Zitto na PAC yake waliteleza?

Duu!! sasa ukawa wamefanya nini mpaka sasa? au ndio wameungana, sijui unaitafsir vp harakati ya kweli? ni ile inayoonekana kwa vitendo kama PAC ifanyavyo au ya kufikirika!!!
 

Lissu si msaliti, hayo a Zitto kuitwa msaliti kwa kutaka kugombea urais umeyaibua wewe hakuna aliyewahi kusema hivyo.
 


Ndugu yangu,sijawahi ona mimi duniani mikataba yenye maslahi kwa nchi ikafichwa kwa chombo chenye dhamana ya kuisimamia serikali.Embu jipe picha US Senate commitee inahitaji mkataba wa kuchimba mafuta Alaska baina ya serikali ya USA na kampuni fulani,halafu mtumishi wa shirika husika akatae kuwasilisha mkataba?Pata picha kitamkuta nini.

Mkuu tusimjadili ZITTO,mada husika nayo ni ufisadi uliokithiri nchini kwetu mpaka maofisa wanakataa kutoa nyaraka kwa kamati ya BUNGE,hichi ni kiburi na dharau ya hali ya juu kwa Watanzania.Hivi jamani mmeangalia uzito wa hili jambo au chuki yenu kwa ZITTO imewafunika kutizama ukweli.Siasa za USIMBA na YANGA zinaimaliza hii nchi.
 

Sangarara,

Labda kwa kumaliza hilo nilipenda UFAHAMU SHARIA ZA TANZANIA ZINARUHUSU MTU KAMA ANAONA HAJATENDEWA HAKI BASI ANA HAKI KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAKE.

Sasa kama viongozi hao wanaona hawakutendewa haki sasa tujiulize kwanini mpaka leo hawajaenda mahakamani.

Tuvute subra tuone kama viongozi hao watakwenda kudai haki yao mahakamani ya kudhalilishwa na bunge.

 

Mkuu Barubaru

Unanichanganya kidogo.

Kwa nini hautaki kuangalia mstakabali wa chanzo cha tukio husika.

PAC iliwakamatisha polisi wakurugenzi wawili wa TPDC sababu walikuwa wanaleta ubishi na kukataa kukabidhi mikataba 26 kwa PAC.

Kwa nini tusisubiri kuangalia kama kwa maamuzi hayo PAC watapatiwa mikataba badala yake tuangalie kama hao jamaa watakimbilia mahakamani kulalamika kwamba wamedhalilishwa?

au lengo ilikuwa kuwadhalilisha na sio kupatiwa mikataba?
 

Nafikiri unajichanganya hapo.

Kumbuka kuwa mikataba ni mali ya Serikali ya JMTz na hilo litabaki kuwa sakata la Serikali na Bunge lake.

Lakin kumbuka waliodhalilishwa kama unavyodai ni viongozi wa TPDC ambao walikataa kutoa mikataba hiyo ima kwa sababu Serikali imewakataza kuitoa au ....

sasa kumbuka wao kama wao binafsi kama waliona hawakutendewa haki na Kamati hiyo ya bunge PAC. Wana haki ya kwenda kudai haki yao mahakamani.

Sasa naomba ulitazame suala hilo katika pande mbili.

Pole sana

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…