VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Ukiendelea hivi hautafanikiwa kamwe. Hautafika mbali.Utaishia njiani. Hutapata utakacho. Tafadhali tafuta Mshauri wako mbobezi wa mambo ya kisiasa ili awe anakushauri kabla ya kuamua. Bado hujitoshelezi kisiasa. Kweli kabisa. Labda kiuchumi-kwakuwa nawe ni mchumi.
Katika Mkutano wenu na Waandishi wa Habari juzi,hukupaswa kutaja tuhuma zote zilizojadiliwa ndani ya Kamati Kuu. Kutaja tuhuma zile ni kutoa siri za vikao nje na kujitetea pasipostahili. Sasa ulipojibu pale tuhuma moja baada ya nyingine ulikuwa unamjibu nani? Ili iweje? Kwa ajili ya kumbukumbu gani?
Ndugu Zitto, yawezekana unachokiamini kuwa una uwezo wa kuongoza chochote popote hapa nchini ni kweli. Lakini,imani yako isikuendeshe. Nenda nayo taratibu. Utafika tu! Ukiruhusu machagizo ya vyombo vya habari kukukimbiza mbio kuelekea unapopataka,utajikwaa;utaanguka na kuumia.
Siku ile, ungesema hivi tu: " Nayaheshimu Maamuzi ya chama changu. Nitayamaliza mambo haya kwa mujibu wa Katika na Kanuni za chama changu. Na kwasasa, sina mpango wa kuhama toka CHADEMA.Hatoki mtu hapa." Basi.Ungesubiri maswali na halafu uyajibu. Hapo, ungepata wasaa mzuri wa kuelezea kwa makini na uangalifu mkubwa mambo yako. Watu wangeshangaa.Wangekusifu. Kukosekana kwa Mshauri kumekufanya uongee mengi yenyemshiko haba.
Itoshe kusema kuwa, Zitto Zuberi Kabwe ni mwanasiasa. Bado yuko safarini.Safari ya mafanikio zaidi. Lakini,anapaswa kuwa makini.Aongee kwa kuchagua maneno;kuzingatia hadhira na kuuchuja ujumbe. Achangamane na wenzake chamani. Wawe kitu kimoja. Wasonge mbele. Lakini, Mshauri hakwepeki. Shauriwa kwanza;amua baadaye.
Kila la kheri katika siku zako 14 za utetezi. Yatakwisha tu haya. Wajibu waliokutuhumu. Sisi tunasubiri matokeo tu.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam