Zitto: Waitara unazungumzia kumwona Lissu, wewe ulienda lini? Wabunge kila siku wana kesi za kupigania haki, hivi wauaji unaenda kushirikiana nao?

Tatizo mmeambiwa ni uenyekiti wa chadema. Kama mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti mtegemee makubwa zaidi. Haki ya Mungu atabaki yeye na .tei wake asipangalia.
 
mbunge wa kigoma zitto kabwe kwa tiketi ya ACT wazalendo ameamua kutumia ukurasa wake wa twitter kumwambia maneno mazito aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya CHADEMA ndugu MWITA WAITARA huku akimwambia alichokifanya si jambo nzuri hata kidogo maneno hayo yanasomeka kama ifuatavyo..

"Mbunge mwenzio yupo hospitali mwaka sasa kwa majeraha ya risasi kufuatia jaribio la kumwua. Viongozi wa Chama chako Karibu wote Ngazi ya Taifa wana kesi inayohatarisha kuwaweka jela. Watu wanauwawa na kupotea kila siku. Halafu unajiunga na hao wanaosababisha hayo? Kweli Mwita?"

zitto kabwe!
Nonsense!!! Wacha mbwembwe katimiza matakwa yake kikatiba si nyienyie mnalalmika kuwa hampewi uhuru... Watu wakifanya wanachotaka mnalalamika teeena au uhuru wa kujieleza na maamzi kumbe n kusimama majukwaaani tu et
 
Kubwa la WANAFIKI katika ubora wake !! Mbona na yeye yuko NJIANI haifiki November atazisifia zile Bombardier 2 zinazokuja na atatangaza kujiunga siasa za HAPA KAZI TU, kama mnabisha. SUBIRINI !
Kwa iyo bombardier zisisifiwe
 
CCM Ilikataa baadhi ya Maombi ya walIotaka kujiunga CCM HUenda ndio chanzo Cha hasira Za Zitto
 
Siasa haihitaji hasira. Zito atulie tu maana kila mtu anajua namna gani afanye kuridhisha nafsi yake na namna gani atailisha familia yake..Chadema humo ndani wanamambo mazito sana ni vile wengine hamjui.

Katumia haki yake kikatiba kuhama na nisawa tu. Waliotaka kumtoa lissu SIYO SISIEMU NARUDIA SIYO SISIEMU

MUDA UTASEMA.
Umeongea yale akili yako inapofikia mwisho wa kufikiri!!
 
Zitto inaonekana una ushahidi usiotia shaka kuwa hao alionde kujiunga nao Mh. Waitara ndio wahusika. Kama ni hivyo unaonaje ukasadia kutoa huo ushahidi ili sheria ichukue mkondo wake? Halafu unapozungumzia kesi, hivi unataka kutuambia kuwa kile kilichozungumzwa na Mbowe wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi kilikuwa sahihi na hakikuvunja sheria za nchi? Au hili nalo unaliona gumu kulisema. Au unajifanya kusahau kuhusu hiyo hotuba? Basi kwa kukusaidia tu hebu isikilize hii hotuba halafu urudi twitter ukaangalie ulichokiandika. Hivi mkishikaga hizo nafasi huwa mnaona sisi wananchi hatujui chochote kuhusu sheria za nchi? Jifunzeni kufanya siasa zinazofuata misingi, kanuni na sheria za nchi.
 
Siasa haihitaji hasira. Zito atulie tu maana kila mtu anajua namna gani afanye kuridhisha nafsi yake na namna gani atailisha familia yake..Chadema humo ndani wanamambo mazito sana ni vile wengine hamjui.

Katumia haki yake kikatiba kuhama na nisawa tu. Waliotaka kumtoa lissu SIYO SISIEMU NARUDIA SIYO SISIEMU

MUDA UTASEMA.
Dah, basi rudisheni cctv camera, mbona mmeziondoa kimya kimya, na matibabu mmegoma kulipa mpaka michango.
 
kama nyinyi mnaona kumuona Lisu Ni hija wengine wanamuona jamaa yenu pimbi tu
 
Back
Top Bottom