Kufuatia maamuzi yaliyo tolewa na Mbowe kwa wabunge wote wa CHADEMA kuacha kuhudhuria vikao vya bunge na kuwaamuru wote waende msibani Arusha, ili kujumuika na makamanda wengine kuwazika wahanga waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa bomu, Zitto amefunguka kuhusu kilichopo moyoni mwake kama ifautavyo;
"Kodi ya Tsh. 1000 kwa mwezi kwa kila kadi uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la wananchi, wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii.
Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na wewe mwenye simu. Kampuni ya simu ina kusanya kwa niaba ya serikali.
Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na bunge, siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kwa kuwa sehemu ya bunge hili.
Ni aibu kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na waziri wa fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya serikali.
Pendekezo lilirudishwa kwa namna gani, kupitia muswaada wa fedha, haieleweki. Ni skandali.
Nasikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili."
My take;
Mbowe unapaswa ujifunze UJASIRI na UKOMAVU unapokuwa kwenye siasa. Hisia zako za kudhani wakienda wabunge wote wa CHADEMA ndio itaonyesha kuwa umeguswa na tukio, basi umepotoka.
Maamuzi yako yamepelekea serikali kufanya maamuzi kandamizi kwa wananchi, kwani wote tunajua kuwa Zitto ndiye waziri kivuli wa fedha, na yeye alikuwa na nguvu katika kusimamia uozo huu usifanyike (hata kwa kupiga makelele tu). Lakini kwa maamuzi ya 'kidikteta' ya Mbowe, taifa limeingia kwenye mzigo mzito.
CHADEMA kwenye hili MMELIANGUSHA TAIFA.