Zitto: Najuta kususia bajeti kuu ya serikali!

Zitto: Najuta kususia bajeti kuu ya serikali!

Status
Not open for further replies.
Nimefurahishwa sana kwa maamuzi hayo kwani yanagusa kila mtanzania na naamini kuwa ndio msumari wa mwisho katika kaburi/jeneza la kuizika ccm mwaka 2015!!!!! hongera KAMANDA MBOWE KWA MAAMUZI HAYO....OVER
 
Zito! Kijana huyu ni hazina kibwa sana ya taifa na kwa kweli ameshaharibiwa na siasa chafu za chadema.
Hivi anapoongeleaga vyanzo vipya vya kodi anamaanishaga nini?? Na sisi watanzania ambao hatuna utamaduni wa kulipa kodi anategemea kodi gani itakusanywa toka kwetu kama sio kupitia simu ya mkononi?
Baadhi yenu humu mmekuwa vinara wa kuilaumu serikali kuhusu ugoigoi wake katika ukusanyaji wa kodi, na ninyi ndio haohao mnaolaumu kodi zikikusanywa.
Zito kabwe anatakiwa asifuate mkumbo wa wenzake kwani uwezo wake uko juu sana ukilinganisha na mangi waliomzunguka
 
Wala huna nia nzuri kuhusu hiyo mada ila unakilenga cdm kwa ujumla. Kwa nini husemi wajibu wa speaker na wanasiasa kwa jumla baada ya wananchi kule arusha kurushiwa bomu wakati vikao vya bunge vinaendelea?

Lengo lake ni kuwafikirisha CDM waone kwa kukibaliana na ushauri wa Mbowe bajeti imekuwa na kasoro. Kwani hotuba ya upinzani ilikuwa siri? Huyu ana nia mbaya. Hajui kuwa kutokuwa bungeni ni makubaliano. Yeye anataka kujenga dhana kuwa wabunge wa CDM waliburuzwa kwenda Arusha. Read the whole thing between lines and you will spot this.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nyinyi dawa yeni ni kwa wananchi na si bungeni maana tumechoka na hizi Ngonjera zenu....

Wabunge wa CCM pamoja wa Washirika wanazidi 300, wabunge CDM wako kama 48 sasa unataka kusema hoja iliyoungwa na watu 300 isipite kwa sababu ya Zitto peke yake??? Acha uwongo.

Usinipotezee muda wangu kwa kunifanya nirudie rudie kitu hicho hicho kila wakati, wakati kipo wazi kabisa.

Nimesema, si lazima kwa Zitto kufanikiwa kubadili maamuzi ya bunge, ila mara nyingi hata wana-CCM wanamkubali Zitto kwa kuwa jasiri wa kupiga kelele tu pale bungeni. Kwangu mimi yanapohusu maslahi ya taifa, sina itikadi, na ndio sababu ya kumpongeza Zitto, kwani yeye ameona kosa lake liko wapi kuhusu kususa kwao.
 
Acha pumba....maamuzi yalipigiwa kura hata cdm wangevimba kama chatu.au simba yangepita tu toa upppuuuuzi wako

Huyu hana akili ya kuelewa hilo. Akili zake ni za unafiki na uchonganishi. We have been to school kwa hiyo tunaweza kuona unafiki wako kirahisi sana.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wakuwalaumu siyo mbowe ni wabunge wa ccm waliopitisha hiyo mswada. Tanzania ilikuwa imewakirishwa kwa zaidi ya nusu ya uwakirishi. Hao wote hawakuliona hili. Hii sasa inanionesha kuwa kumbe CHADEMA ndo wawakirishi sahihi kwa nchi hii waungeni mkono kwa harakati zao. CCM na wanandoa wao walikuwepo kwanini usiwaraumu wao na unakuja na shutuma kwa mbowe na wabunge wake wachache hawa? Muwe mnajarubu kufikiria hata nje ya kiberiti na muache kuwa mnaendeshwa na usisiemu. Au mfunguliwe page ya ze comedy
 
Kwa wenye akili wanajua unakivua CCM nguo kwa hii thread japo kwa uwezo wako mdogo unadhani unamchonganisha Zitto na Mbowe. Hata mfanyeje bajati hii imepitishwa na CCM ndio maana hatuwaoni wala kuwasikia wabunge wa CCM wakienda kifua mbele majimboni kama alivyoogiza Ndugai mkawaleze wananchi bajeti ilivyo nzuri. Inakipandisha Cdm chati bila kujua. Huu uzi wa kuondokea hapo Lumumba na buku 7 umeukosea dada yangu.
 
Acheni kulalamikia kila kitu. Kodi lazima ilipwe, tumezidi kusaidiwa na hela za walipa kodi wa nchi nyingine.
Oneni aibu kidogo! ... bill ya simu kwa wenzetu inatozwa hadi city tax.
Cable, umeme, maji, Wi-Fi zote unalipa tax, na wanakuonyesha ni kiasi gani.
Acheni malalamishi.
 
Hata zito angekuwepo bungeni asingelisaidia chochote kwani magamba kwa wingi wao bajeti yao ingepita tu.
Kufuatia maamuzi yaliyo tolewa na Mbowe kwa wabunge wote wa CHADEMA kuacha kuhudhuria vikao vya bunge na kuwaamuru wote waende msibani Arusha, ili kujumuika na makamanda wengine kuwazika wahanga waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu, Zitto amefunguka kuhusu kilichopo moyoni mwake kama ifautavyo;

"Kodi ya Tsh. 1000 kwa mwezi kwa kila kadi uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la wananchi, wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii.

Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na wewe mwenye simu. Kampuni ya simu ina kusanya kwa niaba ya serikali.

Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na bunge, siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kwa kuwa sehemu ya bunge hili.

Ni aibu kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na waziri wa fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya serikali.

Pendekezo lilirudishwa kwa namna gani, kupitia muswaada wa fedha, haieleweki. Ni skandali.

Nasikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili."


My take;

Mbowe unapaswa ujifunze UJASIRI na UKOMAVU unapokuwa kwenye siasa. Hisia zako za kudhani wakienda wabunge wote wa CHADEMA ndio itaonyesha kuwa umeguswa na tukio, basi umepotoka.

Maamuzi yako yamepelekea serikali kufanya maamuzi kandamizi kwa wananchi, kwani wote tunajua kuwa Zitto ndiye waziri kivuli wa fedha, na yeye alikuwa na nguvu katika kusimamia uozo huu usifanyike (hata kwa kupiga makelele tu). Lakini kwa maamuzi ya 'kidikteta' ya Mbowe, taifa limeingia kwenye mzigo mzito.

CHADEMA kwenye hili MMELIANGUSHA TAIFA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom