Zitto ‘nje’ PAC, Selasini atajwa kuchukua nafasi

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,489
MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, huenda akaondolewa katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo alikuwa Mwenyekiti wake katika Bunge lililopita, Raia Mwema limeambiwa.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameanza kazi ya kupanga wabunge katika kamati mbalimbali wiki hii, kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge, Januari 26, mwaka huu.

Habari kutoka katika vyanzo vya kuaminika vya gazeti hili vimeliambia gazeti hili kuwa Zitto atapangwa katika kamati nyingine ambayo si miongoni mwa zile zinazofahamika kama za kusimamia uwajibikaji wa serikali.

Katika Bunge lililomaliza muda wake, kulikuwa na kamati mbili za uwajibikaji ambazo ni; PAC na ile inayosimamia Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC). Iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyoundwa kwenye Bunge la Tisa chini ya Spika wake, Samuel Sitta, ilivunjwa katika Bunge la 10, chini ya Spika Anne Makinda.

“Spika Ndugai tayari ameanza kazi ya kupanga wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge na kwa uhakika nadhani Zitto hatokuwepo PAC. Spika anaweza kumpanga kamati yoyote atakayoona inafaa.

“Hivi tunavyozungumza, tayari Ndugai amemaliza kuteua wajumbe watakaounda Kamati ya Kanuni ambayo mapendekezo yake yatamsaidia kutengeneza Kamati mpya za Bunge kwa mujibu wa muundo wa sasa wa Serikali ya Awamu ya Tano,” kilisema chanzo hicho.

Ingawa kuna uwezekano wa Ndugai kuirejesha POAC iliyovunjwa na hatimaye kuunganishwa na PAC wakati wa utawala wa Spika Anne Makinda, Raia Mwema limeambiwa hakuna uwezekano wa Zitto kuwamo kwenye mojawapo ya kamati hizo tatu.

Gazeti hili limeambiwa kwamba huenda Zitto akawekwa kwenye mojawapo ya kamati kama ile ya Kilimo, Ardhi na Mazingira au ya bajeti mara Spika atakapomaliza kazi yake hiyo.

Alipozungumza na gazeti hili juzi Jumatatu, Zitto alisema yeye hana taarifa yoyote kuhusu kamati atakayowekwa na Spika ingawa anafahamu si kazi ya mbunge kujipangia kamati anayotaka kuwamo.

Mimi nilikuwa Kigoma Mjini kwa wapiga kura wangu na kusema kweli sijafuatilia mambo ya hizo kamati. Unajua mbunge hapangi atakuwa kamati gani isipokuwa anapangiwa na Spika.

Mimi ni mwanasiasa na niko tayari kufanya kazi kwa bidii katika kamati yoyote ambayo nitawekwa. Hakuna ambaye alidhani ningeweza kuongoza POAC mwaka 2008 wakati nilipochaguliwa na wenzangu kwa sababu nilikuwa kijana sana lakini niliweza.

“Ninaloweza kukuhakikishia ni kwamba popote pale ambapo Spika Ndugai ataniweka nitafanya kazi. Nchi yetu inachangamoto nyingi na popote nitakapowekwa nadhani kutakuwa na changamoto za kutatua,” alisema wakati alipozungumza na gazeti hili.

Raia Mwema halikuweza kuzungumza na Ndugai kwa vile mmoja wa wasaidizi wake alilieleza gazeti hili kuwa alikuwa kwenye mfululizo wa vikao na kwamba pengine angeweza kuzungumza wakati wowote kuanzia leo.

Zitto na PAC
Zitto ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa mbunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka 2005, alianza na Uenyekiti wa POAC mwaka 2008.

Wakati huo, aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alikuwa ameamua kuunda kamati mpya ya Bunge itakayokuwa na kazi ya kusimamia hesabu za mashirika ya umma ya Tanzania.

Mwaka 2012, Makinda aliivunja kamati hiyo iliyokuwa imejipatia umaarufu kwa kuiunganisha na PAC; jambo ambalo baadhi ya wataalamu wa masuala ya uwajibikaji walisema halikuwa na sababu.

Mmoja wa wakosoaji wakubwa wa hatua hiyo ya Makinda alikuwa ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, aliyesema haiwezekani kwa kamati moja kusimamia Serikali Kuu yote na Mashirika ya Umma zaidi ya 200 yaliyo chini ya serikali.

Zilipounganishwa kamati hizo mbili, Zitto alichaguliwa na wabunge wenzake wenzake kuwa Mwenyekiti wa PAC mpya; nafasi ambayo aliishikilia hadi Bunge la 10 lilipovunjwa mwaka jana.

Nani kumrithi Zitto?
Kwenye siku za karibuni, kumekuwapo na taarifa kwamba vyama vinavyounda Ukawa vimekuwa vikifanya jitihada kuhakikisha vinakuwa na udhibiti wa kamati zote za usimamizi wa serikali bungeni.

Chama cha Zitto, ACT- Wazalendo, si sehemu ya Ukawa na kwa vile hakitakuwa sehemu ya kambi rasmi ya upinzani bungeni, mahasimu wake wa kisiasa wanajenga hoja kuwa hastahili kuongoza mojawapo ya kamati za Bunge wanazotakiwa kupewa wapinzani.

Jina ambalo linatajwa kuweza kuchukua nafasi ya Zitto ni la Mbunge wa Rombo, mkoani Kilimanjaro, Joseph Selasini (Chadema).


Chanzo: Rai Mwema.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ahsante kwa taarifa lakini kwa uandishi huu, tarajia maneno makali kutoka kwa wadau.

Naomba upitie tena kusoma ulichokiandika uone kama kinamsaada kisha ufanye marekebisho au uongezee nyama kidogo, hata kama ni muhtasari, hii imezidi.
 
Mkuu ahsante kwa taarifa lakini kwa uandishi huu, tarajia maneno makali kutoka kwa wadau.

Naomba upitie tena kusoma ulichokiandika uone kama kinamsaada kisha ufanye marekebisho au uongezee nyama kidogo, hata kama ni muhtasari, hii imezidi.

Kabisa, na ajifunze kuandika.
 
Huyo Zitto Kabwe aliwekwa lini PAC? Naona kawatuma makuwadi wake kuja kupima upepo hapa thread nzima mnajijibu wenyewe.
Ameshindwa kusimamia bandari makontena yalikuwa yanaibiwa kama hakuna PAC wakati wa uongozi wa Zitto. Mifuko ya jamii aliigeuza shamba la bibi kwa kuchuma fedha na sasa inashindwa kuwalipa wastaafu. Tanesco ameshindwa kuisimamia mgao wa umeme kila siku. Hakuna hata shirika moja lililofanya vizuri wakati wa uongozi wa Zitto PAC. Tunataka mabadiliko, hatutaki wanaofanya kazi kwa mazoea. Zitto na Kikwete hawatofautiani, mi MAJIPU. Tunamtumbua Zitto PAC wakati umefika
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya mashirika ya umma, PAC wakati wa serikali ya nne huenda akaondolewa katika nafasi hiyo.

Chanzo: gazeti la Rai Mwema
Hata asipopewa hii kamati atabaki kuwa shujaa aliyeitendea haki nafasi aliyopewa kwani ameifanya kamati yake kujulikana zaidi pengine kuliko hata kamati zote za bunge.

Hongera raisi mtatajiwa Zito Zuberi Kabwe.
 
Sserikali ya majungu na ya kubebana imeshapita. Sasa hivi huki taka data za ufisadi utafute mwenyewe .sio kama zamani unaretewa kwa sababu ya majungu ya wafanyakazi wa serikalini
 
Hata asipopewa hii kamati atabaki kuwa shujaa aliyeitendea haki nafasi aliyopewa kwani ameifanya kamati yake kujulikana zaidi pengine kuliko hata kamati zote za bunge.

Hongera raisi mtatajiwa Zito Zuberi Kabwe.
So umeridhika tu kwa PAC kujulikana ila kushindwa kufanya kazi,nenda Bandarini na TRA,TRL na hata TANAPA ndo utajua PAC ilifanya kazi au ilicheza
 
Back
Top Bottom