Zitto ninatofautiana na wewe katika hili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto ninatofautiana na wewe katika hili.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Anfaal, Mar 15, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  vyombo vya habari hivi karibuni vimekunukuu ukishauri kuwa, Tanesco iachane na uzalishaji wa umeme na suala hilo wapewe makampuni ya umma ambayo kwa mujibu wako unaamini yanauwezo wa kufanya hivyo (gazeti la Tanzania Daima).
  Nina hakika katika hili ulimaanisha mifuko ya pensheni maana haya ndiyo yamekuwa kimbilio la kila uwekezaji na ndio hasa yanayoonekana kuwa yana faida licha ya ukweli kwamba uwepo wao hutegemea fedha za wananchi.
  Lakini utofauti wangu na wewe umelenga katika maeneo makuu mawili. Mosi, unashau kuwa ufanisi wa mashirika ya umma ni wa kutia mashaka km ilivyo tanesco kwahiyo kinachofanyika ni kuhamisha matatizo kutoka shirika moja kwenda jingine na si kutatua kabisa. Pia km utakumbuka ni hivi karibuni suala la usimamizi wa mifuko hii ndio lilijadiliwa na mifuko hii bado inaonekana inaloop holes nyingi saana za kifisadi, hivi kushauri uwekezaji ufanyike na mifuko hii, huamini kuwa ni sawa na kuidhinisha michango ya wafanyakazi itafunwe yote licha ya kuwa tayari michwa inaitafuna?
  Pili, kuhimiza uwekezaji wa kutumia sekta za umma ni kuupuza uwepo wa sekta binafsi ambazo zenyewe huheshimika zaidi katika kusimamia biashara na ujenzi wa uchumi. Hivi kushauri huko ulikosema, huoni kuwa ni muendelezo wa unfair play kwenye sekta za biashara kwa kuzibana kabisa sekta binafsi ambazo ndio injini za maendeleo?
   
 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Sekta ya binafsi itapata wapi makaa ya mawe/maji?....labda mafuta ambayo ni gharama kubwa! na hizo gharama zitakuwa reflected through tarrifs.Je watanzania tupo tayari kuongzewa gharama za umeme?
   
 3. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  sekta binafsi inawekeza katika eneo hili. Km ilivyo kwenye madini na maeneo mengine. Kwa njia hii hata Watanzania wenyewe wanaweza kujikusanya na kuwekeza pia. Kuhusu bei, ni ushindani na ufanisi (efficiency) ndio zitakazopunguza bei. Hatuna sababu ya kuendelea kutegemea serikali kwenye umeme. Na hili litafanya kupunguza mabilini ya ruzuku yatolewa kila mwaka kwa Tanesco.
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ni bora TANESCO ikatangazwa mufilisi na kuwa winded up, ili iundwe kampuni nyingine ya taifa iliyo clean yenye hisa za watanzania na taasisi credible kama ilivyofanywa CRDB Bank. na ianze kazi kwa upya bila mikono ya wachafu ndani yake.
   
 5. M

  MJM JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nashukuru aliyeleta mada hii muhimu katika mustakabali wa uchumi wa taifa letu.

  Kwanza binafsi nakubaliana kabisa na wale wenye mawazo ya kuipunguia Tanesco mzigo. Ni shirika kubwa sana la Umma ambalo linahitaji kupunguzwa. Ikumbukwe ni wiki hii tu tumesikia uhamishaji wa zaidi ya Bilion 600 kwenda nje ya malengo yaliyowekwa. Ikumbukwe kuwa kwa budget ya Tanzania hicho ni kiasi kikubwa sana lakini kwa ukubwa wa shirika hili ni kidogo sana.

  Suala la ufanisi litaongezeka iwapo kutakuwa na mashirika na makampuni tofauti yatakayoshughulika na uzalishaji wa umeme na kuiuzia Tanesco. Tanesco wabaki kama service providers tu. lakini sikubaliani na wazo la kupewa mashirika ya umma shughuli ya kuzalisha umeme kwa upendeleo bali miundombinu ya uzalishaji wa umeme itolewe kwa ushindani. Ewura wahakikishe makampuni yanayozalisha umeme yanaiuzia Tanesco kwa gharama stahili

  Kwa njia hii Tanesco itaweza kujitegemea na umeme utapatikana kwa wingi na kwa gharama nafuu zaidi
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwa hili sijibu mpaka nifanye utafiti
   
 7. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kinachouwa TANESCO ni political interference yenye malengo ya kifisadi. Mikataba karibu yote ya sasa ya kuzalisha umeme haikuingiwa na TANESCO kwa vigezo vya kibiashara na kiuchumi. Limelazimishwa na wanasiasa kusaini hiyo mikataba. Vipengele vya 'capacity charge' vinavyoilazimisha TANESCO kulipa wazalishaji hata kama hawazalishi umeme ni vya kiuaji. Vikiondolewa kwenye mikataba TANESCO inaweza kuanza kupata faida. Hivi kwa nini baada ya karibu miaka kumi ya kununua umeme wa dharura kutoka kwa makampuni binafsi bila mafanikio bado serikali inang'ang'ania strategy ile ile? Kwa nini isiangaliwe strategy nyingine? Kwa mfano kuna ugumu gani kwa serikali kuiwezesha TANESCO kununua mitambo yake yenywe na hivyo kuepukana na capacity charges? Jibu ni rahisi. Walaji watakosa ulaji. Na walaji tunawajua ni akina nani. Uchumi wa nchi kuparangajika si hoja kwao.
   
Loading...