Mfalme wa Genge
Senior Member
- Mar 30, 2018
- 190
- 224
Zitto Kabwe kweli unachekesha, nadhani unakumbuka vizuri kilichokufukuzisha CHADEMA. Haishangazi sana kukuona unashabikia waraka wa hawa wazee Makamba na Kinana sababu wewe ni bingwa wa usaliti na unafiki umekomaa ndani yako.
Labda nikukumbushe kidogo kama umesahau au kama ulikuwa unafikiri watu hawajui kuwa CHADEMA ilikufukuza sababu ya waraka ulioandika wewe na kikundi ulichotengeneza na kujiita MTANDAO WA USHINDI. Wewe ukiwa kiongozi mkubwa (Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA) uliandika waraka wenye jina la MABADILIKO 2013 ambao mlifanya siri lakini ukaja kugundulika ndani ya chama. Nakumbuka baada ya wewe na kundi lako kujua waraka umeonekana jinsi ulivyokuwa unatapatapa na kijasho chembamba kikikutoka hasa mlipoitwa na Kamati Kuu.
Uliomba kujiuzulu nafasi yako lakini Kamati Kuu ya chama chetu ilikukatalia kwa kuwa kwa nafasi uliyokuwa nayo hasa ukiijua vizuri katiba, kanuni na taratibu za chama hukupaswa kufanya ulichofanya. Kamati Kuu ilikukatalia kujiuzulu ikadai kuwa itakuwa imekupa heshima sana kwa tendo ulilofanya. Kamati Kuu ilikwambia umefanya tukio zito sana ambalo halisameheki la UHAINI kwani ulikuwa na nia ya kukigawa na kukisambaratisha chama.
Sasa kinachonishangaza ni wewe kurukaruka kama popcorn kwenye kikaangio huku umeshupaza shingo kushabikia hawa wazee wa CCM kuwa walichofanya ni sahihi. UHAINI waliouona CHADEMA kwako ni sawa na UHAINI unaofanywa sasa na wazee hawa kwa CCM.
Na kama CHADEMA walivyochukua hatua za haraka kukinusuru chama kwa kukufukuza mimi nashauri CCM pia ichukue hatua za haraka kujitenga na hawa wazee wa busara kwani wewe na wazee wako hao nawaona kama wachawi wa maendeleo.
Na Juma Ramadhani