Ile methali ya kiswahili isemayo "wingi si hoja" siku hizi imepitwa na wakati? Maana watu naona wako bize sana kuelezea jinsi watu "walivyojaa" bila ya kueleza hoja ya watu hao kujaa ni ipi. Zama za utawala wa Warumi watu walikuwa wanajaa uwanjani kuangalia binadamu (wafungwa) wenzao wakipambana na simba. Uwanja mzima ulikuwa ukizizima kwa mayowe!!