Zitto, ungana na wapinzani wenzako...

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Pale anapotokea adui mkubwa, adui wadogo huungana kupambana nae, tujikumbushe wakati wa ukoloni ambapo baadhi ya makabila na jamii hasimu ziliungana kwa ajili ya kupambana na wakoloni, waliweka tofauti zao pembeni na kwa nia moja wakapambana na ukoloni.

Hivi sasa tunashuhudia katika nchi yetu ombwe la kiungozi, tunashuhudia ubinyaji mkubwa wa demokrasia, uvunjaji wa wazi wa katiba yetu, uonevu kwa watumishi wa umma, lakini tunashuhudia kiongozi anaeongoza kwa jazba, hasira, na chuki kubwa, ni wakati wa upinzani kutengeneza Muungano mkubwa wenye nguvu kwa ajili ya kumwondoa mtu huyu.

Zitto wala usiogope kwenye siasa hakuna aibu, wala hamna adui wa kudumu, ni wakati sasa wakuunganisha nguvu na vyama vingine vinavyounda umoja wa ukawa, ili muweze kuwa na sauti moja kupambana na mtu huyu, pasipo kufanya hivyo vyama vya upinzani mtafutika mtafutwa kwa njia zozote zile, kumbukeni teuzi za makada kwenye nafasi mbalimbali za uongozi zina maana kubwa sana, unganeni kupigania demokrasia, msikubali kumuachia huyu mtu nafasi ya kuwajaribu, mkikubali kujaribiwa mmekwisha .
 
Ni kweli wakati umefika wa kuweka tofauti zetu za itikadi na vyama pembeni kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa
 
Hivi bado kuna mdudu anaitwa UKAWA??,hizi mbio za madiwani mbona kila mtu kaweka kichwa chake?..
 
Tatizo akija UKAWA atataka aanze kujiona ye ndio Alwatan lkn pia huyu sio mtu wa kuaminika aisee.Ye aendelee kupiga Jalamba huko huko ACT,then UKAWA itampa support atakayohitaji akiwa huko huko ACT full stop.
 
Tuzungumzie habar ya Lemma..we don't trust Zzk..and we don't need him..nowadays he's lyk toothless dog..
Alipoteza kura zetu kazaa za ukawa kipindi cha kampeni.2015.alisababisha mbabe Kafulila asilud mjengoni shaur ya figisu zake na ccm
Lkn what we say Aluta continue
RIP Mawazo..we will remember ur great effort
 
Tuzungumzie habar ya Lemma..we don't trust Zzk..and we don't need him..nowadays he's lyk toothless dog..
Alipoteza kura zetu kazaa za ukawa kipindi cha kampeni.2015.alisababisha mbabe Kafulila asilud mjengoni shaur ya figisu zake na ccm
Lkn what we say Aluta continue
RIP Mawazo..we will remember ur great effort
Alipoteza kura zenu kivipi?!
 
Na mimi wa Majita

Nimesoma post hapa kuwa Zito Kabwe anataka kupeleka hoja bungeni ili ipigwe KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS na kaongeza Kwa kusema wabunge wa upinzani wakiopo now bungeni akidi inatimia na kura za wabunge wa upinzani zinatosha kukamilisha kazi hiyo. Mimi naona hapa ni kupoteza Muda kwani aina ya SPIKA na NAIBU SPIKA hiyo hoja itatupwa kapuni.

NINI KIFANYIKE?

Kuelekea uchaguzi mkuu 2020 Zito na chama chake waunganishe nguvu Kwa kuacha tofauti zao na kuungana Pamoja kuungana muungano wa vyama vya upinzani Kwa kutumia Jina la UKAWA au libuniwe Jina tofauti na UKAWA. Kwa kufanya hivyo ndipo nitaona ni ya dhati ya Zito katika kulisaidia Taifa na mkwamo wa kiuongozi (utawala).

Nawasilisha hoja.
 
Mnafiki tu huyo, yeye ana sababu zake Binafsi za Kumchukia Magufuli, sasa hivi kapata loop holes za kupitisha malengo yake,
siku ile ya raisi kulihutubia Bunge, wabunge wote wa UKAWA walifukuzwa yeye akabakia na Raisi akamsifia kuwa ni mwanasiasa mkomavu na yeye akabaki kukenua meno tu

Wenzie walishayaona Mapungufu ya JPM yeye akuyaona?, iweje leo umshauri aingie kwenye huo UKAWA?
 
Hahaha! wazee wa makapi#wazee wa kubadilishia gia angani ... mrudisheni na dk. basi aje awaongezee nguvu!
 
Back
Top Bottom