Zitto tulia, acha upotoshaji, omba msamaha

Zitto tulia, acha upotoshaji, omba msamaha

SIASA za Tanzania kila kukicha zinaibua machizi wapya kwenye siasa na safari hii, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka na kuonyesha uchizi wake hadharani.

Kitendo cha kuandika Twitter na kueneza habari ya uongo kuwa kuna mpango wa wagombea wa Urais wa vyama vya upinzani watakatwa sio jambo la ukweli na linapaswa kukemewa na wanasiasa wote.

Anachokifanya Zitto ni mpango katika strategia ya siasa ya kutengeneza agenda ya kuleta wasiwasi kwenye jamii ili ione kuna uonevu mkubwa utakaowezwa kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) jambo ambalo si kweli hasa ikizingatie ndio kwanza vyama vinachukua fomu za kuwania uteuzi wa Urais.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) inaendesha mambo yake kiutaratibu na haina shinikizo kutoka kwa mtawala au vyama vya siasa na ndio maana kila Chama kimepewa fomu hadharani tena na Mwenyekiti mwenyewe wa tume, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage na hakuna chama kilichopewa fomu ya kificho.

Anachofanya Zitto Kabwe sio siasa za ustaarabu na anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kueleza alipopata hizo taarifa kwa kuwa huu ni uchochezi wa kiwango kikubwa hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu ambao unakuwa na mambo mengi kwa wanasiasa kutumia fursa hiyo kuleta mpasuko kwa jamii.

Tume ya Uchaguzi ni chombo huru kilichoanzishwa mwaka 1993 chini ya ibara ya 74(1) ya Katiba ya nchi ya mwaka 1977. Ambako kwa tafsiri ya kawaida kiko huru na kinajiendesha kwa uwazi na kila mtanzania anashuhudia.

Zitto anapaswa kuona thamani na utu wa mtanzania ni bora na hichi anachofanya sio sahihi kwanza ni matumizi mabaya ya mtandao na pili anafanya uchochezi mkubwa ambao una madhara makubwa kwa taifa hapo baadae.

Embu chukulia mfano, kugombea Urais kuna sifa zake ambazo zimewekwa wazi kikatibu na endapo wagombea waliochukua fomu wakakosa hivyo vigezo anataka walazimishwe kuchaguliwa kuwa marais.

Katiba imeweka wazi sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais katika sheria ya 1992 Na. 4, ambazo zimeanisha sifa hizo. Sasa tujiulize Zitto anataka tuamini hata wasiokuwa na sifa zilizotajwa kikatiba wagombee tu Urais.

Huu ni wakati wa wanasiasa kuchunga ndimi zao hasa wanachosema kiwe na uhakika na si kuzusha taharuki na kuleta wasiwasi kwa umma kwa kuwa wanachofanya si sehemu ya kuleta Umoja bali wako kwa ajili ya mpasuko.

Uchaguzi ni kitendo kinachofanyika kila baada ya miaka mitano, Zitto anapaswa kuiona Tanzania ni bora na inayopaswa kuishi zaidi kwa miaka mingi ijayo kwa kulinda ndimi yake au mkono wake kwa kile anachokiandika kiwe na maslahi kwa taifa.

Uwakala wa mabeberu anaoufanya hauna faida kwa kuwa anataka kuibomoa nchi iliyomkuza na kumsomesha na ninaamini hata mwisho wa safari yake itakuwa Tanzania, hivyo asituharibie nchi yetu nzuri ambao wazee wetu waliipigania kwa nguvu kubwa.
Huyu Philipo amewahi wakati wowote kupata matibabu pale Hospitali ya Mirembe? Huenda aliondoka kabla ya wakati.

Historia hufundisha.
1) Serikali za mitaa ilikuwaje?
2) Je, kuna wakati wowote Tume ya Uchaguzi iliwahi kumwengua mgombea wa CCM kwa sababu yoyote ile?
3) Hivi unaamini kweli wagombea tu wa vyama vya upinzani ndio huwa pekee yao wanashindwa kujaza fomu, wakati kwa kufuatana na utafiti wa TWAWEZA, wajinga wengi wamejaa CCM, inakuwaje wagombea wa upinzani ambako wengi ni walioelemika na vijana, ndio pekee wawe wanakosea kujaza fomu?

Lazima uwe mwendawazimu hasa kuamini kuwa Tume ya Uchaguzi huwa inatenda haki, labda ianze uchaguzi huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We waambie wakose sifa za kugombea halafu uwadanganye kuwa watakuwa salama! Tume ipo kwa mjibu wa sheria vyama vyetu vya upinzani mnaokota okota wagombea waliopoteza sifa za kugombea mkidhani watapata rehema??

Zito jiandae kujiondoa wagombea wako kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa 2020-2025. Haki ndio hiyo sheria lazima izingatiwe.

Mfano kamili ni mgombea uraisi kupitia chadema pingamizi lake lipo wazi ,kilichomuondolea sifa ya kuwa mbunge ni insue ya maadili, je! Mnategemea sheria ya itamwacha tu kisa ni mgombea uraisi??? Jiandaeni kulima michikichi


Tume ipo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na CCM ikiwa na 98% makada wa CCM ??? Jiandaeni kulima bangi Chato
 
Zito huwa ni mlopokaji tuu, anatakiwa awekewe break lasivyo atatupeleka kusikojulikana
 
Kwanii kutahadhalisha ni kosa ? Ccm ,Jiwe tunawajua sana kwa hila na walichofanya mwaka jana uchaguzi wa serikali za mitaa hatujasahau ,hivi nyinyi mapimbi wa CCM mnawaona watu( watanzania)wajinga sana ?
 
Sasa kosa la Mh Kabwe liko wapi?
Wewe unaongea waraka mzima kama nani?
Ukada utakuuwa huo, Punguza Pumzi, Hizi ni siasa.
Na ndo maana si kosa kutuhumukisheria katika siasa
Una upofu wa fikra. Hujaelewa nini hapo? Unataka kila atakaye ondolewa isemekane ameonewa? Kwahiyo sheria zikae pembeni tufuate hisia?
 
Tume huru iko wapi hapo mbona tume ya Warioba iliyoundwa na seriakali ya CCM ilisema tume haiko huru Kwani kuungwa kwa mujibu wa sheria ndiyo kuwa huru lazima uwe na matatizo ya uelewa siyo bure. Zito ametoa angalizo kama kuna mchezo mchafu Tume iache huo mchezo wake italeta vurugu. Kwani kama Sifa ziko kwenye katiba inamaana hiyo tume pekee ndiyo inafahamu katiba vyama havifahamu hiyo katiba hadi vipitishe wagombea wasio na Sifa. Chonde Chonde NEC msitupeleke tusikotaka kwenda.
Nenda kajifunze kujua maangalizo huwa yakoje. Tuhuma zinakuaje angalizo?
 
Tuandikie nyingine kama hii ya Lissu.

Lissu kasema akiibiwa kura kitanuka.

Anaruhusiwa kusema hivyo au akisema hivyo nongwa?
Kitanuka nyumbani kwenu lakini Tanzania siyo bahabara ya majaribio sisi tunafanya kweli tujaribuni muone
 
Kwani kupata habari kwa zito kabla ya Mwandishi ndiyo ukweli wa habari husika?
Haijasemwa kua habari yake ni ya kweli au siyo ya kweli,na sutegemei wewe useme kua si kweli au kweli.
Yeye kasema 'inasemwa'.
 
Back
Top Bottom