Zitto: Umeme wa dharura ni ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: Umeme wa dharura ni ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,020
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe akiwahutumia wananchi wa mjini Muheza mkoani Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo juzi. Picha na Edwin Mjwahuzi.

  ASEMA SH 1.7 TRILIONI ZINAZOTUMIKA KWA MWAKA ZINATOSHA KUTANDAZA BOMBA LA GESI NA KUMALIZA KABISA TATIZO.

  Boniface Meena, Muheza

  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema miradi ya umeme wa dharura inayoigharimu Serikali Sh1.7 trilioni kwa mwaka ni kichaka cha ufisadi.Akizungumza na wakazi wa Muheza katika mkutano wa hadhara juzi, Zitto alisema: "Umeme wa dharura unapendwa kwa kuwa ni eneo lililojaa ufisadi.

  Ni rahisi kufanya mikataba ya wizi katika eneo hilo. Si tumesikia wizi wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL? Dola za Marekani 56 milioni zinadaiwa kupotea, Takukuru wanachunguza."

  Kauli hiyo ya Zitto imekuja wakati tayari Bunge limeidhinisha kiasi cha Sh1.6 trilioni kwa Serikali kwa ajili ya mpango wa dharura wa kutatua tatizo la mgawo wa umeme kuanzia Agosti mwaka jana hadi Desemba mwaka huu.

  "Nilimwandikia Spika mwaka jana kumuomba aiambie kamati ya Makamba (Januari) (ya Nishati na Madini) kuchunguza ufisadi katika ununuzi wa mafuta ya IPTL lakini, mwaka unapita hakuna hatua iliyochukuliwa. Nimemkumbusha tena Spika katika mkutano uliopita lakini hajajibu. Mimi sitachoka, nitaendelea kumbughudhi Spika hadi ufisadi huo ufichuliwe."

  Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alipotafutwa jana kuthibitisha kama amepata barua ya Zitto iliyomwomba achunguze wizi kwenye baadhi ya miradi hiyo hakupatikana kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila ya kupokewa.

  Alisema hakuna sababu nyingine ya miradi hiyo zaidi ya mwendelezo wa ufisadi. Alisema fedha hizo zingetosha kama zingetumika kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ili kuondoa kabisa tatizo la umeme badala ya kutegemea umeme wa dharura.

  "Pia sehemu ya fedha hizo zingeweza kutumika katika ujenzi wa bomba jingine la gesi kutoka Kiwira hadi Dar es Salaam ambalo kwa pamoja, umeme huo ungeingizwa kwenye gridi ya taifa na kumaliza kabisa tatizo hilo."

  Alisema Serikali imewagawa Watanzania katika matabaka kwani umeme ukikatika Dar es Salaam na watu wakapiga kelele, inatikisika na kushughulikia matatizo yao haraka, lakini vijijini hata watu wakipiga kelele vipi, hawasikilizwi.

  Serikali imeamua kukalia ripoti inayothibitisha namna ufisadi unavyoliangamiza taifa: "Serikali inatakiwa kutoa ripoti hiyo ili wananchi wajue nchi yao inakoelekea na waweze kuchukua hatua haraka kuinusuru."

  Zitto alisema ni lazima wananchi wasimame kidete ili kulinda maslahi yao dhidi ya mafisadi kwa kuwa Serikali imeshindwa kufanya hivyo na kuwasababishia wananchi umasikini wa kutupwa.

  Katika mkutano huo, Zitto alisema maisha ya wananchi wa Tanzania yako hatarini kwa kuwa wale ambao ni masikini wanaotegemea kilimo wamekata tamaa kwa kukosa msaada katika sekta hiyo.

  "Kila siku mnaambiwa kilimo kimekua kwa asilimia nne, mbona haibadiliki na nyie hamshangai? Ni lazima muwe mnahoji hao wanaofaidika na kilimo ni kina nani hasa kama siyo mafisadi? Umaskini tulio nao nasisitiza wao ndiyo chanzo," alisema Zitto.

  Januari Makamba
  Makamba alipoulizwa kuhusu madai ya Zitto kumwandikia barua Spika alisema amepata nakala lakini kamati yake haijapewa maelekezo rasmi kuchunguza suala hilo.
  Alisema suala la ununuzi wa mafuta ya umeme linatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kibunge kwa kuwa haliko wazi katika mchakato wake.
  "Tatizo ni kwamba zoezi zima haliko wazi, mimi naunga mkono kuwa uchunguzi wa kibunge ufanyike na ieleweke wazi masuala ya ugavi na nani amepataje zabuni," alisema Makamba.
  Kwa upande wa gharama za kukodi mitambo ya dharura, alisema hawezi kushangazwa na matumizi ya kiasi hicho lakini akasema hana uhakika na kiasi cha fedha kwani mchakato umekuwa kwa zaidi ya miezi sita tokea Agosti 8, mwaka jana.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo. http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/20447-zitto-umeme-wa-dharura-ni-ufisadi.html
   
 2. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wakati umefika wa kulipua Transformer kuu zote za umeme.

  If a problem is ignored because of its insignificant blow it to make it Bigger.

  Lipua Transformer na Transmission line zote.
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 1,989
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Naona watu bado ni wazito kubadilika tatizo kubwa ni moja tu "Serikali ni kubwa sana". Kama tukiacha haya mashirika yawe ya serikali basi hatutapata nafuu serikali haiwezi kufanya biashara vizuri kwani hao mawaziri wanafanya uamuzi hawafanyi kibishara bali kishabiki. Kama tunataka Tanzania kuendelea ni lazima tujiulize " Ni vitu gani tutataka serikali ifanye" na vitu gani tunataka serikali ilitoe na kuruhusu kampuni binafsi. Hapa serikali ina kazi ya kulipa tu na kufanya mikataba hatuwezi kufanikiwa hivi. Tatizo ni mfumo wa serikali kubwa.


   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,441
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Zitto,
  Sasa unaanza kunipa raha!...
   
 5. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  siasa at work
   
 6. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto!
  Haya maneno kayaseme Bungeni. Kwani hamjui Tanesco ni chuma ulete ya Jakaya Mrisho Kikwete na baadhi ya majambazi ya CCM wakiongozwa na Ngeleja pamoja na Mustafa Mkullo? Hiki ni kipindi cha lala salama cha CCM na JK anataka kukomba mboga ndiyo maana hata Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco akateuliwa jambazi Robert Mboma, pamoja na wizi wa Meremeta ananapewa shirika aliongoze in short analipeleka kuzimu. In short wanachota mabilioni tena kwa staili ya kufidia mtikisiko wa uchumi wa shirika uliosababishwa na makampuni ya Rostam Aziz. Kabwe tukumbushe kule Bungeni Ngeleja aliahidi nini mbona mgao Kama kawa!
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  haa !

  Hapa mmenikumbusha kuna siku NAPE, SITTA, SENDEKA, MWAKYEMBE walifnya mkutano Mbeya moja ya mambo waliyo yazungumza ni kuwa Tanzania inampango wa kuzalisha umeme mwingi ifikapo Dec 2010 na ziada itauzwa nje mfano South Sudan wakuu nijulishelisheni vipi hizi hatua zimefikia wapi ??
   
Loading...