Zitto: Tumpe Ushirikiano Kamishna Sianga Pamoja na DCEA Katika Kupambana na Madawa ya Kulevya Nchini

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Tumpe Ushirikiano Kamishna Sianga Pamoja na DCEA Katika Kupambana na Madawa ya Kulevya Nchini

Kwa dhati kabisa naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Chama changu kumtakia kila la kheri Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), ndugu yangu Rogers Sianga. Nawaomba Watanzania wenzangu wote tumuunge mkono na kumpa ushirikiano Kamishna pamoja na mamlaka anayoiongoza ili kuhakikisha tunalimaliza au hata kulipunguza tatizo hili la madawa ya kulevya.

Ni matumaini yangu na Chama changu kuwa DCEA watafanya kazi yao kwa weledi na uadilifu. Kauli yake kuwa DCEA watatenda haki na kufuata sheria katika kukabiliana na janga hili ili kuhakikisha nguvu kazi ya Taifa hili, hasa vijana, hawaathiri zaidi ni ya kutia moyo mno.

Mola amtangulie katika mapambano haya.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Dar es salaam
Februari 13, 2017
 
Ushauri wa Mbowe Makonda ameufanyia kazi
Mbona ameshindwa kuwataja?
Aliowataja mwanzoni na wakakutwa hawana tuhuma alishindwa nini kuchunguza kwanza na uchunguzi ukamilike! Nonsense
 
Back
Top Bottom