Baada ya kufunga anga, jeshi la Congo lilibaki na njia tu ya maji. Kumbuka liliombwa kujisalimosha ndani ya masaa 48. Halikutekeleza. Ndipo M23 ikafunga njia ya maji, na kulivaa jiji. Taarifa zilizokuwepo ni kwamba hata kabla ya hayo masaa, tayari ilikuwa mjini, ndipo Monusco ikaamua tu itoe watu wake.
Baada ya kuona wamezingilwa bila utani na njia pekee iliyobaki, jeshi la DRC likapelea siraha kwa MONUSCO. Wanajeshi waliambiwa tatizo lipo kati ya M23 na serikali, siyo jeshi. Hivyo, wakiweka siraha chini, wamehakikishiwa usalama wao. Japo wachache wale makomando wa DRC, wamejaribu kuendeleza mapigano, lakini haikuzaa matunda. Movie ikawa ndo imeisha hivyo Kivu kaskazini. Inaelekea vita vinahamia Kivu kusini sasa. Stay tuned.