Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
chadema_clip.jpg


KWA UFUPI

Ataka aelezwe kosa lake, kama kweli aombe radhi hadharani.

Dar es Salaam
Harufu ya kuisha kwa mgogoro baina ya Zitto Kabwe na chama chake cha Chadema inanukia, lakini mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anataka kuwapo na mazungumzo kubaini tatizo ili atakayebainika kuwa alifanya makosa awe tayari kuomba radhi hadharani.

Zitto alikiri bungeni kuwa amekuwa "akimiss" harakati zilizokuwa zikifanywa na vyama vya upinzani wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, harakati zilizozaa Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufurahia kuhudhuria kwa mara ya kwanza vikao vya umoja huo.

Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alipata fursa ya kuingia vikao vya Ukawa wakati wapinzani walipoungana tena kupambana dhidi ya wizi wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow, sakata ambalo liliwekwa bayana na kamati yake baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila kulifikisha bungeni, lakini hakudokeza lolote kuhusu Chadema.

Hata hivyo, mapema wiki hii, Zitto, ambaye Novemba mwaka jana alivuliwa nyadhifa zote kwenye chama hicho kwa tuhuma za kukihujumu, lakini akafanikiwa kulinda uanachama wake baada ya kufungua kesi mahakamani na kufanikiwa kupata amri ya kuzuia asijadiliwe.

Baada ya kuongoza PAC kuchunguza wa tuhuma za Escrow na kufanikiwa kulishawishi Bunge kufikia maazimio manane ya kuwashughulikia kisheria wahusika kwenye uchotwaji huo wa fedha, kumekuwapo na wito kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema kutaka pande hizo mbili zimalizane.

"Kabla ya jambo lolote kufanyika, ili kukata kiu ya Watanzania wanaotaka kuona tunaondoa tofauti zetu, ni lazima kusema ukweli na kila upande kuwa tayari kuomba radhi hadharani pindi ikibainika ulifanya makosa," alisema Zitto alipotakiwa kuzungumzia harakati hizo za kumrejesha Chadema.

"Ukweli wangu ndani ya Chadema ni nini? Lakini mimi ninaona sina kosa ndani ya Chadema. Ninachotaka mimi nielezwe ukweli bila chembe ya shaka makosa yangu mimi ni nini," alisema na kuongeza:

"Nitakuwa tayari kuomba radhi hadharani kama ikibainika nilifanya makosa na kama ikibainika chama kilifanya makosa, nacho kiwe tayari kuomba radhi hadharani na ukweli uwe mbele katika maridhiano.

"Kama hakutakuwa na ukweli itakuwa vigumu kupata mwafaka. Mimi sina tatizo. Nirudie nilivyosema bungeni kuwa nina-miss sana (ninapenda sana kuwamo kwenye) harakati za mageuzi kipindi hiki za kuiondoa CCM madarakani."

Katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto alisema: "Natambua kuwa wapo ambao wangependa kutumia nafasi zao kudhoofisha mapambano ya siasa za demokrasia nchini mwetu. Napenda wanachama wa Chadema na wapenda demokrasia watambue kuwa, mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki.

"Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina; waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu; na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka."

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye binafsi aliguswa na mzozo huo, hakuwa tayari kuzungumzia kumaliza matatizo baina ya chama na Zitto.

"No comment (sina maoni) kwa hilo. Siwezi kuzungumzia suala hili katika media (vyombo vya habari)," alisema Mbowe

Hoja ya kutaka Zitto arejeshwe Chadema imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii na kwa baadhi ya wanasiasa baada ya kuonekana kuwa karibu na viongozi wa chama chake wakati Kamati ya PAC ilipoibua ufisadi wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow wiki iliyopita.

Wakati akihitimisha mjadala wa sakata la Escrow, mbali na kueleza bayana kuwa alifurahia kuhudhuria vikao vya Ukawa kwa mara ya kwanza, Zitto alikwenda mbali na kumpongeza "kwa namna ya pekee" Mbowe kwa jinsi walivyoshirikiana katika sakata hilo.

Zitto alisema hilo lilikuwa ni jambo la kitaifa ndiyo maana wabunge wote wa upinzani bila kujali vyama vyao waliungana.

Alisema mara baada ya sakata hilo kumalizika watu mbalimbali wamekuwa wakizungumzia kufanyika kwa maridhiano ili awe sehemu ya Ukawa na kwamba haoni tatizo.

"Katika hili, kipekee namshukuru kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuniunga mkono katika sakata hili," alisema Zitto.

Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema: "Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote."

Kuhusu kesi aliyofungua mahakamani dhidi ya Chadema, Zitto alisema:

"Nilifungua kesi kwa sababu ya kulinda uanachama wangu, lakini mazungumzo yakifanyika na kujua kosa langu ni nini, nitaifuta kesi hiyo na kuanza upya harakati."

Kuhusu taarifa za kujiunga kwake na chama kipya cha ACT-Tanzania alisema, "Hizo ni taarifa ambazo hazina ukweli wowote."

CHANZO: Mwananchi
 
Inanikumbusha stori ya jamaa mmoja ambaye mke wake huwa anafanya analotaka na mumewe mpole, mwisho akaenda mahakamani kuomba talaka, mumewe akasema vema. Alipoona washikaji nao wamemtosa akataka kurudi kwa mumewe naye kasema imetosha kaa hulo huko.
Pole Zito, nadhani there is no way back, you had played your cards very wrongly
 
Inanikumbusha stori ya jamaa mmoja ambaye mke wake huwa anafanya analotaka na mumewe mpole, mwisho akaenda mahakamani kuomba talaka, mumewe akasema vema. Alipoona washikaji nao wamemtosa akataka kurudi kwa mumewe naye kasema imetosha kaa hulo huko.
Pole Zito, nadhani there is no way back, you had played your cards very wrongly
Anaweza kurudi,hata leo arudi tu.
 
Whatever mtachoamua CCM itaendelea kuongoza.
 
Tena sio tu pekee Zitto kurudi bali tunataka pia na Kafulila, Moses Machali na Felix Mkosamali wote warudi CHADEMA, Siasa ni pamoja na kusamehana kwa maslai mapana ya taifa.

Naomba viongozi wangu wa CHADEMA taifa, wasikie kilio cha sisi wanachama wao.
 
chadema bila zitto hawawezi kujiendesha kabisa hata iweje tulisema kitambo kwamba watampigia magoti tu.
 
Tena sio tu pekee Zitto kurudi bali tunataka pia na Kafulila, Moses Machali na Felix Mkosamali wote warudi CHADEMA, Siasa ni pamoja na kusamehana kwa maslai mapana ya taifa.

Naomba viongozi wangu wa CHADEMA taifa, wasikie kilio cha sisi wanachama wao.

Mkuu umewasahau Shonza, Mwampamba, Hamis, etc
 
Naomba kuweka wazi...

Hakuna aliye juu ya chama.Kuna watu wanatafuta kutaka kuwa maarufu kuliko chama.

Zitto akitaka kurudi Chadema anapaswa kuomba radhi ajutie makosa yake na huu ndiyo msimamo rasmi.

Katiba ya chama iko wazi.Kukipeleka chama mahakamani ni kujifukuzisha mwenyewe ndani ya chama.
 
Naomba kuweka wazi...

Hakuna aliye juu ya chama.Kuna watu wanatafuta kutaka kuwa maarufu kuliko chama.

Zitto akitaka kurudi Chadema anapaswa kuomba radhi ajutie makosa yake na huu ndiyo msimamo rasmi.

Katiba ya chama iko wazi.Kukipeleka chama mahakamani ni kujifukuzisha mwenyewe ndani ya chama.

asante sana mkuu .
 
Watu tuwe serious Zitto anaweza wekea masharti CHADEMA?

Anatapatapa tu.Nyota yake ya kisiasa imeshaisha.Ni politically frustrated.

Uchaguzi mwakani hajui ashike tawi la chama kipi kugombea mwakani.Kila akiangalia vyama vingine vinavyoonekana imara vimeshaungana kuunda UKAWA.Hivyo akitaka kugombea chama chochote lazima apate approval ya UKAWA ambayo anajua kuipata si rahisi.

Hapo ndipo jasho linamtoka kuwa aweza pigwa chini na vyama vyote vinavyounda UKAWA akashindwa kugombea ubunge ndio anajifanya ohhhh nataka kurudi kwa masharti!!!!!!!!!
 
Ugomvi na migongano ni hali ya kawaida kwa binadamu, namsihi ZZK arudi Chadema, Chadema nao wampokee pasipo masharti yyt magumu, sina uhakika km Mbowe atahitaji kugombea uenyekiti tena wa chama baada ya kipindi hiki kupita, hivyo nashauri Zitto aandaliwe kuwa mwenyekiti anaefuata baada ya Mbowe kipindi chake kuisha...kumbuka Zitto ni mwanaharakati na anao wafuasi wengi ndani ya chama
Nawasilisha
 
Tena sio tu pekee Zitto kurudi bali tunataka pia na Kafulila, Moses Machali na Felix Mkosamali wote warudi CHADEMA, Siasa ni pamoja na kusamehana kwa maslai mapana ya taifa.

Naomba viongozi wangu wa CHADEMA taifa, wasikie kilio cha sisi wanachama wao.
Kumbe hawa wote walikuwa CDM? Du basi kuna shida CDM kwa nini wapambanaji wote wanapita pale na kukimbia, nadhani kuna shida ya kuadministration ambayo inatakiwa kuwa addressed
 
chadema bila zitto hawawezi kujiendesha kabisa hata iweje tulisema kitambo kwamba watampigia magoti tu.

Hapa nani kapiga magoti? Kwanza elewa kuwa Zitto bado ni mwanachama wa Chadema na hata huko Bungeni yupo kwa tiketi ya Chadema. Yaliyotokea ni migogoro ya "kifamilia" ndani ambayo inaweza kusuluhishwa au kushindwa kusuluhishika na wenye chama sio Mazoba ya nje kama wewe!
Mbona nyie ndani ya CCM wapo watu kama Tambwe Hiza, Msabaha, Nzazugwano nk waliwaacha na waliporudi mliwapa vyeo ina maana bila waochama chenu kingekufa?
 
Hivi mathalani CHADEMA wakikataa hilo sharti alilowapatia Zitto, itakuwaje kwa Zitto?
 
Mkuu umewasahau Shonza, Mwampamba, Hamis, etc

Tofauti ya Zitto na hawa ni kuwa yeye hajawahi kusimama hadharani na kuitukana Chadema hata siku moja. Hao vijana ni waste product ambayo haifai hata kugusa kwa mkono. Walitumwa watukane basi wacha wakae na matusi yao hukohuko ambako walidhani wamefika ila sasa wamegundua kuwa walitumika kama toilet paper.
 
Back
Top Bottom