Zitto, wabunge 50 uliosema watahamia ACT - Wazalendo wako wapi?

Zitto, wabunge 50 uliosema watahamia ACT - Wazalendo wako wapi?

Wabunge 50 unafikiri ni mchezo kuwapa. Ni kazi kuliko unavyodhani. Hadi swahiba wake Affi kamkimbia dogo.
 
Bwana ZZK kuna watu wanakuamini sana wewe na kauli zako. Sasa kama kweli ulilisema hili ni vema ukalitolea ufafanuzi
 
Tehe tehe..jamaa kapotezwa vibaya.

Mradi wa kuvuta pesa toka gambani umeota mbawa
 
huyu msariti ni msema ovyo mara majina ya uswiz mara wabunge.Zzk ni msanii na msariti
 
Kiongozi mkuu au baba wa ACT alisema wabunge 50 WA vyama mbali mbali watahamia kwenye chama cha act mpaka sasa hatujawaona au ndo kauziwa kekundu

Wanaomwamini ndio wajue kuwa mtu wao ni mlopokaji
 
Ni wachache tu wenye moyo wa kuhamia kwenye tuvyama tudogotudogo, hivi hamkumsikia mkosamali?
 
Kachama kenye Lowassa na Mwigulu wamekatosa..nasikia amemwambia akafute arudi CHADEMA
 
hata lowasa kagoma kujiunga nao pamoja na wao kumtaka
 
wamempiga chenga na sasa ona washachukua form, kwenda kwenye usaliti dot com sio mchezo yahe!!!
 
Toka lini zitto akaaminika? Alisema atataja majina ya waficha fedha uswiss, hakutaja.
Hao wabunge 50 hatakaa apate, hata robo yake.
 
Kwa hiyo wakishahamia huko automatically wanakuwa wabunge? upuuzi wa Lumumba bana!
Mkuu usiconclude kwa kuniita Mlumumba unanipa sifa nisiyoipenda.Mkuu angalia kwa jicho la tatu hawa wanaohama mwishoni.Hawa hawa walisema Ndiyoooooo kwenye katiba pendekezwa,wakaja kwenye mswada wa gesi wakasema ndiyoooooo,ila sasa hivi wamebaki wao kwa wao CCM,Wale wenye hofu ya kukatwa na chama chao au watakaokatwa watakimbilia upinzani.Kwa mfano wakija Chadema wakakosa nafasi hawahawa watahamia kwingine.Huku Upinzani nafasi wapewe kwanza wale waliosotea kwa kupigwa mabomu then waje hawa wahamiaji
 
Bwana ZZK kuna watu wanakuamini sana wewe na kauli zako. Sasa kama kweli ulilisema hili ni vema ukalitolea



Hakuna kiongozi anayeweza kufikia levo ya zitto pale ufipa ogopa mtu mwenye uwezo wa kubeba chama cha siasa mpaka kikawa na nguvu sio mchezo sasa ngojeni arudi bungeni ndio mtamjua ni nani wote mtaonekana wachumia tumbo uzuri wa watanzania wanaamini wanachokiona hawezi waletea mboyoyo huku kazi haionekani
 
Kwa mtamzamo wangu naona zito anajutia sana uamuzi wake, lakini anchojutia zaidi sio kitendo cha kutoka chadema bali kule alipoamua kuelekea baada ya kutoka chadema. Hapo ndipo alikosea sanaa, inaonekana mpaka sasa mambo mengi hayaendi kama vile alivyotaraji kwamaana umaharufu wake umebaki kuwa wa kawaida na nguvu ya chadema imezidi kuwa kubwa ata kuliko kipindi alichokuwepo (pengo lake halionekani) lakini kama angeamua kutoka na kuelekea kwa ccm waziwazi, hapo chadema ingeonja joto ya jiwe. Pole sana bwana zito kwa kuchanga karata zako vibaya
 
Back
Top Bottom