Zitto: Usipoongoza, utaongozwa

Zitto: Usipoongoza, utaongozwa

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,486
Reaction score
68,288
Nimeona mahala Ndg. Zitto Kabwe Kiongozi wa ACT Wazalendo anasisitiza matumizi ya hiyo kauli yake hapo juu.

Nikajiuliza, hii kauli ina mantiki ndani yake? imebeba maana kamili ya ujumbe mzima unaotakiwa ili itimie kwa kufuata sheria za nchi? au ni kauli tu ya mtu anayeonesha yupo tayari kuwa madarakani kwa mbinu zozote ilimradi aendelee kuwepo.

Tujiulize, unaongoza au kuongozwa kwa namna gani? ni kwa kufuata sheria za nchi, na kiongozi halali ni yule aliyepatikana kwa kuheshimu maamuzi ya wananchi/katiba lakini akiwa madarakani atende kulingana na sheria za nchi.

Lakini kwangu kusema tu usipoongoza utaongozwa, hii kauli kwanza inachochea vurugu, kwasababu kama wote tukilazimisha kuongoza nani ataongozwa? inafahamika wazi kwenye uchaguzi wowote, chama kinachounda serikali ni kimoja, sasa huyo mwingine aliyeshindwa atamuongoza nani?

Lakini zaidi, hii kauli inaficha uozo wa watawala, tusilazimishe wote kuongoza bila kujali kama misingi ya uongozi ipo, lazima kila anayetuongoza tuone anafuata taratibu, na asipozifuata, muhimu akumbushwe, kuliko wote kuwa na mawazo ya kibinafsi ya kuongoza pekee.

Pia, mbaya zaidi, hii kauli inachochea ubinafsi, kama wote tukiwa na mawazo ya aina hii, basi ni rahisi kila mmoja wetu kugombania kuongoza hata kama anakiuka taratibu na sheria za uchaguzi.

Na hili ndilo linasababisha kila siku pawepo na maridhiano Zanzibar yasiyotekelezeka, au yanayoishia utekelezaji wake pale uchaguzi mkuu unappfanyika, kwani kila mmoja hurudia tabia yake ya kutaka kushinda kwa njia zozote hata haramu, mwishowe kuwaumiza wananchi wasio na hatia hasa wapemba.

Hii kauli ya Zitto inafaa kukemewa.
 
Nimeona mahala Ndg. Zitto Kabwe Kiongozi wa ACT Wazalendo anasisitiza matumizi ya hiyo kauli yako hapo juu.

Nikajiuliza, hii kauli ina mantiki ndani yake? imebeba maana kamili ya ujumbe mzima unaotakiwa ili itimie kwa kufuata sheria za nchi? au ni kauli tu ya mtu anayeonesha yupo tayari kuwa madarakani kwa mbinu zozote ilimradi aendelee kuwepo.

Tujiulize, unaongoza au kuongozwa kwa namna gani? ni kwa kufuata sheria za nchi, na kiongozi halali ni yule aliyepatikana kwa kuheshimu maamuzi ya wananchi/katiba lakini akiwa madarakani atende kulingana na sheria za nchi.

Lakini kwangu kusema tu usipoongoza utaongozwa, hii kauli kwanza inachochea vurugu, kwasababu kama wote tukilazimisha kuongoza nani ataongozwa? inafahamika wazi kwenye uchaguzi wowote, chama kinachounda serikali ni kimoja, sasa huyo mwingine aliyeshindwa atamuongoza nani?

Lakini zaidi, hii kauli inaficha uozo wa watawala, tusilazimishe wote kuongoza bila kujali kama misingi ya uongozi ipo, lazima kila anayetuongoza tuone anafuata taratibu, na asipozifuata, muhimu akumbushwe, kuliko wote kuwa na mawazo ya kibinafsi ya kuongoza pekee.

Pia, mbaya zaidi, hii kauli inachochea ubinafsi, kama wote tukiwa na mawazo ya aina hii, basi ni rahisi kila mmoja wetu kugombania kuongoza hata kama anakiuka taratibu na sheria za uchaguzi.

Na hili ndilo linasababisha kila siku pawepo na maridhiano Zanzibar yasiyotekelezeka, au yanayoishia utekelezaji wake pale uchaguzi mkuu unappfanyika, kwani kila mmoja hurudia tabia yake ya kutaka kushinda kwa njia zozote hata haramu, mwishowe kuwaumiza wananchi wasio na hatia.

Hii kauli ya Zitto inafaa kukemewa.
Hilo ni dongo kwa wanaoogozwa kibabe pale ufipa kwa wachaga

USSR
 
😁😁😁
AMEsY_.jpg
 
Zitto bado ana kinyongo na CHADEMA tangu 2011 alipoukosa uenyekiti na mengine yote yaliyofuata baada ya hapo.. Lakini licha ya hayo hana misheni kubwa kisiasa zaidi ya hapo alipo.. Anachofanya ni moderate politics ili maisha yasonge na kutengeneza shekeli kupitia siasa kila inapowezekana, na ndio maana tangu uchaguzi uishe hakuna juhudi zozote zimefanyika kukikuza chama chake
 
Naangalia vijana wanavolialia na maisha, ukiangalia kwa undani negotiaon skills ziko chini sana,
We need to put this into our curriculums.
 
Mi nilishamtoaga maana Zitto toka wakati ule yupo chadema, alipokuwa anashirikiana na usalama wa taifa ( Jack Zoka) kuihujumu chadema...wakawa wanamuwekea hela kwenye akaunti zake. Kifupi Mimi wanasiasa wanaotoka kabila la waha, sitaki kuwasikia kabisa....Zitto, Kafulila, Machalii, Kaborou...Rubbish!
 
Zitto bado ana kinyongo na CHADEMA tangu 2011 alipoukosa uenyekiti na mengine yote yaliyofuata baada ya hapo.. Lakini licha ya hayo hana misheni kubwa kisiasa zaidi ya hapo alipo.. Anachofanya ni moderate politics ili maisha yasonge na kutengeneza shekeli kupitia siasa kila inapowezekana, na ndio maana tangu uchaguzi uishe hakuna juhudi zozote zimefanyika kukikuza chama chake
Simply ni mwanasiasa wa kufuata upepo asiyejali future na well being ya wapiga kura wake.
 
Zitto anapambana sana kuonekana yeye na chama chake ndiye vinara wa upinzani nchini ila namba haziko upande wao.
Bahati mbaya zaidi anapambana kwa kujipendekeza kwa CCM, bila kujali uvunjifu wa sheria wanaofanya.
 
Back
Top Bottom