iliyoitwa Gindron(niliiona kwa macho yangu nikiwa mtoto) ikiwasafirisha wamisionari hao wakisambaza misioni zao kando ya Ziwa Nyasa kuanzia Nyasaland mpaka kisiwa Likoma, Kobwe (Mozambique),Ng'ombo (Tanganyika), Kwambe, Mbamba Bay, Ndengele, Liuli (cathedral yao,Askofu mwanzilishi amezikwa pale),Nkili, Mbaha, Saint Thomas Manda, Lituhi, n.k.kando ya ziwa.

Aliposhindwa Vita Kuu ya Kwanza Mjerumani, askari waliokuwa Nyasa walikimbia (retreat), wakazika mabomu na makombora yao katika bwawa la Ngawi,Lituhi,ili Waingereza wasiyapate na kuyatumia. Mimi mwenyewe nililiona moja lao lililetwa shuleni bila kujua na mwanafunzi mwenzetu mmoja aliyekwenda kuoga na kuvua katika bwawa lile siku hiyo; akalileta Shuleni kwetu Nkaya,(Lituhi), mwakaule 1942 -3, na akaamriwa alirudishe huko.


Aliposhindwa Mjerumani vita vile, Tanganyika yaani German East Africa, na German West Africa yaanil eo, Namibia hazikuwa na mlinzi; zikawa chini ya League of Nations, siku hizi UN. League of Nations ikatoa Namibia kwa ulinzi wa Union of South Africa, na Tanganyika ilikabidhiwa kwa Mwingereza aliyetuzunguka kwa Nyasaland Protectorate, Kenya Colony, na Uganda Protectorate, sisi tukiwa Tanganyika Mandated Territory, na Msumbiji kusini chini ya Mreno.

Ndipo lilipotokea kosa la makusudi la Uingereza, kosa lililobarikiwa na League of Nations. Mwingereza alijua sasa anaweza kuwalinda raia wake wakampuni zabiashara na kulinda misioni zaAnglikan zilizozagaa kandokando ya Ziwa Nyasa. Akabadili mipaka au mpaka waziwazi wa uliokuwa katikati na kuuweka pwani ya Nyasa ili misioni zitembelewe vizuri na kirahisi kwa meli kuzunguka ziwa; na akawawekea mipaka Wamisionari Wajerumani wa Peramiho wasisambaze misioni zao huko Nyasa ila wao wakae huko milimani. Ndio maana waAnglikani waliitwa "Wamulochi" yaani watu wa majini au wa kuzunguka ziwa, na walifanya nguvu hata za kiserikali (Governamental Influence) kushindana na Wajerumani Wakatoliki wa Peramiho kujenga kule Nyasa. Fikiria kesi au mzozo wa kwanza wa misioni ya kwanza Nyasa,LituhiwalivyopambananawaAnglikaniwa missionya Saint Thomas, Manda, ng'ambo ya mto Ruhuhu; na kesi walivyochachamaa Misioni ya Litembo kusogeza zamu yake Nyasa,Kilosa, Mbamba Bay na Litembo kuamua baadaye kujenga misioni yao mbali na Ziwa huko Nangombo,Wilaya yaMbinga, sasa wilaya ya Mbamba Bay.


Si siri kamwe; nenda na tazama mwenyewe misioni za Anglikana na za Katoliki zilivyojipanga kwa wingi wake asilia: sehemu za milimani na kando ya Ziwa Nyasa. Utaona kweli ilikuwa sababu (forensic reason) kubadili mpaka wa Ziwa Nyasa. Wote tuliliita Ziwa kilugha "Nyanja" i.e. "bahari, ziwa"; yaani sibwawa la kuchimba na jembe.

Hivi Mwingereza alijipangia mipaka kwa manufaa("convenience")yao na ya wamisionari wale wa "Wamulochi," akazoa ziwa lote kuwalinda wenzake wa dini yake kwa kuweka mpaka wa Tanganyika nje ya ziwa Nyasa. Akawakilisha mipaka mipya huko League of Nations, New York,na wao bila kumdadisi juu ya mgawanyo wazi wa unavyokuwa katika nchi zao zote Ulaya(International Laws), bila kuwa na"foresight"ya magomvi ya baadaye; wakidharau kuwa mtu mweusi hawezi na hatadai mabadiliko kulingana na international law yao ya kugawa katikati ziwa. Walithibitisha mgao na kuubariki kuwa ni wa milele na kumkabidhi Mwingereza. Walijua fika wote wawili, Uingereza na League of Nations ,kuwa utazuka ugomvi lakini hawakutaka kuona mapungufu ya busara ya mwenzao Mwingereza, na kumsahihisha; mzungu ajuae yote; tena alikuwa kati ya "the great five Powers" waliotikisa dunia katika League of Nations; tena alijua haitamhusu tena.

Tulipokomaa na kutupilia mbali kulelewa kwa kunyanyaswa na Ukoloni kwa kujinyakulia Uhuru wetu, Mtukufu Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere, aliwashitusha huko UN, alipowaambia juu ya kosa lao kwa utani wao, eti Watanzania waombe maji ya kunywa Malawi! Wakamwambia angoje Malawi itakapopata uhuru wake; ndipo basi "Mkagombane wenyewe hukohuko juu ya Ziwa Nyasa likiitwa Malawi".

Sasa wote wawili, UN na Uingereza, wanatega masikio; je, watu weusi watagawanyaje Ziwa ambalo sisi tumekwisha kuwawekea changamoto? Walijua Malawi itashukuru, kwa kosa zuri, sisi tung'ang'anie sasa Ziwa lote toka urithi "halali" wa mfadhili Mkoloni. Watanzania, je,waseme nini?UN na Mwingereza wanasema, "Tumieni Busara tuliyoipuuza sisi, irudieni busara ya wazee wenu waliojipangia bila mapigano kuwa maji ya upande wa Tanzania ni ya Watanzania; na maji ya upande wa Malawi ni ya Wamalawi kwa kuwa mpaka uko katikati. Vijana wenu watapima wenyewe hapo baadaye."


Nimejisomea vitabu kadhaa wakati nikiwa masomoni USA, katika tafiti za masomo yangu kwa ajili ya wahusika. Kitabu kimoja kimetafsiriwa toka Kijerumani na kina ramani za zamani za muda tuliposoma sisi Primary School Nkaya, Lituhi. Mpaka wa Ziwa ulikuwa katikati hadi Vita Kuu ya Pili. Ramani za baada ya Vita Kuu ya Pili zimetushangaza kuona mpaka wa Ziwa Nyasa kwetu uko ufukweni mwa ziwa na sisi hatuna tena maji yetu wenyewe ya kunywa wala ya kuoga ziwani; ila labda "bill" tulipe Malawi??!!

Iwe wazi kabisa kwa kila mmoja
kuwa hatakama dini ilichangia sababu kwa Mkoloni (si raia yoyote) kubadili mpaka huo, swala letu leo la kuweka mpaka katikati ya Ziwa Nyasa sio swala la dini kamwe, maana kuoga maji, kunywa maji na kuvua au kusafiri katika ziwa sio swala la dini, bali ni swala la haki za kibinadamu kufa na kupona (survival and economical)na za sheria za mataifa yote (International Laws).

Ni jaribio kwetu Waafrika. Mtego tumetegewa na Mkoloni kwa nia zake. Natumaini busara tulizorithi kwa wazee wetu zitumike sasa (bila kuiga vishawishi vya kikoloni), ili tufikie uamuzi wa amani na busara. Nawashukuru sana Waheshimiwa Maraisi wa nchi husika; wanalichukulia swala hili maanani kwa moyo wa kutunza uzalendo na amani kati yetu. Waheshimiwa Maraisi wote wanawatuliza raia wao kutunza amani. Wale waliotega mtego wasije wakajipongeza na kufurahia nani atamwaga damu ya raia kwa ajili ya maji ya Mungu, wakisema, "Hivi ndivyo walivyo Waafrika vita tu!"Ziwa si kisima cha kuchimba.

Alkuin Yohanes Chinguku(81)
(Baba yangu ni Mtanzania wa Mbamba Bay na mama yangu ni Mmalawi wa Ushisha).

(Ziwa liwe na majina mangapi? Nyasa upande huu na Malawi upande ule?)
 
pmwasyoke

pmwasyoke

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2010
Messages
3,857
Points
2,000
pmwasyoke

pmwasyoke

JF-Expert Member
Joined May 27, 2010
3,857 2,000
Ninaona dalili za watawala wa sasa kutafuta njia za kukwepa kulimaliza jambo hili na kuwaachia wa baadaye.

Kama walivyofanya wakina Nyerere, Banda, Mwinyi, Muluzi, Mkapa, Bingu. Uone wanavyosuasua kwenda Mahakama ya kimataifa!
 
kinja

kinja

Senior Member
Joined
Oct 10, 2010
Messages
199
Points
195
kinja

kinja

Senior Member
Joined Oct 10, 2010
199 195
nakushukuru mzee wetu kwa historia nzuri. tunaomba jina la kile kitabu nami nakiri wajerumani wanaweza kutusaidia sana kwa hili. serikali yetu itafute doc zote najua peramiho ziytapatikana
 
S

Swat

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
4,204
Points
1,250
S

Swat

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
4,204 1,250
Nadhani wajerumani watakuwa na documents ana publications kadhaa zinazoelezea kwa nini wakati waingereza wana badili mpaka kuupeleka ufukweni wao walikaa kimya!.Utakuwa ni mmojawapo wa ushahidi mzuri ukichanganywa na mwingine Vyombo vya serikali vifuatilie hili,si kukaa ofisini kupigwa na viyoyozi tu.
 
W

wamwala

Senior Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
138
Points
170
W

wamwala

Senior Member
Joined Jan 31, 2012
138 170
Nadhani wajerumani watakuwa na documents ana publications kadhaa zinazoelezea kwa nini wakati waingereza wana badili mpaka kuupeleka ufukweni wao walikaa kimya!.Utakuwa ni mmojawapo wa ushahidi mzuri ukichanganywa na mwingine Vyombo vya serikali vifuatilie hili,si kukaa ofisini kupigwa na viyoyozi tu.
Shida kubwa kwa watawala wetu ni kwamba hawahitaji kabisa kuumiza vichwa. minimekutana na huyu mzee kanipa simulizi nyingi sana. na ana ramani ya Malawi kabla ya vita ya pili ya dunia ana vielelezo vingi sana. Ameshapeleka kwa RC. Ruvuma bt document hizo zote wamezikalia hawahitaji hata kuzifwatilia
 

Forum statistics

Threads 1,405,579
Members 532,041
Posts 34,489,721
Top