Zitto ni mwepesi sana mbele ya Mogha

Zitto ni mwepesi sana mbele ya Mogha

Ndata

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2017
Posts
227
Reaction score
333
Historia ya siasa za Kigoma mjini ni historia tofauti na majimbo mengine ambayo watu wenye umaarufu au pesa nyingi kuwa na uhakika wa ushindi mbele ya wanasiasa wapya, wasio na pesa nyingi au umaarufu mkubwa.

Zitto pamoja na umaarufu wake wote bado hajafanikiwa kuingia kwenye mioyo yetu Wana Kigoma Mjini Kama alivyoingia Kaburu.

Watu walikubali kufa, kufungwa na hata kutengana na familia zao kisa Kaburu ila 2005 walimwambia mzee pumzika.

Zitto anafahamu mwaka 2015 alisaidiwa na CCM, Polisi walimlinda ila aibe ushindi vyema na kwa amri kutoka juu mkurugenzi alimtangaza ikiwa Ni malipo ya kuivuruga Chadema. Wanasiasa was Kariba yake mwaka huu wanekaribishwa CCM na walipewa ubunge kwenye chaguzi za marudio.

Uchaguzi huu Zitto anashindana na watu nyuma ya ushindi wake, 2015 tulimpatia AWIMO free of Charge apange mipango yake uchaguzi huu AWIMO tutaitumia kupanga mipango yetu.

Hawa kina Mogha ndio walikuwa wapanga mipango waliotegemewa na Zitto, Leo wanaenda kujipangia mipango yao.

Ni hakika awamu hii Zitto atakuwa na kazi ya kujenga chama chake tu na sio kutuwakilisha watu wa Kigoma.

Katika wanasiasa waliowahi kuperform chini ya kiwango Kigoma Mjini Zitto ndio wa kwanza.

Mengi tutaongea kwa leo itoshe tuu kusema, tumechoka kuwa wajinga na mwaka huu tunaenda kuwakilishwa na muwakilishi tutaye mtuma sisi na sio wa kuamuliwa na CCM.

 
Zitto sijui CHADEMA aliwafanya nini mlimfukuza akaondoka mkasema kaanzisha ACT kwa mgongo wa Lowassa ambaye baadae mkamchukua nyinyi, sasa hivi naona kuna habari sas kuwa eti alikianzisha kwa pesa ya membe, siasa za Tanzania bwana majungu mengi.

Sasa huyo huyo bado mnasema kuwa mko kwenye mazungumzo naye kuunganisha nguvu sasa hiyo nguvu itakuwaaje kama hata hamuaminiani na bado mnamtuhumu?
 
Yani mogha amshinde zito mnachekesha nyie subilieni mtaona maana zitto mchqwi yule sasa kama uyo mogha anajua kuloga sawa ila vinginevyo mtaona
 
Back
Top Bottom