Zitto: Ufisadi ni agenda endelevu

Zitto: Ufisadi ni agenda endelevu

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Tanzania inaendelea kupoteza mabilioni ya fedha za umma kwa sababu ya ubadhirifu mbalimbali. Taarifa za Serikali zinaonyesha kuwa takribani 30% ya Bajeti ya nchi inaishia kwenye mifuko ya watu binafsi. Kashfa mbalimbali za ufisadi zimekuwa zikiibuliwa na kuleta mijadala mikali lakini watu wanaohusika hawachukuliwi hatua zozote.

Jambo la kushangaza ni kwamba ajenda ya ufisadi imefifia katika uchaguzi tofauti na mwaka 2010. Haipaswi kuwa hivi kwani ufisadi ni Kansa inayotafuna Taifa letu. Lazima kuendelea kupambana dhidi ya ufisadi ili kuhakikisha nchi yetu inamaliza umasikini na kujenga dola la maendeleo ( developmental state ).

Juzi nilikuwa Mkoa wa Tabora. Wananchi wa Tabora wanalia Tumbaku yao kutonunuliwa. Tabora huzalisha Tumbaku nyingi zaidi kuliko mikoa yote nchini na kiungiza mapato ya fedha za kigeni zaidi ya usd 315 milioni mwaka 2014.

Hata hivyo 10% ya mapato haya huibwa na vyama vya ushirika kwa kushirikiana na baadhi ya mabenki yanayosambaza pembejeo za kilimo. Ufisadi huu kwenye tumbaku hauzungumzwi ilhali ndio mustakabali wa wakulima wa tumbaku zaidi ya 1m katika mkoa wa Tabora.

Mwezi uliopita Serikali kupitia mfumo wa kuagiza mafuta kwa pamoja ilitoa zabuni kwa kampuni ya Augusta kutoka Switzerland. Zabuni hiyo ilipandishwa bei ( inflated prices ) kwa thamani ya usd 10m sawa na tshs 20 bilioni.

Ndio maana wakati Dunia nzima bei ya mafuta imeshuka hapa Tanzania bei ipo juu kwa sababu wajanja wachache wamepeana Dili la uagizaji mafuta bila kufuata sheria ya manunuzi. Leo kila mwananchi anaumizwa na bei ya mafuta kwa sababu ya ufisadi huu.

Bado skandali za kifisadi zilizoibuliwa huko nyuma hazijapata majibu. Kwa mfano mpaka sasa bado kampuni ya IPTL inauza Umeme TANESCO licha ya Bunge kuazimia kuwa mkataba wake uvunjwe. Bado anayejiita mmiliki wa IPTL aliyetapeli nchi yetu hajakamatwa mpaka Leo na waliochota fedha kutoka benki ya Stanbic hawajatajwa na kufikishwa mahakamani.

Vyama vinatamka kauli nyepesi nyepesi kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi. Ni dhahiri kwamba lazima kurejesha agenda hii kwenye kampeni za uchaguzi kwa kila chama kusema kitafanya nini. Sisi ACT Wazalendo tumeweka kwenye ilani yetu hatua tutakazochukua kupambana na rushwa na ufisadi.

1) Kuipa mamlaka TAKUKURU ya kukamata na kuendesha mashtaka ya rushwa ( power to prosecute ) bila kusubiri kibali cha DPP.

2) Kuanzisha idara ya rushwa kubwa kubwa ( Serious Fraud Office ) ambayo kazi yake itakuwa ni kupambana na ufisadi tu

3) Kutunga sheria ya Miiko ya Uongozi ili kudhibiti rushwa kwenye sekta ya umma na siasa. Mali za viongozi kuwekwa wazi na kukaguliwa na pale kwenye udanganyifu hatua kuchukuliwa ikiwemo kuvuliwa madaraka yao.

Ni imani ya chama chetu kuwa ajenda ya ufisadi itajadiliwa kwa kina kwenye kampeni na hasa kwenye midahalo ya wagombea Urais na viongozi wa vyama.

Nawaomba wananchi wa Kibaha muichague ACT Wazalendo ili iweze kuendeleza vita dhidi ya ufisadi na kusafisha nchi yetu dhidi ya wala rushwa. Naomba kura kwa Habib mchange kama mbunge, madiwani wa ACT wazalendo na mumchague mama Anna Mghwira kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chagueni ACT Wazalendo ili kurejesha nchi yetu kwenye misingi.
 
wanazi ukimaanisha, wanaomchukia au wanaompenda?

Namaanisha mashabiki na wanachama!!

hao niliowataja hapo juu ni wanachama watiifu but hawana mda na chama chao kutwa wako na UKAWA na CCM!!!
 
Tanzania inaendelea kupoteza mabilioni ya fedha za umma kwa sababu ya ubadhirifu mbalimbali. Taarifa za Serikali zinaonyesha kuwa takribani 30% ya Bajeti ya nchi inaishia kwenye mifuko ya watu binafsi. Kashfa mbalimbali za ufisadi zimekuwa zikiibuliwa na kuleta mijadala mikali lakini watu wanaohusika hawachukuliwi hatua zozote.

Jambo la kushangaza ni kwamba ajenda ya ufisadi imefifia katika uchaguzi tofauti na mwaka 2010. Haipaswi kuwa hivi kwani ufisadi ni Kansa inayotafuna Taifa letu. Lazima kuendelea kupambana dhidi ya ufisadi ili kuhakikisha nchi yetu inamaliza umasikini na kujenga dola la maendeleo ( developmental state ).

Mwezi uliopita Serikali kupitia mfumo wa kuagiza mafuta kwa pamoja ilitoa zabuni kwa kampuni ya Augusta kutoka Switzerland. Zabuni hiyo ilipandishwa bei ( inflated prices ) kwa thamani ya usd 10m sawa na tshs 20 bilioni.

Bado skandali za kifisadi zilizoibuliwa huko nyuma hazijapata majibu. Kwa mfano mpaka sasa bado kampuni ya IPTL inauza Umeme TANESCO licha ya Bunge kuazimia kuwa mkataba wake uvunjwe. Bado anayejiita mmiliki wa IPTL aliyetapeli nchi yetu hajakamatwa mpaka Leo na waliochota fedha kutoka benki ya Stanbic hawajatajwa na kufikishwa mahakamani.

Vyama vinatamka kauli nyepesi nyepesi kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi. Ni dhahiri kwamba lazima kurejesha agenda hii kwenye kampeni za uchaguzi kwa kila chama kusema kitafanya nini. Sisi ACT Wazalendo tumeweka kwenye ilani yetu hatua tutakazochukua kupambana na rushwa na ufisadi.

Chagueni ACT Wazalendo ili kurejesha nchi yetu kwenye misingi.

Tatizo ni kuwa CHADEMA wameamua kumuajiri FISADI PAPA EDWARD LOWASSA na kujaribu kumsafisha ingawa inaelekea imeshindikana. Kwa hiyo ufumbuzi wao ni KUACHA KUONGELEA UFISADI MOJA KWA MOJA.
 
Kwani chama pekee cha siasa ni CHADEMA tu?
 
Hahahaha chuki binasfi hizo kuna sela nying za kuongelea Edo ni nan?? Mbona anawapa wakati mgumu hvi??
 
Tatizo la zito anawaza raisi mwaka 2020. Angekuwa sehemu ya mabadiriko leo
 
Kwani chama pekee cha siasa ni CHADEMA tu?

Kwa hivi sasa ni CHADEMA pekee ambacho kimeamua kusimamisha mgombea ambaye ni FISADI PAPA EDWARD LOWASSA.

CCM wamejisafisha kwa kuweka mgombea msafi, wengine hawana nafasi ya kushinda.
 
Una uhakika Magufuli ni msafi?

Kwa hivi sasa ni CHADEMA pekee ambacho kimeamua kusimamisha mgombea ambaye ni FISADI PAPA EDWARD LOWASSA.

CCM wamejisafisha kwa kuweka mgombea msafi, wengine hawana nafasi ya kushinda.
 
Ni Magufuli pekee anayepiga vita rushwa na kubainisha wazi wazi kuwa anaichukia.Akawa hawana agenda hiyo kwa sababu iliyo wazi kwa kuwa na wao wamenunuliwa na fisadi mkuu
 
Tanzania inaendelea kupoteza mabilioni ya fedha za umma kwa sababu ya ubadhirifu mbalimbali. Taarifa za Serikali zinaonyesha kuwa takribani 30% ya Bajeti ya nchi inaishia kwenye mifuko ya watu binafsi. Kashfa mbalimbali za ufisadi zimekuwa zikiibuliwa na kuleta mijadala mikali lakini watu wanaohusika hawachukuliwi hatua zozote.

Jambo la kushangaza ni kwamba ajenda ya ufisadi imefifia katika uchaguzi tofauti na mwaka 2010. Haipaswi kuwa hivi kwani ufisadi ni Kansa inayotafuna Taifa letu. Lazima kuendelea kupambana dhidi ya ufisadi ili kuhakikisha nchi yetu inamaliza umasikini na kujenga dola la maendeleo ( developmental state ).

Juzi nilikuwa Mkoa wa Tabora. Wananchi wa Tabora wanalia Tumbaku yao kutonunuliwa. Tabora huzalisha Tumbaku nyingi zaidi kuliko mikoa yote nchini na kiungiza mapato ya fedha za kigeni zaidi ya usd 315 milioni mwaka 2014.

Hata hivyo 10% ya mapato haya huibwa na vyama vya ushirika kwa kushirikiana na baadhi ya mabenki yanayosambaza pembejeo za kilimo. Ufisadi huu kwenye tumbaku hauzungumzwi ilhali ndio mustakabali wa wakulima wa tumbaku zaidi ya 1m katika mkoa wa Tabora.

Mwezi uliopita Serikali kupitia mfumo wa kuagiza mafuta kwa pamoja ilitoa zabuni kwa kampuni ya Augusta kutoka Switzerland. Zabuni hiyo ilipandishwa bei ( inflated prices ) kwa thamani ya usd 10m sawa na tshs 20 bilioni.

Ndio maana wakati Dunia nzima bei ya mafuta imeshuka hapa Tanzania bei ipo juu kwa sababu wajanja wachache wamepeana Dili la uagizaji mafuta bila kufuata sheria ya manunuzi. Leo kila mwananchi anaumizwa na bei ya mafuta kwa sababu ya ufisadi huu.

Bado skandali za kifisadi zilizoibuliwa huko nyuma hazijapata majibu. Kwa mfano mpaka sasa bado kampuni ya IPTL inauza Umeme TANESCO licha ya Bunge kuazimia kuwa mkataba wake uvunjwe. Bado anayejiita mmiliki wa IPTL aliyetapeli nchi yetu hajakamatwa mpaka Leo na waliochota fedha kutoka benki ya Stanbic hawajatajwa na kufikishwa mahakamani.

Vyama vinatamka kauli nyepesi nyepesi kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi. Ni dhahiri kwamba lazima kurejesha agenda hii kwenye kampeni za uchaguzi kwa kila chama kusema kitafanya nini. Sisi ACT Wazalendo tumeweka kwenye ilani yetu hatua tutakazochukua kupambana na rushwa na ufisadi.

1) Kuipa mamlaka TAKUKURU ya kukamata na kuendesha mashtaka ya rushwa ( power to prosecute ) bila kusubiri kibali cha DPP.

2) Kuanzisha idara ya rushwa kubwa kubwa ( Serious Fraud Office ) ambayo kazi yake itakuwa ni kupambana na ufisadi tu

3) Kutunga sheria ya Miiko ya Uongozi ili kudhibiti rushwa kwenye sekta ya umma na siasa. Mali za viongozi kuwekwa wazi na kukaguliwa na pale kwenye udanganyifu hatua kuchukuliwa ikiwemo kuvuliwa madaraka yao.

Ni imani ya chama chetu kuwa ajenda ya ufisadi itajadiliwa kwa kina kwenye kampeni na hasa kwenye midahalo ya wagombea Urais na viongozi wa vyama.

Nawaomba wananchi wa Kibaha muichague ACT Wazalendo ili iweze kuendeleza vita dhidi ya ufisadi na kusafisha nchi yetu dhidi ya wala rushwa. Naomba kura kwa Habib mchange kama mbunge, madiwani wa ACT wazalendo na mumchague mama Anna Mghwira kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chagueni ACT Wazalendo ili kurejesha nchi yetu kwenye misingi.

Zitto kwa upande wangu mimi ckuamini na ctakuja nikuamini ww ni kikwazo kikubwa cha harakati za kumkomboa mtanzani maskini wa leo hii hivyo hufai na hutatufaa. Ww mwenyewe ni mmbadhilifu (fisadi mkubwa) ulipewa hela na ccm ili uivuluge chadema tena pesa nyingi ukashindwa, Kweli wa tz cjui ni njaa au ujinga, kweli wako watu wanaambatana na Zitto et wanajiita wao Act Zitto huyu huyu ambae anamkataba tayri na ccm kwamba hatakuwa kikwazo sana dhidi ya ccm
 
Akisema Mbowe zitto kafanya hivi na vile nani wa kumpinga???
 
Zitto kwa upande wangu mimi ckuamini na ctakuja nikuamini ww ni kikwazo kikubwa cha harakati za kumkomboa mtanzani maskini wa leo hii hivyo hufai na hutatufaa. Ww mwenyewe ni mmbadhilifu (fisadi mkubwa) ulipewa hela na ccm ili uivuluge chadema tena pesa nyingi ukashindwa, Kweli wa tz cjui ni njaa au ujinga, kweli wako watu wanaambatana na Zitto et wanajiita wao Act Zitto huyu huyu ambae anamkataba tayri na ccm kwamba hatakuwa kikwazo sana dhidi ya ccm
Kwa akili yako kumwelewa Zitto ni kazi sana, Mbaya zaidi hutumii akili yako kuchanganua Mambo maamuzi ya ubongo wako umewakabidhi wanasiasa .

Siku ukija kuanza kuchambua mambo kwa akili yako ndio utamwalewa Zitto.
 
Back
Top Bottom