Zitto nakuunga mkono!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto nakuunga mkono!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Hunter, Mar 29, 2012.

 1. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Niliposoma mawazo yako kile ulichokinena na kile unachokiamini nakubaliana na wewe uraisi si umri, hii nikutokana na ukweli kwamba wengi wa viongozi wenye umri mkubwa wameonyesha kushindwa na hata wakati mwingine wamepwaya katika nafasi zao. mfano
  Ndugu Mwinyi
  .
  Japo kuwa alikuwa na umri mkubwa ktk uongozi wake alipelekea uchumi kushuka kwa kasi ya ajabu, ikafiki kipindi watu wachache wakawa na pesa kuliko serikali.
  .Aliruhusu soko holela ambalo lilididimiza uzalishaji wa viwanda vya ndani na hivyo kupelekea kufa ka viwanda vingi
  .Aliendesha serikali yake kisela, ilifikia kipindi wauzaji wa dawa za kulevya wakawa ndo mabwana wakubwa, kumbukeni ile kashfa ya mkewe mama siti.

  Ndugu Benny Mkapa
  Kidogo tunaweza sema alifanya kitu japo hakufanya sana
  kumbukeni Wizi na uuzaji mkubwa wa mali za umma alifanya yeye


  Ndugu Jakaya
  .Huyu kiukweli nae kwa umri wake mkubwa, yanayotokea mnayaona na kuyashuhudia
  mfano
  -Kashfa ya mikataba mibovu ya madini
  -Mdororo wa uzalishaji umeme hapo Tanesco
  -Mambo ya Richmond na Dowans
  -Kusafirishwa kwa wanyama huku serikali yake ikiwa bubu na bumbuwazi
  -Safari za kila kukicha ambazo hazina tija
  -Uuzaji holela wa raslimali zetu
  -Kutokuwa na kauli juu ya mawaziri aliowateua wenyewe
  -Rushwa iliyopitiliza

  Sasa leo tunapomsakama Zitto tukumbuke nchi yetu ni moja ya nchi zinazosema zinaamini katika demokrasia, na kama ni hivyo swala la umri halilingani ama halifafanui ubora wa kiongozi
  Raisi wa Burundi si mzee kihivyo lakini anaendesha nchi, tuone ni haki kwa kila mtu kuamua ama kutoa maoni yake na tuhimize katiba hii ya kikoloni iondoke kigezo cha umri kwani viongozi wazee wengi ni viongozi hovyo wasio na uchungu wa kesho kwani hujua watakufa karibuni na hivyo kuendesha serikali kishkaji bila kujali kama kesho na kesho kutwa jamii itawataka waseme walifanya nini.
  Vuta picha fikiria hawa goigoi japo ya umri wao ona wanafanya nini na fikiri iwapo watachaguliwa kuongoza sababu wanakigezo cha umri serikali yao itakuaje
  Mfano
  .Ole sendeka
  .Msekwa
  .Pinda
  .Anne malecela
  .Makinda
  .Sofia simba
  .Mkuu wa mkoa wa arusha
  .Membe
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ukiipata kamusi tafuta neno Paka shume. hivi mkuu kazi ya umamluki ikiisha utafanya kazi gani?
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Kamanda joji!
  Hebu tumsitiri naye huyu!
  Bila shaka ndiyo kageuka kitandani akaja na hii thread!

  Pole sana!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kanywe naye uji! Zito is a simple mInded kind of a person! Just ignore him
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaaaaa!!


  Ama kweli wanainchi wamepichafukwa na mioyo!!
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ndugu umamluki unaujua wewe, simjui Zitto wala sina undugu nae, bt mawazo yake na dhamira yake ndo imenifanya nimuunge mkono! silazima tufanane kimtazamo, ukiona nimepotea niache bt na uhuru wa kutoa mawazo
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huu ni uchafu unaoletwa jamvini na vibaraka wa Magamba.Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kuandika uchafu kama huu?
   
 8. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  The Hunter na Zitto kosa lao ni nini hasa? kama wanataka umri wa kuwa rais uangaliwe upya, mbona ni jambo jema kwa maslahi ya vijana wote? Tuache mawazo hasi kwa mambo yaliyo chanya.
   
 9. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tutaanza kukuIGNORE wewe kwanza,nasi Zitto,wewe nani?umetumwa,sishangai hata manabii walipata tabu sana kwenye familia zao,Zitto usirudi nyuma bro,ni zamu yetu vijana sasa

   
 10. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni katiba tuipiganie ibadilike na kuweza kuwatambua vijana kuwa wapo wenye uwezo na kipaji cha uongozi, katiba iondoe huu ubaguzi. Zito anaweza kuwa kiongozi mzuri endapo atatulia na kubadili aina ya upambanaji alionao, labda 2020 atakuwa ameiva na kujua kutembea anapostahili lakini si sasa.
   
 11. FKM

  FKM Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wakuu JF swala la umri wa kugombea urais haimanishi likilekebishwa tayari Zitto au J. Makamba watakukwaa urais. watalazimika kwanza kupata ridhaa ya kugombea urais kwenye vyama vyao then kupigiwa kura na watanzania. hili jambo nalifananisha na mtanzania mzalendo anapokuja na maada ya mgombea binafsi. watu humshambulia utafikiri akipishwa tu basi yeye anakuwa rais.

  my take: wana JF tuondokane na mtazamo kama wa wabunge magamba Bungeni wanaojadili hoja bungeni kwa kuangalia "nani mtoa maada/hoja au imetoka upande gani" badala ya kuangalia umuhimu wa hoja katika swala zima la maendeleo ya nchi na watanzania kwa ujumla.

  Ni mtazamo chanya wakuu.
   
 12. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,292
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  GO GO GO GO GO ZITTTOOOO, I'M SUPPORTING YOU!

  SASA NI ZAMU YA KIZAZI KIPYAAAA!!!!!

  Wanaokupinga hawana hoja, hawajelewa kile ulichokiandika au hawataki kuelewa, au wanakurupuka tu na nadhani haswaa wanasukumwa na chuki binafs tu!!!
   
 13. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Kuna Zitto wawili. Kuna Zitto wa 2007 aliyekuwa mzalendo kwa taifa lake.
  Pia kuna Zitto wa sasa ambaye ameshanunuliwa na magamba na wanamtumia wanavyotaka.
  Zitto ni kibaraka !
   
 14. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yaani hiyo mifano ya hao wazee uliyoitoa imenichefua na hasa ulipoanza na huyo Sendeka ingawa umenisaidia ukufatia Wassira maana ningedislike the post ingawa kwakweli Zitto for President jamani ni BIG NO
   
 15. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,292
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Wanaokupinga hawana hoja, hawajaelewa kile ulichokiandika au hawataki kuelewa, au wanakurupuka tu na nadhani haswaa wanasukumwa na chuki binafs tu!!!

  Hoja yako ni kibaraka, kwa vipi??!!
   
 16. mathematics

  mathematics JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 3,292
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  ZITTO Wanaokupinga hawana hoja, hawajelewa kile ulichokiandika au hawataki kuelewa, au wanakurupuka tu na nadhani haswaa wanasukumwa na chuki binafs tu!!!

  huyu hata hoja nyepesi hana, anakurupuka au anasukumwa na chuki binafsi tu!


   
 17. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,366
  Trophy Points: 280
  Binafsi hua simkubali sana Zitto, namuona kama mpenda sifa flani hivi, but kwa hili namtetea.
  Zitto kama Mbunge, kutamani Urais sio jambo la ajabu. Lah, hata kama sio Mbunge pia anaweza akautamani Urais pia.
  Tumekua wepesi sana kuingia mkenge na hizi "Modified Titles" za kuuzia gazeti. Mtu kaulizwa kama anafikiri ni zamu ya Vijana kushika nafasi kama ya Urais, mngetaka ajibuje?? Na be kama anafikiri anaweza kuwa Rais ajae angejibuje??
  Je ni yeye tu kakurupuka akasema anahitaji kua Rais na atachukua Form?? Au alikua akijibu swali kua anafikiri anaweza au hawezi???
   
Loading...