Zitto: Tumekataa kuwa mateka


Kuwa wanachama wake waliuwawa walisema na picha zilirushwa sana tu humu. Na sio Zanzibar, tu bali hata huku bara watu waliachwa na vilema vya kudumu, na kesi za kubambikiwa.

Ila anachokisema Zito sasa ni kama lugha ya kujihami wasisakamwe maana CDM wamejitoa kushiriki huo uchaguzi kwani matokeo ya 2020 hawayatambui. Hivyo anaposema hawataki kuwa mateka, anamaanisha CDM ndio mateka wa uchaguzi ule.
 
Hivyo anaposema hawataki kuwa mateka, anamaanisha CDM ndio mateka wa uchaguzi ule.
Kwa ivo wanataka kusema wao hawaoni athari za uchaguzi ule pamoja na hao wanachama wao 20 kuawa!? Kwa ivo kukataa kwao kuwa mateka wa Uchaguzi ule wa 2020 hakuwafanyi kuwa mateka wa utawala wa sasa wa CCM?

Yaani wao sasa wanaamini CCM ni wema na hawana tena tabia zile walizokuwa nazo mwaka 2020?
 
Mnafiki mkubwa! unatibuje kwa kuungana na waliokujeruhi! Nimeona na ubunge wa EA mnautaka! Kumbe 2020 mlikuwa na watesi kwa siri ndio maana mnatambua ule uchafuzi Stupid!
 

Anachofanya Zito ni kuhakikisha anacheza na nafasi yoyote CDM wanayoiacha. Anajua fika tatizo la Ccm hasa huku bara ni CDM, hivyo anajua CDM wakipotezea hizo nafasi, CCM wanaweza kumpa yeye na chama chake ili kunulify malalamiko ya CDM ya uchaguzi wa kihuni.

Ama pia anategemea wananchi wakiona CDM wanasusia, basi wanaweza kuenda cha chama chake. Ifahamike kuwa ACT pia imeshafaidika na CUF ya migogoro huko Zanzibar. Kwa sasa anaomba usiku na mchana afaidike na wafauasi wa CDM huku bara. Anajua fika CDM ndio yenye fanbase ya uhakika huku bara.
 
Huyu ZZK ndiye yule yule aliyewekewa fedha Ujerumani na kina kimei wa serikali ya Jakaya ili auvuruge upinzani! A dangerous unobjective nicompoop!
 
Historia inaonesha ni CHADEMA pekee ndiyo imeweza kuwa na wigo endelevu wa wafuasi wake huku Tanganyika. Tatizo Zitto anatamani sana kuwa Rais wa Tanzania lakini huwa kila mara anakosea njia anazotumia kuupata huo Urais.
 
Historia inaonesha ni CHADEMA pekee ndiyo imeweza kuwa na wigo endelevu wa wafuasi wake huku Tanganyika. Tatizo Zitto anatamani sana kuwa Rais wa Tanzania lakini huwa kila mara anakosea njia anazotumia kuupata huo Urais.

Kama CDM wanataka kubaki na fanbase yake, ni lazima Mbowe apumzike kwa sasa kwenye nafasi ya uenyekiti. Naona Mbowe anaanza kuacha brand ya siasa za CDM, na polepole anaingia kwenye siasa za kujinyenyekeza kwa CCM. Hizo siasa za miafaka na CCM awaachie vyama kama ACT, CUF, TLP, NCCR nk, hivyo ndio vinahitaji hisani ya CCM kufanya siasa za ushawishi.
 
Mbowe alikuwa na "Option" zaidi ya hiyo?? Ila ni lazima watu wengine nao waoneshe kuwe wanaweza kuchukua nafasi ya Mbowe hivi sasa. Hofu ya kuwa na watu kama kina Lipumba, Mrema au Zitto ndani ya CHADEMA ni kubwa sana.

Angalau Mbowe kaonesha kwamba anaweza kuhimili hila nyingi tu za CCM.
 
Watu 20 wamekosa haki ya kuishi mbona hatukusikia kesi ya mauaji.kwa hiyo uraisi wa mwinyi una damu lita ngapi??

..Jamhuri / serikali ndiyo yenye mamlaka ya kushitaki kesi za mauaji.

..Kama wana-Act 20 wameuawa, halafu jamhuri haishitaki inabidi tujiulize kulikoni.

..Je, nani amehusika kuua wana-Act? Kwanuni jamhuri / serikali haishitaki?
 
..Jamhuri / serikali ndiyo yenye mamlaka ya kushitaki kesi za mauaji.

..Kama wana-Act 20 wameuawa, halafu jamhuri haishitaki inabidi tujiulize kulikoni.

..Je, nani amehusika kuua wana-Act? Kwanuni jamhuri / serikali haishitaki?
Na jee ACT-Wazalendo wanaona sawa wanachama wao kuuawa?? Mbona wanaongea kama watu kuawa ni jambo dogo sana kuliko wao kuwa mateka wa Uchaguzi wa mwaka 2020?
 

Mkuu huu utetezi kuwa Mbowe tu ndio anaweza kuiongoza CDM ni philosophy ya ajabu sana. Hata CCM kwa sasa wanaendelea kutawala nchi hii kwa shuruti kwa kisingizio cha kwamba hakuna chama kingine kinaweza kutawala.

Ila huwa najiuliza inakuwaje mtu kama Mbowe amekaa miaka zaidi ya 15 akiwa mwenyekiti, kisha hana succession plan?! Matokeo yake ndio haya anakwenda kujilegeza mbele ya CCM, baada ya yeye binafsi kukata tamaa na mapambano.
 
Hujamwelewa...mateka wa 2020 maana yake hawataki kuendelea kuulalamikia huo uchafuzi kuwa amejiunga na hii sijui kamati ya siasa sijui kitu gani kwa ajili ya kuratibu njia bora za maridhiano na siasa.
 
Zitto ni mdini na mkabila sn
 
Mku mm ni mwanaccm lakini kuendana Tozo ninayopigwa ktk Mafao yangu nimejiweka pembeni yaani sina tena chama
Sasa kuhusu swala Mbowe na Chadema nitaelezea kidogo kwa ujumla kinachowachelewesha ni maongezi yanayoendelea pamoja kazi wanayoifanya Kikosi Kazi kwani Chadema wanaonekana wapole kwa sababu ya haya yanayoendelea baina ya ccm na Chadema.
Pia Chadema ni tasisi ambayo tayari inaviongozi na wanachama waliojengwa kiitikadi hata wasiowanachama kwa ujumla ni chama chenye ushawishi mkubwa kwa Watanzania waliowengi.
Chadema ina viongozi Makini kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu mfano Watu kama Heche,Lisu, Lema,yaani inawatu waelewa wasiotegemea dola.
Juzi nilimsikiliza Mzee Msuya akawa ana wazungumzia Chadema ilivyo imara zaidi ccm.
Kwa hiyo wamejitahidi kuijenga Tasisi iliyoimara sana
 
Historia inaonesha ni CHADEMA pekee ndiyo imeweza kuwa na wigo endelevu wa wafuasi wake huku Tanganyika. Tatizo Zitto anatamani sana kuwa Rais wa Tanzania lakini huwa kila mara anakosea njia anazotumia kuupata huo Urais.
Chadema ni chama cha mapinduzi wachaga hakina ishu kile kilianzishwa na wanywa benge

USSR
 
Mbowe ni Mungu wenu mnamtoaje

USSR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…