Zitto ulitaka bunge limchague Masha, umesahau haya maneno yako!

Hata Chadema walimtuhumu sana Masha kupitia Chamber Yake kwa Ufisadi Mkubwa wa EPA , Meremeta nk na wakamkabili Jimboni mpaka akaanguka 2010 na wakamtuhumu kwa Ubadhirifu wa Vitambulisho vya Taifa mpaka Masha Nusura alie Bungeni Enzi zile akijitetea lakin ha kushangaza Huyu Huyu Masha ndio anaonekana Mgombea bora zaid wa Chadema kwny EALA na hata alipokataliwa Bungeni akarudishwa tena!

Kama Masha ndio Mgombea bora zaid ki maadili Pamoja na Scandle zote walizotoa Chadema Wenyewe hao waliobaki huko sijui wakoje ki maadili!
Ninakubaliana na angalizo lako.

Ninashindwa pia kuelewa CHADEMA walikuwa wanatuma ujumbe gani kwa kumteua Masha mara mbili kuwa mgombea ubunge wa EALA wakati wanafahamu tuhuma zake.
 
Ulishaambiwa na Lipumba, Ufisadi wa Tanzania ni mfumo!!!

Hata hao wapiga deal anaowasema Rais ni mafisadi kiaina kwa sababu ya mfumo wetu. Kwenye huo mfumo kuna watu ambao pia ufisadi umo damuni!!

Chadema ilimtuhumu Lawrence Masha sio Waziri wa Mambo ya Ndani Bwege Wewe?

Tuhuma za Masha walizokuwa wakitoa Chadema ni Kabla ya kuwa Waziri na baada ya kuwa Waziri!

Hata Siku mkiamriwa kumpigia Deki Paul Makonda mtakuja na hoja ya 'Tatizo ni Mfumo' kwa kuwa ndio hoja aliyowapandikizia Kichwani Mbowe ili msiwe mnamhoji!
 
Hata Chadema walimtuhumu sana Masha kupitia Chamber Yake kwa Ufisadi Mkubwa wa EPA , Meremeta nk na wakamkabili Jimboni mpaka akaanguka 2010 na wakamtuhumu kwa Ubadhirifu wa Vitambulisho vya Taifa mpaka Masha Nusura alie Bungeni Enzi zile akijitetea lakin ha kushangaza Huyu Huyu Masha ndio anaonekana Mgombea bora zaid wa Chadema kwny EALA na hata alipokataliwa Bungeni akarudishwa tena!

Kama Masha ndio Mgombea bora zaid ki maadili Pamoja na Scandle zote walizotoa Chadema Wenyewe hao waliobaki huko sijui wakoje ki maadili!
Kama sio mgombea bora mnapoteza muda wa nn kumjadili humu JF?
 
Watakwambia kwenye siasa Hakuna adui au rafiki wa kudumu. Unajaribu kuleta sense kwa watu waliofilisika kabisa kihoja na kikanuni
Hii dhana ya kusema hakuna adui au rafiki wa kudumu ni kutaka kutafuta hoja ya kuhalalisha uovu/dhambi.

Shetani ni shetani tu na haiwezekani shetani akageuka kuwa rafiki katika matendo mema/mazuri.
 
Kama sio mgombea bora mnapoteza muda wa nn kumjadili humu JF?

JF sio Jukwaa la kujadili Wagombea bora pekee hata Wezi, Wauaji, Machoko na Vilaza Kama Wewe mnaweza kujadiliwa any time

Usikariri kila anajadiliwa ni kwa sababu ya Ubora wake!
 
Hata Chadema walimtuhumu sana Masha kupitia Chamber Yake kwa Ufisadi Mkubwa wa EPA , Meremeta nk na wakamkabili Jimboni mpaka akaanguka 2010 na wakamtuhumu kwa Ubadhirifu wa Vitambulisho vya Taifa mpaka Masha Nusura alie Bungeni Enzi zile akijitetea lakin ha kushangaza Huyu Huyu Masha ndio anaonekana Mgombea bora zaid wa Chadema kwny EALA na hata alipokataliwa Bungeni akarudishwa tena!

Kama Masha ndio Mgombea bora zaid ki maadili Pamoja na Scandle zote walizotoa Chadema Wenyewe hao waliobaki huko sijui wakoje ki maadili!
Kuwaelewa Chadema ni kazi ngumu, na ukiwafuatilia sana utachukia siasa, wanataka kushika dola kwa msaada wa watu ambao wao wenyewe wametuaminisha hao ndiyo mchwa wa taifa letu.
 
Kwani katika miaka tisa mtu haruhusiwi kubadilisha mawazo kutokana na mabadiliko yote yaliyotokea?

Mbona Zitto na Masha wote wamehama vyama katika hiyo miaka tisa?
 
Unafiki unaruhusiwa kwenye siasa!

Mmesahau yaliyosemwa na Lema kuhusu Lowassa?

Au mnadhani Lowassa angekuwa mgombea wa CCM ile 2015 hawa ambao leo wanamuunga mkono wangemuunga mkono wakati huo?
Mimi nadhani kimaadili unafiki hautakiwi lakini tunajaribu kuhalalisha kwa manufaa yetu binafsi.

Ninaamini siasa za kinafiki ndizo zinazokwamisha maendeleo ya haraka nchini.

Yaliyotokea katika teuzi za wagombea Urais wa Tanzania na Uchaguzi Mkuu 2015 yameonyesha ni jinsi gani wanasiasa wetu ni wanafiki.

Uchaguzi wa wabunge wa EALA kutoka upinzani ni muendelezo tu wa unafiki uliofanyika katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2015.
 
JF sio Jukwaa la kujadili Wagombea bora pekee hata Wezi, Wauaji, Machoko na Vilaza Kama Wewe mnaweza kujadiliwa any time

Usikariri kila anajadiliwa ni kwa sababu ya Ubora wake!
Asante mwalimu wa vilaza.
 
CHADEMU HAWANA MAANA SIKU MAKONDA ATAYO AMIA CHADEMA WATAMPOKEA BILA SHAKA NA ATA SAFISHWA KUWA MPYA
 
Nadhani,kwa hoja yako hii ingekuwa vizuri kama ungekuwa umeambatanisha na "kauli ya Zitto" alipoeleza kuwa anajuta kuzaliwa Tanzania kufuatia matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa EALA kutoka Chadema. Kwa wengine maneno ya Zitto hayakuwa na maana kwamba anajuta kwa sababu hawakumchagua Lawrence Masha kuwa Mbunge wa EALA, bali anajuta kwa sababu hawakujachaguliwa wabunge "wengine" badala ya waliochaguliwa. Sasa kwenye "wengine" kulikuwa na Profesa Safari, Wenje, Masha na Salum. Swali linaweza kuwa ni kwanini umemchomoa Masha na kumlisha maneno Zitto? Je, unamchukia tu Zitto au ni bahati mbaya?
Indeed, wazo lako limeendana na langu. Nakumbuka alilaumu jinsi ambavyo wameacha nguli wakachagua wachanga na lawama zake hazikuwa kwa hao tu ni kwa hata wale wa awali. Wengi ni wachanga wa mambo mazito ukilinganisha na wale ambao wamechaguliwa kwenye nchi zingine.

Wa kwetu hawataweza kustahilimi kwenye hoja nzito tusijeishia kwenye ndio mzee!!!
 
Ficha Upumbavu wako kwa vihoja vya Kipumbavu!

Chadema ilimtuhumu Lawrence Masha sio Waziri wa Mambo ya Ndani Bwege Wewe?

Tuhuma za Masha walizokuwa wakitoa Chadema ni Kabla ya kuwa Waziri na baada ya kuwa Waziri!

Hata Siku mkiamriwa kumpigia Deki Paul Makonda mtakuja na hoja ya 'Tatizo ni Mfumo' kwa kuwa ndio hoja aliyowapandikizia Kichwani Mbowe ili msiwe mnamhoji!
You idiot, I am not talking about Masha. Learn how to read and understand before you answer. That's what we're told at school .............. I am talking about people in general!!

That's was too low .................. where did I mention Masha!!?
 
..Magu aliunga mkono mchanga wenye madini kusafirishwa nje then 10+ years later anaibuka kudai tunaibiwa.

..Pia alihusika ktk dili la kifisadi la kuuza nyumba za serikali, halafu sasa hivi anadai anachukia madili.

..dili lingine ni ununuzi wa meli mkweche ambayo sasa hivi amewapa kama " offer " taasisi moja nyeti.

..Sasa mtu wa aina hiyo utamuita jina
gani?
Wenzako wsmeweka na kumbukumbu wwewe hujaweka.
 
I'm daily saying raia tunatumika kama mitaji ya kisiasa kwa wana siasa. Zitto kawa mnafiki sn na bendera fata upepo.
 
Cdm nao wanafiki sn. Walisema upupu wa Masha mwingi sn na kutuaminisha raia then kwenda kwao msafi. Tutakua mitaji ya wanasiasa hadi ln?
 
Scandle ndo nini? Jinga kabisa. Si uandike kiswahili tu
Hata Chadema walimtuhumu sana Masha kupitia Chamber Yake kwa Ufisadi Mkubwa wa EPA , Meremeta nk na wakamkabili Jimboni mpaka akaanguka 2010 na wakamtuhumu kwa Ubadhirifu wa Vitambulisho vya Taifa mpaka Masha Nusura alie Bungeni Enzi zile akijitetea lakin ha kushangaza Huyu Huyu Masha ndio anaonekana Mgombea bora zaid wa Chadema kwny EALA na hata alipokataliwa Bungeni akarudishwa tena!

Kama Masha ndio Mgombea bora zaid ki maadili Pamoja na Scandle zote walizotoa Chadema Wenyewe hao waliobaki huko sijui wakoje ki maadili!
 
Nyie Zito hamwezi kumwelewa kwani level zenu ni tofauti sana. Inasaidia nini kuwa na maadili EALA kama huwezi kuyetea hoja kunusuru Tz yetu. Kule ni kama vitani eti ukizubaa unaingizwa mkenge na kujikuta mnaweka sahihi mambo yasiyoeleweka kwa niaba ya nchi. UTAIFA ulihitajika kuliko maadili ambayo ni wachache waloonayo Tz.
 
Nilishangaa sana baada ya kusoma ujumbe wa Zitto akidai anajuta kuzaliwa Tanzania kwa sababu wabunge hawakumchagua Lawrence Masha kuwa Mbunge wa EALA.

Zitto amesahau kuwa miaka tisa iliyopita alimtuhumu Masha akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa anapanga mkakati wa kumfilisi Mzee Reginald Mengi kwa sababu Media zake zilikuwa zinaandika habari za kupinga ufisadi.

Zitto huyu huyu leo eti anajuta kwa nini wabunge hawakumchagua Masha kuwa Mbunge.

Wanasiasa wa Tanzania ni viumbe wa ajabu kweli.

Ninaambatanisha maneno ya Zitto aliyoyasema mwaka 2008 kuhusu Lawrence Masha.

Zitto apasua jina la waziri kijana.
2008-12-07 13:37:18

Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema ana ushahidi kuwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ndiye aliyepeleka hoja ya kumhujumu Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi katika vikao vya juu na kwamba taarifa hizo alithibitisha kuzipata jana.

Akiongea na Nipashe Jumapili jana, Zitto alisema waziri huyo, kwa taarifa alizonazo za kuaminika, alitoa hoja kuwa vyombo vya habari vya IPP vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi na hii inailetea matatizo serikali.

Hivyo, aliomba serikali ipange mikakati ya kumfilisi Mengi, kitendo ambacho kitasababisha kudhoofishwa kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vitashindwa kuendelea kuupinga ufisadi.

Zitto alisema yeye hana sababu ya kumtetea Mengi ila hawezi kunyamaza kuona Mtanzania anayeipenda nchi yake na kulazimika kupinga ufisadi anafanyiwa hujuma.

Aidha, Zitto aliliambia Nipashe Jumapili kwamba, vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kuanika maovu ya ufisadi na vyombo hivyo lazima vilindwe na Watanzania wote wazalendo.

Akijibu hoja ya Mengi iliyotolewa jana kuwa yupo tayari kutupwa jela ikithibitishwa kuwa amedanganya na kumwomba Masha pia aseme kama atakuwa tayari kujiuzulu iwapo ukweli wa maneno ya Mengi yatathibitishwa, Masha aliliambia Nipashe Jumapili kuwa hawezi kujiuzulu kwa sababu nia yake ya kuwaagiza polisi kufanya uchunguzi ni kumlinda Mengi.

Alisema kutokana na taarifa ambayo Mengi aliipeleka kituo cha polisi cha Oysterbay, polisi wameamua kuifanyia uchunguzi ili kuhakikisha maisha yake yanakuwa salama.

``Nia ya serikali ya kuchunguza tuhuma zilizotolewa na Mengi ni kuhakikisha kuwa tunamlinda,`` alisema Masha na kuongeza kuwa hana tatizo na maneno yaliyotolewa na Zitto ili mradi awe na ushahidi.

Amesema, hata kama hawamuamini, basi waupeleke huo ushahidi kwa Rais au Waziri Mkuu kuuonyesha na kama ikibainika kama ni kweli yeye ndiye anayemhujumu Mengi, basi atajiuzulu.

Akasema kuwa yeye hakusema kuwa atamshughulikia Mengi kama alivyonukuliwa kwenye baadhi ya magazeti ila alisema kuwa sheria itachukua mkondo wake kama ikibainika kuwa tuhuma zilizotolewa ni za kweli.

Akiongea na TBC1 juzi, waziri Masha, alisema kuwa kama Mengi ana ushahidi wa tuhuma alizotoa, serikali haitapata shida ya kuhangaika na ushahidi na imemtaka apeleke ushahidi huo.

Kuibuka kwa sakata hilo kunatokana na Mengi kumtuhumu waziri mmoja kuwa ameagiza abambikiwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa ili hatimaye afilisiwe.

Alimtuhumu waziri huyo kuwa amekuwa akimtumia ujumbe wa vitisho kutokana na vyombo vyake vya habari kuwa mstari wa mbele katika kupigia kelele ufisadi.

Akifungua kongamano la kuwajengea uwezo vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa vijana wa chama hicho, John Mnyika, aliwataka vijana kuendeleza vita ya ufisadi na kutokatishwa tamaa na vitisho vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Aliwakumbusha vijana kuwa ni wajibu wao kupigania haki zao kwa manufaa ya taifa na kwamba wanapaswa kukosoana pindi mwenzao anapofanya vibaya.

``Kwa maoni yangu naona kama kauli ya Masha ya kumtaka Mengi awasilishe ushahidi ndani ya siku saba ni ya kukurupuka kwa kuwa mbona nilipotuhumiwa na Mtikila kwamba nimeshiriki kumuua Chacha Wangwe hakusema lolote hadi leo?

Tunashangazwa sana na kauli ya Masha, tulidhani labda angechunguza kwanza kabla hajazungumza na katika hili nawaomba vijana muwe makini na vijana kama hawa na muwakosoe waziwazi,`` alisema.

Alionya kuwa iwapo vijana hawatakosoana jamii itapoteza imani juu ya utendaji wao na kuondoa matumaini ya taifa kuhusu umuhimu wa vijana.

Hata hivyo,alisema vita dhidi ya ufisadi bado ni kubwa kwa kuwa ni asilimia 10 tu imetekelezwa.

``Msibweteke na ushindi huu, ufisadi unaozungumziwa ni wa utawala wa Mkapa, katika awamu ya nne kuna ufisadi kama wa Richmond na Buzwagi kwa hiyo tunapaswa kupambana zaidi,`` alisema.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom